SEKIONE KITOJO:- SAUTI ILIYOACHA ALAMA KATIKA HISTORIA YA UTANGAZAJI TANZANIA

Ukiachana na ile fainali ya 1986 kule Shamba la Bibi, mimi namkumbuka Kitojo kwa kunifanya niamini Abubakar Salum ndio mchezaji bora duniani kuliko hata akina Maradona! The guy had a serious hype machine! Yaani akitangaza unahisi Yanga inacheza UEFA Champions League wakati ni kombe la mchangani tu la Afrika Mashariki!
 
It's all about, skills, commitment and the love of the game
 
It's all about, skills, commitment and the love of the game
Sekioni Kitojo ndie aliyetangaza goli la pili la Stella Abidjan dhidi ya Simba pale Shamba la Bibi kwenye fainali ya Kombe la Abiola 1993

Jean Boli Zozo alikua kama anakaanga chapati wakati akimgeuza beki wa Simba Rashid Abdallah Magongo kabda ya kuachia shuti lililotinga nyavuni na kumuacha mlinda mlango wa Wekundu Mohamed Mwameja asijue la kufanya

Kuna kauli aliyoitoa Sekioni Kitojo hadi leo naikumbuka; "Leo tunaiangalia Simba nyoronyoro kabisa" mwisho wa kunukuu

Siku hiyo Mzee Kitojo alikua uwanjani na Mnazi wa Simba akiitwa Mikidadi Mahamoud (R. I. P )
 
Mikidadi Mahmood baadaye akaenda Radio 1
 
Ni kweli alikua chain smoker lakini aliacha kuvuta sigara katika utu uzima wake na akawa swala tano
Nakumbuka ka kihozi kake alikokuwa nako DW anakohoa pembeni na kuendelea kutangaza. Wasikilizaji hawasikii. Alikuwa mshikaji wangu na alinipa vibarua vingi hapo DW si haba, vilinisukuma. Hiyo ni 90s katikati, sijui yupo wapi siku hizi.
 

Very good memory...hawa wazee walikuwa sehemu ya maisha yetu sababu enzi hizo, bila RTD hakuna namna nyingine nyingi za kupata habari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…