Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SEKONDARI MPYA YA KIJIJINI BUTATA YAKARIBIA KUFUNGULIWA
Serikali yetu inajenga sekondari mpya tatu (3) ndani ya Jimbo letu la Musoma Vijijini, na kila ujenzi/mradi umepewa Tsh milioni 584 (Tsh 584m)
Sekondari hizo mpya zinajengwa:
(i) Kijijini Butata, Kata ya Bukima
(sekondari ya pili ya kata hii)
(ii) Kijijini Kasoma, Kata ya Nyamrandirira
(sekondari hii ya amali ni ya tatu ya kata hii)
(iii) Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango
(sekondari hii ni ya pili ya kata hii, na ni ya Kumbukumbu ya Prof David Massamba)
Sekondari mpya 6 kufunguliwa mwaka huu Jimboni mwetu:
Mbali ya sekondari hizo tatu zinazojengwa kwa kutumia fedha nyingi kutoka Serikalini, zipo nyingine tatu zinazojengwa kwa nguvu za wananchi na viongozi wao, nazo ni:
(iv) Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema
(sekondari hii ni ya pili ya kata hii, na imeanza kupokea michango kutoka Serikalini)
(v) Kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu
(sekondari hii ni ya pili ya kata hii)
(vi) Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro
(sekondari hii ni ya tatu ya kata hii)
Butata Sekondari:
Sekondari hii ya kisasa inajengwa Kijijini Butata, Kata ya Bukima. Maabara tatu za masomo ya sayasi, chumba cha TEHAMA, na Maktaba ni miongoni mwa miundombinu muhimu inayojengwa hapo!
Ongezeko kubwa la Sekondari Jimboni mwetu:
Tunazo Sekondari 26 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi (Madhehebu ya Dini ya Katoliki & SDA)
Mwaka huu tunaongeza:
(i) Sekondari sita (6) mpya
(ii) Tunaanzisha High Schools 2 za masomo ya Sayansi
Shukrani:
Wana-Musoma Vijijini tunaendelea kumshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali yetu kwa ujumla wake kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Jimboni mwetu - ahsanteni sana!
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Hatua mbalimbali zilizofikiwa kwenye ujenzi wa Butata Sekondari ya Kijijini Butata, Kata ya Bukima. Sekondari hii inayojengwa na Serikali yetu imepangwa ifunguliwe mwezi ujao, Februari 2025
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumanne, 21 Jan 2025