KERO Sekretariati ya Ajira Ileje wanatunza kanzidata kwa mwaka mmoja tu na kwa nafasi inayojitokeza ndani ya halmashauri ya Ileje pekee

KERO Sekretariati ya Ajira Ileje wanatunza kanzidata kwa mwaka mmoja tu na kwa nafasi inayojitokeza ndani ya halmashauri ya Ileje pekee

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari, mimi dukuduku langu ni kuhusu sekretarieti ya ajira, haifanyi fair kabisa.

Mwanzo nafasi za kazi za halmashauri zilikuwa zinatangazwa na halmashauri wenyewe na kusimamiwa na wenyewe sekretarieti ya ajira ikasema hawatendi haki, wakaamua kusimamia wao tokea mwaka huu mwezi wa pili.

Lakini cha kushangaza nilikuwa kwenye interview moja ya Mtunza Kumbukumbu Ileje mtumishi kutoka Sekretarieti ya Ajira akatutangazia kuwa kanzidata inadumu ndani ya mwaka mmoja tu ni mpaka nafasi ijitokeze ndani ya halmashauri Ileile.

Sasa najiuliza isipojitokeza je? Na kwanini halmashauri wanatufanyia hivi? Mbona ukifanya interview taasisi nyingine hawafanyi hivyo ukifikisha alama za ufaulu kutokana na uchache wa nafasi ukakosa kazi ikijitokeza nafasi taasisi nyingine yoyote unapelekwa huko, why sisi waseme mpaka ijitokeze nafasi ndani ya halmashauri uliyofanya interview? Hawafanyi fair kabisa!

Najiuliza kama walitaka nafasi za halmashauri ziwe chini yao ili watende haki mbona hawatendi haki? Sasa kulikuwa ulazima gani wa hizi nafasi za halmashauri kusimamiwa na wao kama mambo yenyewe ndio haya?
 
Back
Top Bottom