Tetesi: Sekretariet ya Kamati Kuu CHADEMA kufumuliwa

THE FORBES

Member
Joined
Nov 25, 2019
Posts
7
Reaction score
7
Ni taharuki katika viunga vya mitaa ya ufipa, taarifa zisizo rasmi ni kuwa Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama Afrika Mh. John John Mnyika anatarajia kufanya mabadiliko makubwa ya think tanks wa chama katika kipindi kisicho zidi wiki moja ijayo. Hii inatokana na msukumo mkubwa uliopo katika kutimiza strategic mission alizozitangaza kwa waandishi wa habari mapema baada ya uteuzi wake.

Kwa kuzingatia mabadiliko yaliyofanywa katika safu ya makatibu wa kanda katika wiki tatu zilizopita ambapo kati ya makatibu 10 ni watatu tu ndiyo waliosalia yaani Masonga wa Nyasa, General Kaduma aliyekuwa wa Magharibi na Golugwa wa Kanda ya Kaskazini. Hali hii ilitokana na viongozi wakuu kutoridhishwa na utendaji wa makatibu wengi wa kanda.

Watonyaji wangu wananiambia ni wakurugenzi wawili tu ndiyo wanaweza rudi kwenye nafasi zao; Ndugu John Mrema na Dr Bujiku. Yapo majina mapya yanatajwa katika uteuzi hu mpya wengi ni vijana waliokitumikia chama kwa mda mrefu sana. Majina haya ni pamoja na Daniel Naftar na CPA Kitalika. Hata hivyo haijadhibitishwa kama hawa watateuliwa kama wakurugenzi au maafisa katika kurugenzi.

Daniel Naftar anatajwa kuwa kipenzi cha Salumu Mwalimu na Benson Kigaila wakati CPA Kitalika hana ukaribu sana na viongozi hawa wakuu lakini jina lake linatajwa haswa kutokana na jinsi wajumbe wengi wa kamati kuu walivyovutiwa na ufundi katika kujieleza na historia katika nafasi mbili alizowahi kukitumikia chama katika ngazi za chini kabisa.

Joseph Kasambala anatajwa kupewa nafasi y a uafisa katika kurugenzi ya habari na uenezi kutokana umashuhuri wake ndani ya chama taifa na katika mikoa mingi ya Tanzania Bara. Kasambala amewahi kuwa mwenyekiti wa Bavicha Jimbo la Mbeya mjini, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya na Mjumbe wa Baraza kuu kupitia BAVICHA.

CPA Kitalika amewahi kuwa mwenyekiti wa tawi la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), mratibu wa CHASO mkoa wa Arusha na mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa CHASO Taifa mwaka 2015. Msomi huyu wa ngazi ya juu katika fani ya uhasibu na mwanafunzi wa shahada ya pili ya utawala wa Mashirika (Corporate Management) anatajwa kuwa dosari moja ya kutoshiriki katika shughuli za chama mara kwa mara kutokana na kuwa mwajiriwa katika moja ya taasisi ya fedha jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa katika vijana watano walioteuliwa na kamati kuu ya Chadema kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa BAVICHA ni wawili tu ndiyo hawapo katika utumishi wa chama mpaka sasa. Ally Hemed na Gwamaka Mbughi wameteuliwa kuwa Makatibu katika kanda za Pwani na Kati mtawalia. Noel Shao na CPA Kitalika hawapo katika utumishi wa chama. Wajuzi w masuala wanasema pengine ni kwasababu wawili hawa wamekuwa hawajihusishi na shughuli za chama moja kwa moja tofauti na ilivyokuwa kwa Hemedi Ally na Gwamaka.

Wengine wapya wanaotajwa katika safu ya makao makuu ni Regnard Massawe ambaye kwa sasa ni Katibu wa chama mkoa wa Arusha na mtu wa karibu wa mbunge Godbless Lema na mmoja wa waliokuwa watia nia wa nafasi ya uenyekiti wa Bavicha Taifa kwa jina la utani Emeka. Reginard massawe amewahimkuwa rais wa serikali ya wanafunzi katika Chuo cha uhasibu Arusha na Spika wa bunge la vijana Tanzania.
 
Kwahiyo kwako ndiyo taharuki?

In God we Trust
 
Habari murua hii. tumechoka hadithi za SGR.
MATAGA wameimba weee, mara fedha etu za ndani kumbe mkopo tena wa commercial banks kwa riba ya 9% , yaani tumeshindwa kukopa WB kwenye riba ya 2% kwa ubishi wa jiwe, badala ya kuendeleza watu anaendeleza vitu, haya alijenga barabara ya mwenge -morroc kwa bilioni mbili za sikukuu ya uhuru , mika miwili baadae anaivunja ,
 
Ni taharuki katika viunga vya mitaa ya ufipa, taarifa zisizo rasmi ni kuwa Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama Afrika Mh. John John Mnyika anatarajia kufanya mabadiliko makubwa ya think tanks wa chama katika kipindi kisicho zidi wiki moja ijayo. Hii inatokana na msukumo mkubwa uliopo katika kutimiza strategic mission alizozitangaza kwa waandishi wa habari mapema baada ya uteuzi wake.

Kwa kuzingatia mabadiliko yaliyofanywa katika safu ya makatibu wa kanda katika wiki tatu zilizopita ambapo kati ya makatibu 10 ni watatu tu ndiyo waliosalia yaani Masonga wa Nyasa, General Kaduma aliyekuwa wa Magharibi na Golugwa wa Kanda ya Kaskazini. Hali hii ilitokana na viongozi wakuu kutoridhishwa na utendaji wa makatibu wengi wa kanda.

Watonyaji wangu wananiambia ni wakurugenzi wawili tu ndiyo wanaweza rudi kwenye nafasi zao; Ndugu John Mrema na Dr Bujiku. Yapo majina mapya yanatajwa katika uteuzi hu mpya wengi ni vijana waliokitumikia chama kwa mda mrefu sana. Majina haya ni pamoja na Daniel Naftar na CPA Kitalika. Hata hivyo haijadhibitishwa kama hawa watateuliwa kama wakurugenzi au maafisa katika kurugenzi.

Daniel Naftar anatajwa kuwa kipenzi cha Salumu Mwalimu na Benson Kigaila wakati CPA Kitalika hana ukaribu sana na viongozi hawa wakuu lakini jina lake linatajwa haswa kutokana na jinsi wajumbe wengi wa kamati kuu walivyovutiwa na ufundi katika kujieleza na historia katika nafasi mbili alizowahi kukitumikia chama katika ngazi za chini kabisa.

Joseph Kasambala anatajwa kupewa nafasi y a uafisa katika kurugenzi ya habari na uenezi kutokana umashuhuri wake ndani ya chama taifa na katika mikoa mingi ya Tanzania Bara. Kasambala amewahi kuwa mwenyekiti wa Bavicha Jimbo la Mbeya mjini, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya na Mjumbe wa Baraza kuu kupitia BAVICHA.

CPA Kitalika amewahi kuwa mwenyekiti wa tawi la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), mratibu wa CHASO mkoa wa Arusha na mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa CHASO Taifa mwaka 2015. Msomi huyu wa ngazi ya juu katika fani ya uhasibu na mwanafunzi wa shahada ya pili ya utawala wa Mashirika (Corporate Management) anatajwa kuwa dosari moja ya kutoshiriki katika shughuli za chama mara kwa mara kutokana na kuwa mwajiriwa katika moja ya taasisi ya fedha jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa katika vijana watano walioteuliwa na kamati kuu ya Chadema kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa BAVICHA ni wawili tu ndiyo hawapo katika utumishi wa chama mpaka sasa. Ally Hemed na Gwamaka Mbughi wameteuliwa kuwa Makatibu katika kanda za Pwani na Kati mtawalia. Noel Shao na CPA Kitalika hawapo katika utumishi wa chama. Wajuzi w masuala wanasema pengine ni kwasababu wawili hawa wamekuwa hawajihusishi na shughuli za chama moja kwa moja tofauti na ilivyokuwa kwa Hemedi Ally na Gwamaka.

Wengine wapya wanaotajwa katika safu ya makao makuu ni Regnard Massawe ambaye kwa sasa ni Katibu wa chama mkoa wa Arusha na mtu wa karibu wa mbunge Godbless Lema na mmoja wa waliokuwa watia nia wa nafasi ya uenyekiti wa Bavicha Taifa kwa jina la utani Emeka. Reginard massawe amewahimkuwa rais wa serikali ya wanafunzi katika Chuo cha uhasibu Arusha na Spika wa bunge la vijana Tanzania.
Kibatala apewe cheo cha zamani cha Tundu Lisu........Mwanasheria mkuu wa Chadema!
 
Back
Top Bottom