Sekretarieti ya ajira kulikoni?

Determinant

Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
10
Reaction score
4
Tar 14-18 Mei kulikuwa na interview katika fani mbalimbali. Mojawapo zilikuwa za mamlaka ya EPZA watu wameishaitwa waliofuzu usaili huo, lakini cha kushangaza baadhi ya post katika mamlaka hiyo hawajaonyesha watu na hakuna taarifa yoyote. Post hizo ni:

1. Human Resources Manager na
2. Investment Promotion Officer II

Hizo nafasi wamewapa watu juu kwa juu? au hakuna mtu aliefuzu hizo nafasi? ni bora wakawa wawazi vinginevyo hawataaminika. Watu wanatoka mikoani kuja kufanya interview wanapoteza nauli na muda halafu mambo yanakuwa hivyo loo! Wajitazame.
 
Na bado watu watasaga meno sana kushikwa mkono muhimu mzee hawa jamaa wapo na wenyewe kimslahi
 
Niliomba nafasi ya Udereva hata sijajibiwa!
 
Afadhali mkuu umesema. Kwakweli wanavyofanya si vizuri kabisa. unakuta mtu umejiandaa vizuri kwa interview halafu kwenye selection haupo. Inaumiza sana. Sijui kama watanzania tutafika kwa hali hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…