maiyanga1
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 1,340
- 1,832
Nimesikitika sana baada ya kusikia kwamba pamoja na ajira zote za umma, ukiacha waalimu, kusimamiwa na tume ya ajira, eti kuna taasisi za umma ambazo usaili ukifanywa na tume ya ajira, bado nazo zinakuwa na vigezo vyake kuwachukua waliopita katika usaili wa tume ya ajira.
Hili likoje?
Mtu anatajiwa vigezo vya kupata ajira, anavitimiza, anafanyiwa usaili, anafaulu kisha akishafika kwenye taasisi anaambiwa hana vigezo vya taasisi.
Mfano, kuna watu walifaulu usaili wa tume ya ajira kufanya kazi TRA/NSSSF mwezi wa pili, wakapelekwa mafunzo miezi mitatu makao makuu, baada ya kupelekwa mikoani wanaambiwa hawana vigezo.
Matokeo yake:
1. Serikali inakuwa imepoteza pesa kumfanyia mtu mafunzo ambayo hatayafanyia kazi
2. Kwenye hizo taasisi watu wanaingiza watoto/jamaa zao ambao aidha walifeli usaili au hawakufanya kabisa.
Wengi wa wanaofanyiwa hivyo ni watoto wa walala hoi ambao hawana mahali pa kukimbilia.
Ndio tulipofikia watanzania.
TUME YA AJIRA MNAYAJUA HAYA?