Sekta ya Afya siyo ya kufanyia mchezo na mzaha

Sekta ya Afya siyo ya kufanyia mchezo na mzaha

Aramun

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
461
Reaction score
2,213
Nafikiri watu timamu tunakubaliana kwamba @ummymwalimu alikuwa ni ‘mzigo mzito’ katika wizara ya afya, na alikuwa kati ya waziri bingwa wa porojo, uongo na propaganda nyingi, lakini kazi sifuri.

Wametuletea JENISTA. Tunamfahamu vizuri sana. Ni mzigo na chawa mwandamizi. Kazi yake kubwa nyakati zote ni kusifu na kutaja jina la RAIS kama pumzi ya uzima. Amebobea katika idara ya upambe.

Kama ilivyokuwa kwa UMMY (mwanasheria) ndivyo ilivyo kwa JENISTA (mwalimu) ni viumbe wasioweza hata kushika sindano na kufunga gloves ikihitajika. Wanaongoza wizara kwa hisia siyo kitaaluma.

Jenista Mhagama, alitakiwa kuwa mbunge (kazi nyeti Tanzania isiyohitaji wasomi hata kwa ufaulu wa mtihani wa kidato cha pili) siyo kumpa kazi ya kusimamia utekelezaji wa sera za Afya. Hayo ni makosa.

Waziri wa Afya Kenya ni Deborah Mulongo. Debora Mulongo ameitwa na Rais William Ruto kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO). Kitaaluma, Debora Mulongo ni dakari (Medical Doctor) kwa miaka zaidi ya 15.

Nani kamueleza RAIS Wizara ya Afya inahitaji ‘bootlikers’ ambao watakuwa na kazi ya kumwaga sifa na pongezi kwa RAIS? Hii haitakiwi kuwa wizara ya kufanyia propaganda na mizaha. Hii ni wizara ya Afya.

Sekta ya afya siyo ya kufanyia mchezo na mzaha. Marekani, katika bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024, Wizara ya Afya ndiyo inaongoza kwa kutengewa fedha nyingi. Imetenga $1.7 trilioni.

Bajeti ya Serikali ya Marekani ni $6.9 trilioni. Vipaumbele ni uimarishaji wa matibabu na Usalama wa Jamii, kurejesha Mikopo kamili ya mtoto, na kuongeza ufikiaji wa huduma za afya na dawa za bei nafuu.

Bajeti ya Serikali ya Tanzania mwaka wa fedha 2023/2024 ni Sh44.38 trilioni. Bajeti ya wizara ya afya kwa mwaka 2023/24 ni Sh1.2 trilioni. Jina la SAMIA likitamkwa mara 46 katika bajeti ya serikali

Serikali ya Tanzania inatenga fedha nyingi kulipa madeni ya serikali na matumizi na vitafunwa, kuliko kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa watanzania. Serikali ya CCM katili sana.

Brigedia Mtikila, MMM.
 
Wana wasiwasi gani wakati wao wanaenda kutibiwa India.
 
Nafikiri watu timamu tunakubaliana kwamba @ummymwalimu alikuwa ni ‘mzigo mzito’ katika wizara ya afya, na alikuwa kati ya waziri bingwa wa porojo, uongo na propaganda nyingi, lakini kazi sifuri...
Aiyewateua ana CV ipi? particularly education-wise/acdemic, tuanzie hapo
 
Kwani hii nchi haina miongozo ya kuteua viongozi hususani hao mawaziri? Kama miongo hyo haipo basi ni muda mwafaka sasa wa kuiweka mapema kabisa.

Yaani wizara iwe na waziri angalau mwenye taaluma inayoendana na mahitajio yake.
 
Huyu mpya ndo bogus kabisa
Mi kuna vitu vinanishangaza hivi mtu anakuwaje waziri wa kitu fulani ikiwa hana taaluma ya hiyo kitu?
 
Back
Top Bottom