daniel mgomo
New Member
- Apr 21, 2015
- 4
- 13
SEKTA YA AFYA YAVAMIWA NA “VIWAVI JESHI”
Kila binadamu anahitaji kuwa na afya njema ili aweze kuishi maisha marefu yenye furaha na fanaka. Afya maana yake ni hali ya kutokuwa na ugonjwa kimwili, kiakili, kiroho na kijamii.
Wizara ya afya ndio pekee iliyopewa jukumu la kusimamia afya za Watanzania kwa kutoa mwongozo wa tiba sahihi, kinga sahihi, lishe sahihi na mazingira bora.
Taasisi za dini zimeruhusiwa na serikali kuendesha kazi zao ili wafuasi wao waweze kuishi maisha ya kiroho yenye amani na upendo, pia kuwafanya watu wawe na hofu ya Mungu ili waache kutenda dhambi. Kwa mintaarafu ya waraka huu nitachukua fursa hii kujadili kwa kina changamoto kuu tu chache zinazotishia uhai na maendeleo ya afya kwa Watanzania. Aidha changamoto hizi zinafanywa kwa makusudi, bahati mbaya au kwa kutokujua. Mimi mwandishi wa makala haya kwa jina la mtandaoni naitwa Tyupa. Tyupa ni jina langu la utani la Kinyiramba lenye maana ya baba lao. Tyupa ni neno la majigambo linalotumiwa na wanaume pale inapodhihirika kuwa amewazidi wenzake kwenye tukio fulani. Inaweza kuwa mitihani shuleni, michezo ya ndondi, riadha, ugomvi halisi, utajiri n.k.
Mimi nina fani ya udaktari wa binadamu kwa kiwango cha Stashahada (Diploma In Clinical Medicine). Nina uzoefu wa kufanya kazi hii kwa zaidi ya miaka arobaini katika vituo vya ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya Zahanati (Dispensaries),Vituo vya Afya (Health Centers), Hospitali za Wilaya (District Hospitals) na Hospitali binafsi ya Consolata Sisters.
Katika utumishi wangu nimejifunza mambo mengi sana kutoka kwa watumishi wenzangu niliofanya nao kazi pamoja. Pia nimejifunza mengi kutoka kwa wagonjwa wenyewe niliokuwa nawahudumia. Lakini pia nimejifunza na kuona madhaifu na kasoro zinazotoka moja kwa moja wizara ya Afya yenyewe. Lengo la makala haya kama nilivyosema awali ni kubaini kwa ujumla changamoto muhimu tu ambazo zinaendelea kuzorotesha maendeleo ya afya kwa Watanzania kwa njia moja au nyingine. Changamoto nitakazozijadili nitaziweka katika makundi maalum. Makundi hayo ni serikali yenyewe, wahudumu wa afya, wagonjwa wenyewe, taasisi za kidini, tiba mbadala na waganga wa jadi. Makundi yote haya yapo ndani ya sekta ya afya kwa malengo chanya au hasi ya kupambana na adui maradhi. Kuna maadui watatu wakubwa wa taifa hili ambao ni maradhi, ujinga na umaskini. Lakini adui maradhi ndiye pekee ambae makundi yote nilioyataja yameivamia sekta ya afya kama viwavi jeshi kwa lengo la kujipatia pesa zaidi kuliko kumtokomeza adui kwa kupambana kwa kutumia njia stahiki.
Changamoto ya kwanza ni hii ambayo inahusu viongozi wa juu wa wizara ya Afya. Inaonekana kama wizara ya Afya inalegalega katika suala zima la kuzalisha wahudumu wa afya waliokamilika kimaadili na kitaaluma. Wahudumu wengi wa afya wanaonekana kutokuwa na maadili ya kazi. Wengi wanaonekana kujihusisha zaidi na vitendo vya rushwa, hila, uzembe, ubaguzi, na kutowajibika vizuri kazini. Ref. Muhimbili kitengo cha Moi Madaktari walikata mguu wa mgonjwa badala ya mkono kimakosa.
Wizara ya afya inapaswa sasa kuandaa mitaala mizuri ya masomo ili iweze kuzalisha wahudumu wenye taaluma nzuri na wenye kuwajibikaji ipasavyo katika utendaji wa kazi zao. Kwa wale wanaokiuka taratibu za utoaji huduma serikali iwachukulie hatua kali za kisheria. Changamoto nyingine ambayo ipo mikononi mwa serikali katika kutatuliwa ni kuhusu mawakala wanaoingiza dawa nchini ambazo serikali imeziruhusu kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu ziagizwe na kusambazwa na kampuni ya MSD (Medical Stores Department).
Mawakala hawa wamekuwa na tabia mbaya ya kuwaingilia madaktari na kuwashawishi waandike dawa nyingi kwa wagonjwa. Ushawishi huu huambatana na kuwapa madaktari pesa na zawadi zingine mbalimbali. Mtego huu hata mimi umenipata hapa nilipo, ninazo zawadi nyingi za mawakala tulizokuwa tunapewa nikiwa kazini. Wakati mwingine tulikuwa tunapelekwa kwenye hoteli za gharama kubwa ambako huko tulikuwa tunalishwa na kunywa kadiri ya uwezo wetu na mwisho tunalipwa pesa. Sasa ukifika kazini ni lazima ulipe fadhila kwa kuandika dawa nyingi kwa wagonjwa kama ambavyo wao wanataka. Matokeo haya ndio tunayoyaona leo ambapo wagonjwa wanaandikiwa lundo la madawa ambayo mengine hayana maana yoyote. Kuwahonga madaktari ili wakiuke taratibu za kutoa dawa sahihi kwa wagonjwa ni kosa la jinai.
Changamoto nyingine inayotokana na uzembe wa wizara ya Afya ni kushindwa kuagiza na kusambaza baadhi ya dawa muhimu. Kwa muda mrefu serikali imeshindwa kuagiza na kusambaza dawa ya Podophiline 25% Ointment inayotibu ugonjwa nyemelezi wa VVU aina ya “genital warts” zinazotokana na virusi vingine vya Human papilloma virus. Hivi ni viotea sehemu za siri vinavyowakumba wagonjwa wengi wa VVU. Lakini viotea hivi vinaweza pia kutibiwa kwa kuunguza na umeme (Electrical cauterization). Lakini njia hii hufanyika kwa nadra sana na katika utumishi wangu kazini sijawahi kuona aina hii ya tiba ikifanyika.
Sasa tuangalie changamoto zinazoletwa na taasisi za dini ambazo hutoa tiba za kiimani ( Faith Healing ). Kuna manabii na mitume wengi hivi sasa ambao wanadai kuwa na uwezo wa kuponyesha magonjwa kwa njia ya miujiza. Wafuasi wa dini mbali mbali wamekuwa wakimiminika kusaka aina hii ya tiba ya miujiza. Miujiza hii zamani tulikuwa tunaoneshwa mashuleni kama sanaa ya mazingaombwe. Mtu analishwa maharage lakini anatapishwa nyembe. Ref. (1). Nabii Mwamposa amkojolesha mtu mjusi. (2) Nabii Suguye amtapisha mtu nyembe 1.Ref. www.facebook.com - Nabii Mwamposa amkojolesha mtu mijusi.
2. Ref. https:// YouTube. be/ytlgjLMOpAhU - A lady vomited Razor in the church
Manabii au mitume hawa wanahubiri neno la Mungu kwa wafuasi wao ambapo hili ni jambo jema. Lakini nyuma ya pazia kuna biashara kubwa hufanyika kwa lengo la kujipatia fedha zaidi kwa manabii au mitume hawa. Manabii wengi wanadai kuwa na uwezo wa kutokomeza magonjwa yote kwa njia ya miujiza, kutoa nuksi na mikosi, kufufua watu na kutoa baraka. Biashara inayofanyika ni watu kuuziwa maji , mafuta vitambaa, leso, keki kwa kwa kubwa kwa imani kwamba bidhaa hizi zimewekwa wakfu kwa hiyo zina upako mtakatifu. Wafuasi wanaamini wakishakuwa na vitu hivyo inakuwa vigumu kwao kupatwa na magonjwa na shida zingine. Magonjwa yanayotajwa kutokomezwa kimiujiza ni VVU, Corona, Saratani, TB, Ukoma, Ugumba n.k. Lakini kisayansi inajulikana wazi kuwa magonjwa yote yatokanayo na vimelea tiba ya kiimani (Faith healing) haiwezi kuwa tiba ya kutokomeza magonjwa hayo.
Isipokuwa magonjwa ya kisaikolojia zaidi ndio yanaweza hutoweka kwa tiba ya kiimani ( Faith healing ) Hivyo hospitali itabaki kuwa sehemu pekee ya uhakika kwenda kutatulia kero za magonjwa yote. Wizara ya Afya au Serkali inahitaji kutumia mbinu mbadala ya kuwakabili watu hawa kwa sababu wao wanaamini serikali haiingilii mambo ya dini hata kama watateketeza wafuasi wao wote kwa moto kama alivyofanya Kibwetere kule Uganda.Ref. Nabii Mwamposa kule Moshi alisababisha vifo vya watu ishirini (20) lakini serikali haikumchukulia hatua yoyote kwa sababu serikali haiingilii dini. Ref 1. https//youtube.be/YvWsu 7qa13w .2.Mh. Gwajima na kanisa la ufufuo na uzima –You tube- Gwajima afufua mtu
Waganga wa tiba asilia nao ni changamoto kubwa inayotishia uhai wa maendeleo ya afya kwa Watanzania. Waganga wa jadi wengi wamekuwa wanajinadi kuwa na uwezo wa kutibu kwa ufasaha kama ambavyo waponyaji wa kiimani wanavyodai. Wapo waganga wachache wa tiba asili ambao kwa hakika wanaweza kuponya baadhi ya magonjwa lakini walio wengi wamevamia sekta ya afya si kwa lengo la kutibu bali ni kutengeneza pesa. Hasara wanayoileta hawa watu wa tiba ya jadi ni kule kuchelewesha magonjwa hadi yanafikia hatua ngumu ya kutibiwa hospitalini.
Serikali kwa hili pia inapaswa kuangalia ni waganga gani wa jadi wanastahili kutoa tiba hii.Lakin pia waganga wa jadi huchonganisha watu na kusababisha ugomvi.
Tiba mbadala kama walivyo waganga wa jadi nao wamevamia sekta ya afya kwa malengo hasi. Hawa wana mashine za bandia wanazotumia kupima wagonjwa. Mashine hizi hazipatikani mahospitalini na zinapima magonjwa yote yaliyopo mwilini kwa kushika na mkono tu. Halafu msomaji anaetafrisi magonywa hayo hana elimu yoyote ya uganga. Hapa sasa haijulikani anayajuaje magonjwa anayotafsiri na jinsi anavyotoa dawa wakati hana hiyo elimu. Dawa zao zina gharama kubwa na wagonjwa wengi hushindwa kumudu. Tiba mbadala nao wakiachwa waendeshe shughuli zao kiholela wanaweza kuleta madhara kama yale yaliyopo kwenye tiba ya kiimani (Faith Healing), Wagonjwa watakuwa wanacheleweshwa kupata tiba sahihi mahospitalini pamoja na kutozwa fedha nyingi kwenye huduma ambayo haijulikani inafanya kazi kivipi. Serikali inapaswa kukaa chonjo na watu hawa.
Changamoto ya mwisho ya kujadiliwa kwenye makala haya ni kuhusu ugonwa wa UTI. Huu ni ugonjwa unaojulikana mno na Watanzania lakini ukiwa ni ugonjwa unaoongoza kwa kutokueleweka vizuri na wagonjwa na hata kwa watoa huduma ya afya wenyewe.
Wagonjwa wengi wanaamini kuwa huu ni ugonjwa mpya na wa hatari zaidi unaoshambulia watu ovyo na kuwaletea mateso. Lakini ukweli ni kwamba huu ni ugonjwa wa kawaida na ulikuwepo tangu enzi za Sodoma na Gomora.
Wagonjwa wengi wanaofika katika vituo vya matibabu wakiwa na dalili nyingi mbali mbali huwalazimisha madaktari wawapime mkojo kujua kuwa wana maambukizo ya UTI au la. Inawezekana kabisa katika dalili zote hizo alizozitaja mgonjwa ukakuta hakuna hata moja inayohusiana na ugonjwa wa UTI. Daktari yeyote makini hawezi kumwandikia mgonjwa vipimo ambavyo havirandani na dalili alizosimulia mgonjwa.
Kwa ufupi hii ni taarifa sahihi zaidi inayohusu ugonjwa wa UTI.
UTI ni kifupi cha maneno ya kiigereza ya Urinary Tract Infection, kwa Kiswahili ni maambukizi kwenye njia ya mkojo. Njia ya mkojo inaanzia kwenye figo (Kidneys) ambako ndiko mkojo unakotengenezwa. Baada ya figo kufuata mirija miwili ya Ureters ambayo ndiyo huingia kwenye kibofu cha mkojo (Urinary Bladder) na mwisho kuna mrija mmoja unaotoa mkojo nje ujulikanao kama Urethra. Ref. Picha 2
Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) yanasababishwa na vimelea vingi vya aina mbalimbali.
Vimelea vya magonjwa ya zinaa ndivyo vinavyoongoza kusababisha UTI ingawa kuna dhana potofu ambayo imejikita kwenye vichwa vya wagonjwa na hata kwa wahudumu wa afya kuwa E. Coli ndio vimelea nambari moja vya kuleta UTI. Vimelea vingi vya magonjwa ya zinaa ni kama ifuatavyo:- Kisonono, Chlamydia Trachomatis, Trichomoniasis, Fungus, Herpes virus simplex type II na Mycoplasma.
Ref. medicinet.com - Tämä WWW-sivu on myynnissä. - medicinet Lähteet ja tiedot.
Vimelea vingine ni vile ambavyo havienezwi kwa njia ya kujamiiana kama E. Coli Klebsiela pneumonia, Staphyloceocus saprophyticus, Enteroccocus faecalis na Proteus spices. Kuna vimelea vya kichocho cha kibofu cha mkojo (Schistosoma haematobium. Hiki ni kichocho kinachoathiri kiungo cha mkojo cha kibofu kwa kiwango kikubwa. Shule nyingi za msingi utakuta karibu robo ya wanafunzi wanakojoa damu. Hata watu wazima wanaoshughulika na kilimo cha mpunga mara nyingi nao hukumbwa na ugonjwa wa kichocho cha kibofu. Ref. Merck Manual of Medical Information (Home edition) By Drs, Robert Pekow, Dr Mark, Dr Robert Bogin na Dr Andrew Flecher page 620 - 621
Pamoja na kwamba inajulikana wazi kabisa kichocho cha kibofu cha mkojo kinashambulia moja ya viungo vya mfumo wa mkojo na kusababisha UTI, baadhi ya wataalamu wa afya na wagonjwa wenyewe wanaona kichocho sio ugonjwa unaoleta UTI, jambo ambalo si kweli. Vimelea vya Leshimania ambavyo husambazwa na mdudu aina ya sandfly husababisha ugonjwa wa ngozi. Lakini vimelea hivi vya Leshmania vinaweza kusafiri hadi kwenye viungo vya ndani vya mwili wa mwanadamu hususani figo (Visceral leshmaniasis). Dalili za UTI iliyoletwa na Leshmania ya kibofu cha mkojo ni kukojoa damu, maumivu wakati wa kukojoa na kukojoa protini. Ref.1. PubMed.gov
2. https//www.ncbi.nlm.gov - pcm
Njia za kueneza UTI zilizo muhimu ni kwa njia ya kujamiana zaidi. Hapa ndipo penye shida na utata mkubwa kwa sababu wagonjwa na baadhi ya wataalamu wa afya wanaamini kwa kiwango kikubwa kuwa UTI inaenezwa zaidi kupitia vyoo vya kuchangia (Public toilets). Dhana hii ni potofu sana kwa sababu mirija ya mkojo ya watu haigusi makalio ya choo (toilet seats) wakati wa kujisaidia. https://www.fortishealthcare.com/blog/public-toilets-uniranry-infection/
Sababu nyingine ya kutoenezwa kwa UTI kwa njia ya choo ni kwamba vimelea vya magonjwa ya UTI vinapokuwa mwilini vinazaliana na kukua kwa msaada wa uwepo wa mazingira rafiki yaani Ph sahihi. Ph ni Potential hydrogen yaani ni uwepo wa acid na alkaline vitu ambavyo husaidia viumbe hai vyote kuzaliana na kukua vizuri.
Vimelea waliopo mwilini wakipelekwa chooni kwa njia ya kujisaidia kamwe haviwezi kuishi chooni au kwenye makalio ya choo (Toilet seats) kwasababu Ph ya hapo chooni ni tofauti kabisa na Ph ya mwilini, kwa hiyo vimelea hao watakufa kirahisi bila kuleta madhara yoyote. Ni sawa kwa mfano huu, huwezi kuotesha na kustawisha zao la karafuu Dodoma kwa sababu Ph ya Dodoma ni tofauti na Ph ya Zanzibar.
Dalili kuu za UTI zimegawanyika katika makundi mawili muhimu ambazo ni dalili za mwanzo ambazo ni kali (Non Complicated au Acute) ambazo ni kukojoa mkojo mchafu wenye damu, usaha, mkojo kuwa wa njano na harufu mbaya. Dalili za baadae (Complicated) ni kupata maumivu chini ya kitovu, homa au maumivu ya viungo. Lakini ieleweke wazi kuwa dalili hizi zinaweza kuwa za magonjwa mengine pia.
Vipimo vinavyotumika kupima UTI viko vingi, kuanzia vidogo hadi vikubwa. Kuna kipimo cha mkojo cha urinalysis na urine for microscope. Kwenye vipimo hivi unaweza kuona chembechembe za damu, chembechembe za usaha, vimelea vya kichocho, Trichomonas Epethilial cells, Yeast cells, Shahawa na vinginevyo. Mkojo wenye shahawa waweza kuwa wa mwanamke au wa mwanaume aliyefanya zinaa muda mfupi kabla ya kwenda kupima. Kuna vimelea vingine ni vidogo zaidi ambapo ni lazima utumie vipimo vya gram stain na culture. Vipimo vikubwa vyaX-ray, Ct scan, MRI na Ultrasound hutumika kuangalia uharibu uliotokana na vimelea wa UTI kushambulia viungo vya mwili hususani vya mfuno wa mkojo (Urinary system).
Matibabu ya UTI mara nyingi hutegemea na kujulikana kwa aina ya kimelea kilichohusika baada ya vipimo. Lakini dawa za Antibiotic aina tofauti tofauti kutumika kama vile Doxycyline, Ampiclox, Azithromycine, Ciproflaxine na zingine nyingi. Dawa zingine zaweza kuwa ni za kichocho kama vile Prazequantel au za Leshimania. Pia unaweza kutumia Metronidazole kwa vimelea vya Trichomoniasis.
Jinsi ya kujikinga na UTI, kwanza ni lazima elimu ya afya kwa umma juu ya UTI itolewe kwa ukamilifu ili kuondoa dhana potofu. Watu wajue kwanza vizuri UTI ni kitu gani na inasababishwa na nini na jinsi inavyoenezwa kwa usahihi. Watanzania wafundishwe kuwa kujamiana ndiyo njia pekee kubwa ya kusambaa kwa UTI tofauti na sasa wanavyoamini kuwa matumizi ya vyoo vya kuchangia (Public toilets) kuwa ndiyo njia pekee kubwa ya kuenezwa kwa UTI.
Mwisho ni matumaini yangu kuwa Watanzania watazinduka kutoka gizani baada ya kuziona vizuri changamoto kuu katika sekta ya afya kama nilivyobainisha kwenye makala haya.