Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
Mwanamke aliingia kwenye bucha ya nyama na kumuuliza muuzaji,
"Una kuku?"
Muuza nyama akafungua friza na kutoa kuku pekee ambaye ndiye alikuwa amesalia akamweka kwenye mizani. Mizani ikasoma Kilo 1.5.
Yule mwanamke akamtazama kuku kisha akauliza
"Hakuna mwingine ambaye walau ana kilo mbili?"
Muuzaji akamrudisha kuku kwenye friza kisha akamtoa tena yuleyule na kumuweka kwenye mizani. Kwa ujanja wa hali ya juu akakandamiza mizani kwa kidole gumba na mizani ikasoma kilo 2.
"Safi sana" Alisema yule mwanamke.
"Nitachukua kuku wote wawili"
Hadi sasa kichwa cha muuza nyama bado kimo ndani ya friza akitafuta kuku wa pili.......
SEMA KWELI siku zote
SHARE