Sema kweli siku zote

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Mwanamke aliingia kwenye bucha ya nyama na kumuuliza muuzaji,

"Una kuku?"

Muuza nyama akafungua friza na kutoa kuku pekee ambaye ndiye alikuwa amesalia akamweka kwenye mizani. Mizani ikasoma Kilo 1.5.

Yule mwanamke akamtazama kuku kisha akauliza

"Hakuna mwingine ambaye walau ana kilo mbili?"

Muuzaji akamrudisha kuku kwenye friza kisha akamtoa tena yuleyule na kumuweka kwenye mizani. Kwa ujanja wa hali ya juu akakandamiza mizani kwa kidole gumba na mizani ikasoma kilo 2.

"Safi sana" Alisema yule mwanamke.

"Nitachukua kuku wote wawili"

Hadi sasa kichwa cha muuza nyama bado kimo ndani ya friza akitafuta kuku wa pili.......

SEMA KWELI siku zote

SHARE
 
Easy tu, ni kumpanga tu,

"dada kuku wapo hawa hawa wawili, huyu mmoja tayari ameshawekewa oda, huyu wa kilo 2,ila kwakuwa namuweza ndio maana nikakubali kukuuzia mteja moya, nitajua cha kumueleza, ila si kuuza woote, mwenyewe anampitia muda si mrefu,so nikupe wa kilo 1.5 ama 2?"
 
umenikumbusha yule jamaa wa kijiwe cha kahawa akiwapa stori wenzie..
kwamba walienda kuwinda...
wakapata swala sasa yeye akaambiwa akaanze ukata nyama..
akakata miguu miwili ya swala na kuweka begani!!
ghafla simu yake ikaita;
akapokea alivyomaliza akauliza wanywa kahawa wenzie niliishia wapi kwenye stori??!!
wakamjibu uliishia ukiwa umeweka mguu na paja begani!!
jamaa akajibu basi nilimtia yule demu balaaaa!!
kasahau kwamba aliweka miguu y swala begani sio ya demu...
 
πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ™
 
Apo ndo utajua ujui🀣
 
Mwambie butcher man siku nyingine apandishe mashetani mteja akimbie, sasa kichwa kikiganda humo?
 
oyaaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Maneno kumi ktk igizo LA mambo na vijimambo
 
uongo mwingine haufaiπŸ’ͺ🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…