Semina ya ujasiriamali bure

TheThreatTr

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
339
Reaction score
13
Habari wanajf, Green world International Limited Company inapenda kuwatangazia watu wote wanapenda kufanya ujasiliamali kwa kianzio cha 30000/= kama mtaji wako wa biashara na kuwa millionea wa mafanikio katika ujasiliamali wako......Semina hizi hufanyika bure kila Jumatatu, Jumatano na Jumamosi kuanzia saa tatu asubuhi, Tunapatikana Dar es salaam Posta mkabara na Holiday Inn, kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kufika katika hiyo semina PIGA 0654158574/0765353056 NA UTAPOKELEWA VIZURI NA KUKARIBISHWA SANA...ASANTENI SANA.
 
kuanzia saa tatu asubuhi? nitamwambia boss naenda wapi siku hizo tatu? au wafanyakazi hamuwaitaji? hata kama nina biashara nitafunga kila siku siku zote hizo? nilidhani muda mzuri ni jioni au weekend.
 
Bure kweli?
Maana unaweza aambiwa bure kumbe ukifika kuna kuambiwa ukumbi uulipie,mara vitafunwa,ukitoka hapo huo mtaji wenyewe umakula.Mara mumchangie mwana semina.Stationary,Wengi wamekuwa wakifanya hivyo.
Ila kama nyie hakuna chochote cha kulipia basi ni nzuri zaidi.
 
Hakuna umilionea wa kirahisirahisi hivyo. Halafu hawa watu wanaojiita waalimu wa ujasiriamali mjini wameshakuwa wengi sana. Mtu anakufundisha umilionea na yeye hata baiskeli hana.. inanikera sana..
 
Jameni sio bure ila ni sh. 30,000/= na imefichwa kama mtaji wako

du ama kweli mmefika mbali kwa hili
 
Mtanzania kuwa makini.Ukosefu mkubwa wa ajira nchini umepelekea uwepo wa wimbi kubwa la matapeli

Wanatumia mbinu nyingi,na wanaadvance mbinu zao kila leo

Tumia akili kureason kabla hujaingia mkenge wowote ukaliwa hata hicho kidogo ulicho nacho

Lakini pia usiwe too blind ukakosa kuziona fursa
 


Ninyi hamna nia njema hata kidogo......huo muda si sahihi na hauja zingatia maslahi mapana ya kitaifa. shame on you.
 
Hiyo semina itahusu mambo gan haswa?
 
ni wezi tu maaana hicho wanachotoa si ujasiriamali ila ni ujuzi tu , ambao mtu unaweza upata popote pale kama ukitafuta kwa umakini
 
kuanzia saa tatu asubuhi? nitamwambia boss naenda wapi siku hizo tatu? au wafanyakazi hamuwaitaji? hata kama nina biashara nitafunga kila siku siku zote hizo? nilidhani muda mzuri ni jioni au weekend.

Nafikiri unazungumzia muda wako ukiwakilisha wengine bila kuombwa. Usiwe na Utanzania uliopitiliza wa kukosoa kila kitu. Mtu ambaye hana nia siku zote atatafuta excuses. Kinachokufanya upatikane weekend ni kwa sababu hiyo ni siku yako ya kupumzika, je watoa semina hawapumziki? Ingekuwa Ngwasuma ungchukua hata likizo, lkn kwa kuwa ni jambo la maana na tumerogwa basi excuses kibao.

Semina hizi zingewekwa weekend bado wangepatikana kama wewe watakaosema HIZO NI SIKU ZA IBADA NA KUPUMZIKA, we kama unataka tailor made funguka., sio kutoa masharti.
 
Aisee JF kwa kunanga watu.
Yaaani jamaa amesepa moto mkali,anasikilizia gia ya kuja nayo.

Sio siri hawa watu siku hizi mjini wamekuwa wapiga hela kweli.

Mie wife alienda kwenye mafunzo hayo,kwa siku mbili elfu 35,wakatakiwa watoe mchango wa cheti,aisee kwenye cheti elfu 10,mpaka leooo.

Mbaya zaidi,wanasema bure na hawaendi vijijini,wao wamekazania mjini tuuuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…