seminari seminari

Kashishi yetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2014
Posts
3,509
Reaction score
3,741
wakubwa msaada, kijana wangu mtoto wa kaka yangu kang'ang'ania kwenda kusoma seminari,nimeamua kutii maamuzi yake, je ada ya seminari ya visiga na ya maua ni sh. ngapi?au kama kuna mtu anajua seminari ya kikatoriki na gharama zake anijulishe ili huyu mwanangu nimpeleke huko maana amelilia sana kusomea huko.
 
Seminari za Kikatoliki huwa hawaendi kwa mtindo huo. I gather from your bandiko kwamba wewe sio Mkatoliki, ladba nakosea lakini seminari ni kwa ajili ya kuaandaa vijana wanaotaka kuwa makasisi hapo baadae na sio kwa kila kijana aliyemaliza darasa la saba.
To cut the story short, kijana anapaswa kupitia parokiani kwake ili kuweza kupata nafasi.
 
Yawezekana ni mkatoliki jina tuu, ambaye hata mlango wa kanisa ajui, ambaye hata jumuia ndogondogo haudhurii anajifanya yupo bise.Week end yote anaimalizia bar akiwa na ipad ambayo ameiamini atapata taarifa zote humo ndio maana kaamua kuuliza hili. Angekuwa anaudhuria kanisani angemuuliza hata katekista
 
Ili aweze kwenda Semimari(Kitalu) lazima awe na nia ya kuwa Padre hilo ndo la msingi.....

Kuna tofauti kati ya Seminari na Catholic managed school....Hata madhehebu mengine wanaiga kuita shule zao seminari lakini kwa uhalisia si Semnary....

Kama ana nia ya kuwa padre basi mpeleke.....Kipaumbele (Priority) hupewa wale Altar Boys kwa asilimia kubwa...

Ada ya Simninary si kubwa maana Seminanry zinapata ruzuku kutoka Vatican..
 

Inavyooneka wewe si Mkatoliki na maana ya Seminari hujui.....Anyway mpeleke kwenye shule za Kanisa za Katoliki..(Catholic managed schools)

Hata hizo Catholic schools zipo very selective 70% must a Catholic Student....

Kwa hiyo kama wewe si Mkatoliki una chance ya 30% kupata....

Shule hizo ni (Best Catholic Schools)
1. Marian(Boys/Girls)

2. St. Francis Girls Mbeya
3. St Mary Gorett Kilimanjaro
4. St. Joseph Millenium
5. St Marys Mazinde Juu
6. Kifungilo Girls Tanga
7. Rosmin Tanga
8. Abbey Mtwara
9. Bethel Sabs Iringa
10. Precious Blood Girls Arusha
11. Tengeru Boys Arusha
12. St Amedeus biys Kilimanjaro
13. Bendel Kilimanjaro
14. Anwarite Girls Kilimanjaro
15. Kandoto science Girls Kilimanjaro

Na nyingine nyingii ......Zote hizo ukifungua matokea ya Necta ni.Div 1 na 2...bhasssd
 
Seminari ni nini? Mseminari ni nani? Hayo ni baadhi ya maswali niliyoulizwa katika mtihani wa Dini wakati nilipofanya mtihani wa kujiunga na Seminari mwaka 1997 katika Ukumbi wa Msimbazi Centre.Kimsingi,Seminari ni shule maalum za kikatoliki ambazo huandaa vijana kuwa Mapadre. Ni wavulana tu.

Kujiunga na Seminari kuna taratibu zake. Kwahiyo,usianze kuuliza ada wakati hujui taratibu za kujiunga na Seminari. Labda umpeleke kwenye shule alizoorodhesha mkuu tedo. St.Mary's Junior Seminary Visiga ni kati ya Seminari ninazoziongelea.
 
Last edited by a moderator:

ahsante,
 

Aliyekwambia rosmin ni shule ya catholic ni nani???
Rosmin haina uhusiano na catholic kabisa ni mtu binafsi tu

Kwa seminary

Uru seminary ipo uru
Maua seminary ipo marangu
St james ipo kilema
St amedeus ipo kilema form zake nenda office za marian pale msimbazi center
Visiga seminary
St mary's seminary nyegezi mwanza
Ndanda abbey

Uwahi mapema kuchukua form pia seminary anatakiwa apate barua ya paroko wa kanisani kwake
 
kama wewe ni mkatoliki, nenda kwa paroko wa parokia yako na umweleze nia ya kijana wako (nia ya kwenda Seminari), utapata maelezo zaidi. Paroko anaweza kukuidhinishia barua ambayo itakusaidia kupata nafasi (kama zipo) ktk Seminary unayotaka.
 

Umawazimu nini.....

Rosmini ni shule ya Katoliki...Inamilikiwa au managed na Rosminian Fathers...Ipo Tanga

Google basi usiwe kichwa panzi..(Google Rosminian Fathers halafu ujionee aibu mwenyewe)

Anyway hata catholic schools ni Binafsi(Ptivate)
 

Halafu St. Amedeus sio Seminary....
 
kama wewe ni mkatoliki, nenda kwa paroko wa parokia yako na umweleze nia ya kijana wako (nia ya kwenda Seminari), utapata maelezo zaidi. Paroko anaweza kukuidhinishia barua ambayo itakusaidia kupata nafasi (kama zipo) ktk Seminary unayotaka.

Priority kubwa ni kwa Alter Boys....
 
Halafu St. Amedeus sio Seminary....

Hii st.amedeus nakumbuka alienda kuianzisha padre faustine furaha aliekuwa mwl wangu wa historia pale st.james seminary....ndo yalikuwa mashamba ya seminary mandaka kule kilema...aiseee umenikumbusha mbali sana....viva fr.furaha mana alisema shule yake italeta ushindani sana kwa seminary ya st.james na kwakweli nimeona hilo...
 
Hasa kwa wale wanaokwenda Diocesan seminaries

hata wale wanaoenda seminary za mashirika mana huko lazima uende na barua kutoka kwa paroko kwahiyo hoja ya alter boys bado ni ya muhimu sana kwa mseminary yeyote na siku hizi naona wanasema either alter boys or chama cha upapa cha wale watoto wanaochezacheza....
 


anataka akasome seminary au anataka akasome ili aje kuwa padre...ada zao huwa si kubwa ila cha msingi awe na nia thabiti ya kuja kuwa padri...seminari ni kitalu cha malezi ya wito wa upadre kwa hiyo kwa njia yoyote seminary ni sehemu ya vijana wanakopata malezi ya kuja kuwa mapadre.
 

st´majuse...mkuu ulitoka lini visiga
 
Last edited by a moderator:

st.james seminary nikikusahau na mkono wangu wa kuume unyauke....u made me be the way I am today....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…