BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Sendeka awavaa wanaokingia kifua vigogo
2008-12-24 12:38:07
Na Simon Mhina
Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, amesema kamwe hakuna kigogo nchini atakayekamatwa na nchi kutikisika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Sendeka alisema madai hayo yanatolewa na wapambe wa baadhi ya vigogo kwa lengo la kujijengea `kinga`.
Sendeka alisema hakuna mtu anayeweza kutikisa nchi kama Tanzania ambayo inaongozwa na sheria, huku ikiwa na vyombo thabiti vya dola; serikali, bunge na mahakama.
``Nashangaa wanaosema eti fulani akikamatwa na kufikishwa mahakamani nchi itatikisika, hakuna wa kutikisa nchi.
Wanaotoa madai hayo ni wapambe wa vigogo ambao wanadhani wapo hatarini kufikishwa mahakamani,``alisema.
Mbunge huyo alisema kama kuna mtu ambaye akiguswa nchi inaweza kutikisika ni Rais.
Alikuwa akitoa maoni yake juu ya mjadala unaoendelea, ambao ulianzishwa na wanasiasa na wanasheria, wakitaka Rais mstaafu Benjamin Mkapa aondolewe kinga ili aweze kuburuzwa mahakamani.
Sendeka alisema kimsingi yeye hakubaliani na wazo la kumuondolea kinga Mkapa kwa sababu kuu mbili;
mosi, wanaosema apokonywe kinga hawajawa na ujasiri wa kutaja waziwazi makosa yake.
``Wengi wanasema aunganishwe na fulani aunganishwe na yule, lakini hawasemi, kuwa wanataka yeye kama Mkapa asomewe shtaka gani?`` alihoji.
Pili, alisema kumfikisha mahakamani rais mstaafu, linaweza kuwa jambo ambalo halina maslahi kwa hatima ya taifa.
Alisema kutangaza kwamba mtu fulani akikamatwa nchi itatikisika, ni sawa na kumdhalilisha rais aliyeko madarakani kuonekana serikali yake ni legelege.
SOURCE: Nipashe