Senegal yaitaka Ulaya kusaidia kukabili ugaidi Sahel

Mrengwa wa kulia

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
1,091
Reaction score
3,695
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameitaka Ulaya kusaidia kukabiliana na tishio la usalama linaloongezeka huko Sahel, eneo tete ambalo limekabiliwa na mfululizo wa mashambulizi mabaya katika siku chache zilizopita.

Ametoa wito huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, ambaye alikuwa anamaliza ziara yake Afrika Magharibi.

"Hali katika eneo la Sahel inataka uhamasishaji wa kimataifa wa jumuiya ya kimataifa," alisema Rais Faye, kurejesha Mali, Niger, na Burkina Faso katika umoja huo. Alisisitiza haja ya Ulaya kuzidisha uungaji mkono wake kwa Sahel, ikizingatiwa kwamba "Afrika na Ulaya zina hatima iliyounganishwa ya usalama."

Ombi lake linawadia siku chache baada ya Burkina Faso kushuhudia moja ya mashambulizi yake mabaya zaidi.

Makumi ya raia na vikosi vya usalama waliuawa na wanamgambo katika eneo la Kaskazini la Barsalogho mnamo Agosti 24.

Kundi la wanajihadi lenye uhusiano na Al-Qaeda,(JNIM) lilidai kuhusika na shambulio hilo la kikatili, ripoti zikidokeza kuwa watu 200 waliuawa kwa jumla wakati wakichimba mitaro ili kulinda kijiji chao dhidi ya wanamgambo.
Bado haifahamiki jinsi Burkina Faso, Mali, na Niger zitatafsiri wito wa kiongozi wa Senegal wa kuingilia kati kwa Ulaya katika mgogoro wa Sahel, kwani walivunja uhusiano na vikosi vya Magharibi na kuwaamuru watoke katika eneo hilo hilo la Sahel wakati bado hali ikiwa tete.

Nchi hizo tatu ziliunda muungano wa kijeshi ili kukabiliana na uasi na kuendelea kuwa na uhusisano wa kiusalama na Urusi ambayo huwapa silaha na wale inaowaita kama "wakufunzi wa kijeshi." russia mziki wa sahel umemzidi uwezo.

source.
AFP
BBC
 
View: https://x.com/ajsteelshow/status/1829187261428314515
 
Senegal nayo inatishio la ugaidi ?
 
Jihadists wanakuwa bubu hapa maanake wanaoleta chokochoko zote hizi ni wapiganaji wa kiisilamu wanaodai kumpigania mungu wao anayeitwa allah.

Wanaoshambuliwa ni serikali zile zilizozikataa nchi za magharibi na kuungana kwa Russia ambaye hata hivyo ameshindwa kuwasaida.
 
Hivi hao waasi nani anawafadhili!? Hao waasi madai yao hasa ni ya kisiasa au kikabila au kidini? Kinacho sikitisha zaidi tunauana wenyewe kwa wenyewe kwa maslahi mapana ya watoka mbali,duh!
 
Wanafadhiliwa na itani. Hujui?
 
Back
Top Bottom