Sensa 2022 ingeratibiwa na mabalozi wa nyumba kumi ingeleta takwimu sahihi zaidi ya zitakazotolewa na maafisa watakaopita nyumba kwa nyumba

Maulaga59

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2021
Posts
2,984
Reaction score
2,971
Najaribu kuangalia changamoto wanazopata maafisa wa sensa wanaotumwa na serikali katika kukusanya taarifa muhimu za idadi ya watanzania.

Ukweli ni kwamba kwa sababu ya mazingira ya Tanzania yalivyo kijiografia ni vigumu sana hawa maafisa kuweza kupata takwimu sahihi za kusudio lao. Kuna sehemu ambazo huwa siyo rahisi kufika kwa gai au kwa mguu kwa sababu mbalimbali kama vile mapori, mabonde, milima, wanyama wakali na kadhalika.

Wenyeji wa maeneo hayo wao wanao uzoefu hata wa kufika makao makuu ya wilaya lakini si kwa wageni na muda mfupi wanaokuwa wamepewa kufanikisha zoezi.

Balozi wa nyumba kumi wangepewa semina za kufanya zoezi hilo wangeweza kuja na takwimu sahihi zaidi kuliko zile za maafisa waliotumwa.

Kila balozi angeweza kupeleka takwimu za watu wake kwenye ofisi ya kata na ofisi ya kata ingeratibu zoezi hilo katika eneo lake, kisha kupeleka ngazi za juu hadi ngazi ya taifa.

Zoezi hili siyo tu lingeleta takwimu sahihi zaidi bali pia lingepunguza gharama kubwa ambazo serikali hutumia katika kufanikisha zoezi zima.

Kwa huu utaratibu unaotumika kila baada ya miaka 10 watu wengi huwa wanaachwa bila kuhesabiwa hasa kwenye maeneo magumu kijiografia.

Nadhani miaka ijayo kazi hii ifanywe na mabalozi wa nyumba kumi.

Nawasilisha.
 
Ni kweli lakini utaratibu ungekuwa ni Afisa kushirikiana na mabalozi au hata wenyeviti wa mtaa ili kuratibu zoezi ingependeza zaidi (nafikiri inafanyika hivyo), kumbuka dodoso la sensa lina maswali mengi ambayo yanahitaji mtaalamu wa masuala hayo, hivyo uwepo wa mtaalamu kunaleta tija zaidi kwani si kila balozi ana elimu ya kutosha kufanikisha suala hilo.

Na pia kutokana na jinsi tunavyoishi nao huku mitaani kuna baadhi ya mabalozi hawapatani kabisa na baadhi ya wakazi kutokana tu na migongano katika utekelezaji wa majukumu, hivyo itakuwa ngumu mtu ambae mmeshazinguana hata kupelekana polisi au kuitiana mgambo, leo aje na dodoso lake mkae pamoja muanze kuzungumza na kukusanya taarifa, ni ngumu sana.

Utaishia tu kupika data na kujaza taarifa kutokana na uelewa wa kawaida.
 
Kwa hiyo unataka Serikali iikabidhi CCM iendeshe zoezi la sensa 2022!

Au sijakuelewa, kwa sababu katika mfumo wa Kiserikali hakuna cheo Cha balozi bali mwenyekiti/myendaji wa mtaa. Mabalozi ni utaratibu wa Chama ili kuhakikisha kaya zote wakati wa kampeni za uchaguzi zinafikiwa na rushwa ya chumvi.
 
Ni kweli lakini utaratibu ungekuwa ni Afisa kushirikiana na mabalozi au hata wenyeviti wa mtaa ili kuratibu zoezi ingependeza zaidi (nafikiri inafanyika hivyo), kumbuka dodoso la sensa lina maswali mengi ambayo yanahitaji mtaalamu wa masuala hayo, hivyo uwepo wa mtaalamu kunaleta tija zaidi kwani si kila balozi ana elimu ya kutosha kufanikisha suala hilo,

na pia kutokana na jinsi tunavyoishi nao huku mitaani kuna baadhi ya mabalozi hawapatani kabisa na baadhi ya wakazi kutokana tu na migongano katika utekelezaji wa majukumu, hivyo itakuwa ngumu mtu ambae mmeshazinguana hata kupelekana polisi au kuitiana mgambo, leo aje na dodoso lake mkae pamoja muanze kuzungumza na kukusanya taarifa, ni ngumu sana.

utaishia tu kupika data na kujaza taarifa kutokana na uelewa wa kawaida.
una akili kubwa sana mkuu..
 
Mbona sensa ilopita maafisa walisaidiana na wenyeviti,at mwaka huu nadhani itakuw ivo
 
SENSA ni biashara ya maafisa wa sensa na wanasiasa.
Haingii akilini kwa teknolijia ya karne ya 21 eti serikali inasubiri miaka 10 ndio ihesabu watu.
Ni upuuzi wa maafisa wachache wanaotaka kupiga pesa.
Senza zingeweza kupatokana kila mwaka bila hata ya gharama kubwa.
 
Najaribu kuangalia changamoto wanazopata maafisa wa sensa wanaotumwa na serikali katika kukusanya taarifa muhimu za idadi ya watanzania.

Ukweli ni kwamba kwa sababu ya mazingira ya Tanzania yalivyo kijiografia ni vigumu sana hawa maafisa kuweza kupata takwimu sahihi za kusudio lao. Kuna sehemu ambazo huwa siyo rahisi kufika kwa gai au kwa mguu kwa sababu mbalimbali kama vile mapori, mabonde, milima, wanyama wakali na kadhalika.

Wenyeji wa maeneo hayo wao wanao uzoefu hata wa kufika makao makuu ya wilaya lakini si kwa wageni na muda mfupi wanaokuwa wamepewa kufanikisha zoezi.

Balozi wa nyumba kumi wangepewa semina za kufanya zoezi hilo wangeweza kuja na takwimu sahihi zaidi kuliko zile za maafisa waliotumwa.

Kila balozi angeweza kupeleka takwimu za watu wake kwenye ofisi ya kata na ofisi ya kata ingeratibu zoezi hilo katika eneo lake, kisha kupeleka ngazi za juu hadi ngazi ya taifa.

Zoezi hili siyo tu lingeleta takwimu sahihi zaidi bali pia lingepunguza gharama kubwa ambazo serikali hutumia katika kufanikisha zoezi zima.

Kwa huu utaratibu unaotumika kila baada ya miaka 10 watu wengi huwa wanaachwa bila kuhesabiwa hasa kwenye maeneo magumu kijiografia.

Nadhani miaka ijayo kazi hii ifanywe na mabalozi wa nyumba kumi.

Nawasilisha.
Mbalozi wa nyumba kumi hawapo na hawatbuliwi kisheria. Hao ni makada wa CCM tu
 
Mkuu unataka sisi jobless tukale wapi. 😊
Hebu tuendee na utaratibu uliozoeleka tu
 
Acha watumie vyema pesa ya serikali hiyo ni ajira juu ya ajira kwa wenye ajira.
 
Najaribu kuangalia changamoto wanazopata maafisa wa sensa wanaotumwa na serikali katika kukusanya taarifa muhimu za idadi ya watanzania.

Ukweli ni kwamba kwa sababu ya mazingira ya Tanzania yalivyo kijiografia ni vigumu sana hawa maafisa kuweza kupata takwimu sahihi za kusudio lao. Kuna sehemu ambazo huwa siyo rahisi kufika kwa gai au kwa mguu kwa sababu mbalimbali kama vile mapori, mabonde, milima, wanyama wakali na kadhalika.

Wenyeji wa maeneo hayo wao wanao uzoefu hata wa kufika makao makuu ya wilaya lakini si kwa wageni na muda mfupi wanaokuwa wamepewa kufanikisha zoezi.

Balozi wa nyumba kumi wangepewa semina za kufanya zoezi hilo wangeweza kuja na takwimu sahihi zaidi kuliko zile za maafisa waliotumwa.

Kila balozi angeweza kupeleka takwimu za watu wake kwenye ofisi ya kata na ofisi ya kata ingeratibu zoezi hilo katika eneo lake, kisha kupeleka ngazi za juu hadi ngazi ya taifa.

Zoezi hili siyo tu lingeleta takwimu sahihi zaidi bali pia lingepunguza gharama kubwa ambazo serikali hutumia katika kufanikisha zoezi zima.

Kwa huu utaratibu unaotumika kila baada ya miaka 10 watu wengi huwa wanaachwa bila kuhesabiwa hasa kwenye maeneo magumu kijiografia.

Nadhani miaka ijayo kazi hii ifanywe na mabalozi wa nyumba kumi.

Nawasilisha.
Tafuta pesa
 
Back
Top Bottom