Kama kawaida kwa kuwa hukubaliani na jinsi mwingine anavyofikiria unaamua kutoa kashfa, sasa sijui unatumia kigezo gani kuita mawazo ya mtu mwingine dhaifu hayafai kuwekwa hapa kama uko sahihi kwa nini sasa mods hawajaitoa au unashauri na mods wa JF nao dhaifu kwa maana wameshindwa kuona udhaifu wa mawazo yangu? Inabidi ukue (kiakili) sio lazima wote tukubaliane, nchi tuko mill 40 hivyo haiwezekani wote tukawa na mawazo sawa!Mawazo yako ni dhaifu sana, na ayaendani na level ya JF.
Kwa maoni yako mwenyewe umesema sio lazima watu wote wakubaliane kwa kila kitu humu,hivyo ulipaswa kukubali kupokea opposition pia na muhimu ni kuvumiliana kimawazo,haya ni maoni yangu unapaswa kuyaheshimu pia
Nimekuwa nikisikia kila kukicha kuhusu baadhi ya watu kugomea Sensa, hivi ni kwa nini Serikali isiwapige faini wale wote ambao hawatataka kuhesabiwa badala ya kupoteza muda sijui kukamata shehe huyu sijui mwenyekiti wa kijiji yule.
Naona imefika wakati sasa Serikali iwe Serikali hamna kubembelezana tena, tunakuja nyumbani kwako hutaki kuhesabiwa faini na ni lazima ulipe usipolipa tunataifisha mali tunaendelea mbele.
Haiwezekani watu kugomea Sensa ikimbukwe serikali inatumia pesa nyingi sana kwa zoezi hili na watu hao hao wanaolia umaskini kila siku ndio wa kwanza kuhujumu rasilimali zetu!
Nyie na serikali yenu dhaifu endeleeni kutapatapa bt waislam msimamo uleule hakuna kipengele cha dini hakuna muislam kuhesabiwa,chezea waislam ww!
hebu nipe namna ya kuwatoza hiyo faini
Sina haja ya kujibizana na wewe kwani wewe ndio wale wanaosema mtoto ni wangu naamua mwenyewe kama aende shule au akae nyumbani na serikali haipaswi kuniuliza!Yaani hapa ndo mwisho wa upeo wako wa kufikiri? sasa faini hiyo kwa kosa gani? kwani mtu asipohesabiwa ni kosa,
mbona hamna uhusiano wowote kati ya sensa na faini, jitahidi kuuliza na kupata mawazo kabla hujapost hizi pumba zako humu jf.
Mi nazani Elimu ndo inatakiwa kutolewa kuhusu sensa na sio mabavu..