Sensa ijayo iboreshwe

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Matumizi ya teknolojia kwenye sensa hii yameanza kuonekana. Yapo baadhi ya mambo tukiboresha itasaidia zaidi.

Mfano. Kuwe na online forms ambazo wananchi wata download na kujaza taarifa zao kisha kuziwasilisha huko ofisi ya Takwimu.

Baada ya hapo, wanapata ID ambapo watu wa sensa wakipita wanaweza ku verify tu.

Hii ingepunguza muda majumbani, hotelini, hospitals na sehem nyingine. Au ni sensa app tunajaza wananchi wenyewe.

Lakini pia, kungekuwa na mapping ya mapema ambayo itaonesha maafisa sensa wanapita eneo fulani saa ngapi au siku gani. Ikibidi watu wabuku muda wao wa kuhesabiwa au kuwa verified.
 
Kuna aina nyingi za kuchukua taarifa. Hiyo unayoisema inaitwa self enumeration. Hii kwa watu kama nyie si sahihi maana mauongo ndiyo kwao.
 
Kuna aina nyingi za kuchukua taarifa. Hiyo unayoisema inaitwa self enumeration. Hii kwa watu kama nyie si sahihi maana mauongo ndiyo kwao.
Tumesema afisa sensa ata verify. Pamoja na hivyo, kumtuma afisa sensa hakuzuii uongo. We should embrace technology
 
Sure ww u meona mbali. Mom nimesubiri hadi muda huu hawajafika na niliahirisha shughuli zangu. Hapa nawaza kesho cjui itakuwaje.
 
Tumesema afisa sensa ata verify. Pamoja na hivyo, kumtuma afisa sensa hakuzuii uongo. We should embrace technology
Hakuna kitu kama hicho my friend katika utafiti. Kunakuwa na misleading answers. Sasa hata akiverify si kazi nyingine errors zitakuwa nyingi. Mfano neno kaya kwa kila utafiti lina defenition yake na ndo maana kila utafiti kabla ya kuanza huwa kuna mafunzo
 
Tumesema afisa sensa ata verify. Pamoja na hivyo, kumtuma afisa sensa hakuzuii uongo. We should embrace technology
Mawazo mazuri ila mimi nawaza tofauti,kila mtu awe na namba ya Nida na record zake ziwe kwenye system
Ukioa system ijue
Ukifa system ijue
Ukitoa talaka mahakamani system ijue
Ukipata kazi ijue
Ukifukuzwa kazi system ijue
Ukichukuacmkopo pia ijue
Mwisho wa mwaka you run the report na kujua nani kafa nani kazaliwa,nani kaoa nani kaacha.
 
Watanzania wengi tu wanaweza kujaza hizi forms. Mie nilikuwa nchi X wakati fulani, tulikuwa tukiletewa form tujaze, na zoezi lilifanikiwa. Tatizo ni Tanzania tu?
 
Watanzania wengi tu wanaweza kujaza hizi forms. Mie nilikuwa nchi X wakati fulani, tulikuwa tukiletewa form tujaze, na zoezi lilifanikiwa. Tatizo ni Tanzania tu?
Ngoja nikuache, kwaheri
 
Sio kwa Nchi hii muktadha wa Sensa ni jambo jema na la haki kabisa kama inavyojipambanua kwa malengo yake,Shida ni pale inapogeuka fursa kipesa ukiwahoji makarani wengi wanafikiria pesa tu huko ngazi za juu ndio usiseme watu wanafikiria asali tu kwa hivyo nihitimishe kwa kusema kama serikali ipo serious iandae hyo app Raia wajisensabishe wenyewe
 
Ni uelewa wa watu na utayari tu ndio unaohitajika
 
Sensa ya michongo.
Haikuuliza kuhusu status ya employment / unemployment.
Wanauliza vijana Wana umri gani, elimu kiwango gani, ukishawatajia chuo hawaendelei kuuliza Kama huyo mwamba aliyemaliza chuo ana ajira au analima. Wanauliza Kama mama Yao mstaafu anadhughuli za ujasiriamali.
Sasa tutapata wapi statistics za watu waliomaliza vyuo lkn hawana ajira?
 
Sio rahisi kihivyo
 
Hii sensa ilipaswa kuwa coordinated na watendaji wa mitaa ambao wapo exposed wa namna ya kufanya kazi na wananchi, wamewapa wadogo huku wanasiasa wakitumia fursa ya kujinadi kwamba wametoa ajira lakini ukweli ni kwamba madogo exposure ya namna ya kufanya kazi inakuwa ngumu kwa kuwa ndio first time kutia timu kwa jamii alafu anakuwa na dodoso refu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…