Sensa kata ya mbezi hakuna posho,peni unanunuwa mwenyewe!

Mnyella

Member
Joined
Aug 8, 2012
Posts
43
Reaction score
6
Sisi wana mafunzo wa kata ya MBEZI,ambako kituo chetu cha mafunzo kipo SEKONDARI YA KIBAMBA,tangu tuanze mafunzo hatujapewa hata senti moja kila kitu tunajigharamia wenyewe,cha ajabu mpaka peni ya kuandikia unanunua mwenyewe,wengine sasa hali imekuwa ngumu darasani tunalala tu kwa ajili ya njaa,nauli ndio ya kuomba kila siku,hivi haya ni mafunzo ya sensa au mateso ya sensa.
 
Vumilieni, kama unaona vipi, achia ngazi ili usiteseke kama unavyosema.
 
poleni sana tatizo hilo liko hata huku mwanza wilaya ya ilemela watu bado hawajapewa pesa.........sijui tatzo nn
 

Kwenye Dodoso hujakutana na kitu TUNZA SIRI?
 
Si muwaulize hao wanasimamia tatizo, au kama vipi mtie mgomo ili wastuke. Si unajua ukweli kuwa "corrupt people have got currupt means, and they need to be currpted to neutralise the situation"
 
Si huko tu hata kata za wilaya ya ilala,hata walioanza alhamis(dodoso refu) hawajapata hata shilingi na hakuna taarifa zozote
 
Wengine nimewaona weeeengi leo Sinza wamebeba MIKOBA ya kichina yaani SENSA mmeaibisha nchi, ile mikoba ya kichina ya kkoo buku mbili ndo mnawapa watu wenu? Haina hata chata/LOGO mlivyochukua dukani mkawagawia...
 
nchi hii umeisahau hakuna mafanikio bila mgomo gomeni tuuu mtapewa mapesa,,,
 
...sensa kwa maendeleo, jiandae kuhesabu...achana na pesa...hahahaaaaa. Hii ndo sirikali, kila kitu dosari tuuu...
 
Sie huku tumepewa pen, penseli, kifuto, daftari na tushakatiwa nusu alowance so poleni xana. I thnk kupata au kuchelewa inategemeana na mratibu wenu au wamtuogopa Wanakilimanjaro? Teh! Mchaga afanye kazi ya bure tampata sasa? Teh teh!
 
Serikali Dhaifu haina uwezo
 
Serikali haina fedha so Mfanye kwa Mkopo kama Maticha walivyokuwa wakifanya miaka nenda rudi
 
Dah kumbe bora sisi tushakula laki na sitini na mbili na miatano ila kwa mbinde sanaaaaa ...tbr
 
Tatizo majina na walioripot tofaut so wakawa wanashndwa kupeleka exactly names, juz 2memaliza kusaini na pesa 2kapewa.
 
Kata ya Mbezi nadhani kuna walakini. Applicants wa form V1 wengi wamekuwa turned down kwa kazi ya ukarani wa sensa sijui kwa nini. Hii kitu kuna watu wanatafuta ulaji kwa nguvu lakini wajue jamii itawalipua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…