BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakati kazi ya sensa ikitarajiwa kumalizika leo, baadhi ya viongozi wameendelea kueleza changamoto katika kufanikisha kazi hiyo.
Changamoto hizo ni wizi wa vishikwambi, kukosekana mtandao kwenye baadhi ya maeneo, kuisha kwa chaji za vishikwambi na baadhi ya watu kuchelewesha kazi hiyo kwa maelezo hawaoni umuhimu.
Mkoani Iringa hadi jana kuliripotiwa matukio sita ya kuibiwa vishikwambi huku sababu kubwa ikitajwa ni ulevi wa makarani na kutokuwa makini katika utunzaji wake.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego kwenye taarifa yake kwa umma alisema, ‘tangu kuanza kwa kazi hii hadi leo tumeshapoteza vishikwambi sita, ingawa tumefanikiwa kuvipata vinne, lakini vingine viwili hatujavipata. Changamoto kubwa ni ulevi kwa baadhi ya makarani wetu.”
Hata hivyo, aliwataka wananchi waondoe hofu na kwamba wote watahesabiwa huku akisema hadi jana mchana zaidi ya kaya 200,000 zilikuwa zimefikiwa.
Mkoani Songwe, kazi ya sensa imeonekana kukubwa na kizingiti kwa baadhi ya maeneo kutokana na mwingiliano wa mambo matatu kwa wakati mmoja.
Wakati wananchi wanaandikishwa kwa ajili ya sensa, wengine wanaandikisha wakulima kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku huku kukiwa na kampeni inayowataka wapangaji kulipa asilimia 10 ya kodi wanayotozwa na wamiliki wa nyumba.
Baadhi ya makarani waliozungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti walisema baadhi ya maeneo ya miji ya Mlowo na Tunduma hawajafanikiwa kukutana na wakuu wa kaya kwa maelezo wameenda kujiandikisha kupata mbolea.
Msimamizi wa sensa Kata ya Mlowo, Harry Kapele alisema kazi ya kuandikisha mbolea imeathiri upatikanaji wananchi nyumbani, hali inayolazimu makarani kurudia nyumba nyingine kwa ajili ya kupata hesabu kamili.
Akizungumzia kodi ya majengo, alisema licha ya hamasa kubwa iliyotolewa, baadhi wanaona kama inahusiana na kodi ya majengo kupitia tozo ya wapangaji, hivyo hawataki nyumba zao zihesabiwa wakidai hawana anuani za makazi.
Mratibu wa sensa mkoani Songwe, Dotto Alley alisema changamoto zote wanazifanyia kazi, ili kuhakikisha kazi inakamilika kama ilivyopangwa.
Aliwataka makarani kuongeza kasi ya kuhesabu na tayari wameshagawa vitunza umeme 350 kuondoa changamoto ya vishikwambi kuishiwa chaji.
Alisema mpaka juzi walikuwa wamefikia asilimia 90 ya malengo ya mkoa.
Akizungumza jana kutokea Chemba, mratibu wa sensa wa wilaya, Henry Rwejuna alitaja changamoto walizokutana nazo ni kuzima kwa vishikwambi kwa kukosa chaji na mtandao kuwa chini kwenye maeneo mengi.
“Kuna maeneo makarani wakifika wanakosa mtandao, hivyo wanalazimika kwenda eneo lenye mtandao ili kuingiza taarifa zake,” alisema.
Kuhusu kuisha kwa moto (chaji) kwenye vishikwambi, alisema walijitwika mzigo wa kukodi pikipiki ili kwenda maeneo mengine yenye umeme.
Wakati hali ya Chemba ikiwa hivyo, baadhi ya mitaa ya Kata za Nkuhungu, Chang’ombe na Hazina Jijini Dodoma, hadi jana wananchi waliendelea kuwasubiri makarani, ili wahesabiwe.
Mwenyekiti wa sensa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri aliliambia Mwanachi jana asubuhi kuwa hadi kukamilika kwa siku hiyo, wananchi wengi wangekuwa wamefikiwa.
Mwasu Malatu, mkazi wa Hazina, alisema nusu ya mtaa hawajahesabiwa, hivyo walipiga simu kwa mkuu wa wilaya kumpa taarifa hiyo.
Hata hivyo, alisema makarani wanakutana na changamoto ya wananchi wengi kutokuwapo nyumbani.
Manyara
Wilayani Kiteto mkoani Manyara, vingozi wanasema wametoa namba maalumu kwa wenyeviti wa vitongoji, vijiji na mitaa, ili waripoti maeneo ambayo hayajafikiwa na makarani.
“Hii namba ni maalumu, itakuwa na mratibu wa sensa wilaya, ambaye atapatiwa mawasiliano ya viongozi, ili kuhakikisha haachwi mtu kwenye kazi hii,” alisema mwenyekiti wa kamati ya sensa, Mbaraka Batenga.
Kwa mujibu wa Batenga ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, hadi jana asilimia 80 ya watu walishafikiwa na makarani.
Kilimanjaro yaongeza makarani
Mwenyekiti wa kitongoji cha Shabaha, Kata ya Mabogini, Athumani Msangi alisema awali walikuwa na makarani sita, lakini baadaye wakaongeza sababu kitongoji kina kaya zaidi ya 2,000.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho ambao hawajahesabiwa wanahofiwa kutofiki
Chanzo: Mwananchi