SoC02 Sensa, na Mitazamo ya Jamii Ajira fupi za Sensa

Stories of Change - 2022 Competition

kmasanja20

Senior Member
Joined
Jul 23, 2022
Posts
128
Reaction score
368
Sensa na mitazamo ya jamii ajira fupi za Sensa.
Imeandikwa na: K.Masanja​

DIBAJI
Katika kipindi hiki ambacho nchi yetu pendwa inapoelekea katika utekelezaji wa sensa ya watu na makazi ya awamu ya sita na utaratibu wake ambao hufanyika kila baada ya miaka kumi, Makala hii inalenga si tu kutoa elumu juu ya sensa ya watu na makazi pamoja na umuhimu wake kama alivyoagiza Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, bali kutoa mitazamo tofauti tofauti ya jamii kuhusu wimbi kubwa la ajira hizi kuombwa na vijana wengi hususani vijana wanaoendelea na waliomaliza vyuo vikuu ambao kwa namna moja au nyingine walitakiwa kua katika taaluma zao na si kugombania ajira za muda mfupi za Sensa.​

SEHEMU YA KWANZA

Maana ya Sensa, umuhimu na vikwazo katika utekelezaji wake.

Sensa ya Watu na Makazi ni moja ya zoezi muhimu linalokusanya taarifa za kila mtu aliyelala ndani ya mipaka ya nchi usiku wa kuamkia siku ya Sensa. Kama zilivyo Sensa zilizopita, itahusisha Makarani wa Sensa ambao wata tembelea kaya zote nchini na kufanya mahojiano ya ana kwa ana baina ya Karani wa Sensa na Mkuu wa Kaya. Sambamba na hilo, taarifa zitakazoulizwa wakati wa Sensi zitajumuisha taarifa zifuatazo;

Taarifa za kidemografia (umri, jinsi, hali ya ndoa), ulemavu (aina ya ulemavu, na chanzo cha ulemavu), uhamaji, vitambulisho vya utaifa na uhai wa wazazi, elimu, shughuli za kiuchumi, umiliki wa ardhi na TEHAMA, hali ya uzazi, vifo na vifo vitokanavyo na uzazi, nyumba, hali ya umiliki wa nyumba, vifaa/rasilimali na udhibiti wa mazingira, kilimo, mifugo, uvuvi na misitu, hali kadhalika taarifa kuhusu mpango wa TASAF, majengo na anwani za makazi.

Lengo/Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi.

Lengo la Sensa ya Watu na Makazi ni kupata taarifa sahihi za kidemografia, kijamii, kiuchumi na hali ya mazingira kwa lengo la kupata takwimu sahihi zitakazoiwezesha Serikali na wadau wengine kupanga kwa usahihi mipango ya maendeleo ya watu katika sekta mbalimbali za elimu, afya, hali ya ajira, miundombinu kama barabara, nishati na majisafi. Sensa ni zoezi muhimu ambalo kila mtanzania kwa nafasi yake analazimika kushiriki na kutimiza wajibu wake ili kuhakikisha inakuwa ya mafanikio makubwa. Hii itasaidia Serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi kulingana na idadi ya watu ya eneo husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali katika taifa.(Brosha la Sensa 2022).

Changamoto zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa Sensa.

Zifuatazo ni baadhi ya changamoto zinazoweza kujitokeza na kupunguza ufanisi wa utekelezaji wa Sensa.
  1. Elimu inayotolewa kuhusu Sensa kutofikia kundi husika, hasa maeneo ya vijijini. Pia uwepo wa ufinyu na upeo mdogo wa uelewa kuhusu Sensa.​
  2. Mila, desturi na imani potofu kwa baadhi ya jamii ambazo zinachukulia kutaja idadi ya Watoto au wanakaya waliopo ni kukaribisha laana na mkosi.​
  3. Baadhi ya jamii au familia kuwaficha na kuwazuia watu wenye ulemavu kutoshiriki katika kuhesabiwa jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu.​

SEHEMU YA PILI

Ajira za Muda mfupi za Sensa na Mitazamo ya Jamii.

Ni ukweli usiopingika kwamba, miongoni mwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, suala la ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa. Pia ukiachana na ukosefu wa ajira, hata wengi wao wenye ajira, kipato wanachokipata bado hakijafanikiwa kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Hali hii imejidhihirisha wazi wazi katika ajira za muda mfupi za Sensa ya mwaka 2022, ambapo hadi kufikia tarehe 9 Mei, 2022, walipatikana waombaji 119,468. Kati yao, waombaji 46,159 ni waajiliwa, waombaji 14,393 wamejiajiri na waombaji 58,916 wasio na ajira. Tazama takwimu kama ilivyooneshwa hapa chini.​

1658823275435.png

Takwimu za walioomba ajira za mda mfupi za Sensa mwaka 2022.

Ukijaribu kufuatiliia kwa mapana zaidi watu hawa wasio na ajira wengi wao ni vijana, hasa vijana waliomaliza elimu ya chou kikuu. Kwa upande mwingine, asilimia kubwa ya waajiliwa katika kundi hili ni walimu.

Ilivyo kawaida, ajira za muda mfupi za Sensa na nyingine kama kusimamia uchaguzi mkuu, walimu na wafanyakazi wa uma hupewa kipaumbele zaidi. Kwa mwaka huu, hasa kipindi hichi cha Sensa imekua ni tofauti kidogo hivyo imepelekea mitazamo tofauti tofaauti baina ya makundi haya katika jamii na mitazamo hii ikiangaziwa kwa umakini inaweza kua kama chachu inyochochea mabadiliko ya elimu (fikra) na maendeleo ya kiuchumi katika jamii na taifa kwa ujumla. Mitazamo hii ni kama ifuatavyo;

Mitazamo Pinzani.
Sehemu hii inaonesha mitazamo kuwa, si vyema ajira za muda mfupi za Sensa kupewa vijana ambao kwa upande mwingine wanaweza kujishughulisha na shughuli nyingine za kiuchumi. Mitazamo hii ni kama ifuatavyo;
  1. Kudumaa kwa akiri na utendaji kazi kwa vijana. Jamii inatoa hoja kuwa, vijana kupewa ajira hii inawafanya wadumae kifikra na kubweteka, hali ambayo inawapelekea wasifikirie njia mbadala ya kutumia elimu walioipata katika kutatua matatizo katika jamii na kuweza kujikwamua kiuchumi.​
  2. Vijana wanapenda njia rahisi na mkato zisizo na Subira. Jamii inaeleza kwamba, wimbi kubwa katika ajira hizi limetokana na kuwa vijana wengi wanaamini kuwa kuna malipo na posho nono ambazo watapata nakuweza kutimiza mahitaji yao.​
Mitazamo Changizi.
Sehemu hii inaonesha mitazamo kuwa, ni vyema ajira za muda mfupi za Sensa kupewa vijana. Mitazamo hii ni kama ifuatavyo;​
  1. Ni chanzo cha mtaji na pesa za kujikimu katika kipindi cha kutafuta ajira za muda mrefu. Vijana wanadai kuwa, wengi wao pindi wanapomaliza kipindi chao cha masomo, pindi wakisubiri matokeo pamoja na vyeti wanakumbana na changamoto ya mtaji katika kujiajili pia kunakua na gharama ndogondogo za kujikimu na kufanya aprikesheni za ajira za fani walizosomea. Hivyo wanaona ajira hizi za muda mfupi ni kama baraka kwao katika kuepukana na tatizo hili.​
  2. Ni fursa au njia ya kujitoa kwa kutumia elimu walioipata kwa serikari na ushiriki katika ujenzi wa taifa.

HITIMISHO
Kupitia ajira za muda mfupi zinazotolewa na Serikali, inaonekana ni njia au mkakati wa Serikali kuweza kumfikia mtu mmoja moja na kumuwezesha kusogea kwenye hatua ambayo anaweza kujiendeleza kwani ni ngumu kutoa ajira kwa kila mtanzania. Kwa upande mwingine, mitazamo tofauti katika jamii ni muhimu kwani jamii husika inapata kujifunza na kuzinduka kifikra pale ambapo inakua imejisahau. Hivyo basi, kupitia mitazamo hii ya ajira za muda mfupi za Sensa, jamii hasa vijana, watakua wamejifunza na kupata mawazo tofauti tofauti ya uzalishaji mali na maendeleo ya kiuchumi.​
 
Upvote 4
Ndugu zangu wana JF karibu kuchangia hoja tujifunze kwa pamoja, lakini pia usisahau kunipigia kura hapo mwishoni kabisa ya makala hii palipo na kialama ''^'' kwani kura yakoni muhimu sana.
 
K.Masanja​

View attachment 2304304

Takwimu za walioomba ajira za mda mfupi za Sensa mwaka 2022.

Ukijaribu kufuatiliia kwa mapana zaidi watu hawa wasio na ajira wengi wao ni vijana, hasa vijana waliomaliza elimu ya chou kikuu. Kwa upande mwingine, asilimia kubwa ya waajiliwa katika kundi hili ni walimu.

Ilivyo kawaida, ajira za muda mfupi za Sensa na nyingine kama kusimamia uchaguzi mkuu, walimu na wafanyakazi wa uma hupewa kipaumbele zaidi. Kwa mwaka huu, hasa kipindi hichi cha Sensa imekua ni tofauti kidogo hivyo imepelekea mitazamo tofauti tofaauti baina ya makundi haya katika jamii na mitazamo hii ikiangaziwa kwa umakini inaweza kua kama chachu inyochochea mabadiliko ya elimu (fikra) na maendeleo ya kiuchumi katika jamii na taifa kwa ujumla. Mitazamo hii ni kama ifuatavyo;

Mitazamo Pinzani.

Sehemu hii inaonesha mitazamo kuwa, si vyema ajira za muda mfupi za Sensa kupewa vijana ambao kwa upande mwingine wanaweza kujishughulisha na shughuli nyingine za kiuchumi. Mitazamo hii ni kama ifuatavyo;
  1. Kudumaa kwa akiri na utendaji kazi kwa vijana. Jamii inatoa hoja kuwa, vijana kupewa ajira hii inawafanya wadumae kifikra na kubweteka, hali ambayo inawapelekea wasifikirie njia mbadala ya kutumia elimu walioipata katika kutatua matatizo katika jamii na kuweza kujikwamua kiuchumi.​
  2. Vijana wanapenda njia rahisi na mkato zisizo na Subira. Jamii inaeleza kwamba, wimbi kubwa katika ajira hizi limetokana na kuwa vijana wengi wanaamini kuwa kuna malipo na posho nono ambazo watapata nakuweza kutimiza mahitaji yao.​
Mitazamo Changizi.

Sehemu hii inaonesha mitazamo kuwa, ni vyema ajira za muda mfupi za Sensa kupewa vijana. Mitazamo hii ni kama ifuatavyo;
  1. Ni chanzo cha mtaji na pesa za kujikimu katika kipindi cha kutafuta ajira za muda mrefu. Vijana wanadai kuwa, wengi wao pindi wanapomaliza kipindi chao cha masomo, pindi wakisubiri matokeo pamoja na vyeti wanakumbana na changamoto ya mtaji katika kujiajili pia kunakua na gharama ndogondogo za kujikimu na kufanya aprikesheni za ajira za fani walizosomea. Hivyo wanaona ajira hizi za muda mfupi ni kama baraka kwao katika kuepukana na tatizo hili.​
  2. Ni fursa au njia ya kujitoa kwa kutumia elimu walioipata kwa serikari na ushiriki katika ujenzi wa taifa.

HITIMISHO

Kupitia ajira za muda mfupi zinazotolewa na Serikali, inaonekana ni njia au mkakati wa Serikali kuweza kumfikia mtu mmoja moja na kumuwezesha kusogea kwenye hatua ambayo anaweza kujiendeleza kwani ni ngumu kutoa ajira kwa kila mtanzania. Kwa upande mwingine, mitazamo tofauti katika jamii ni muhimu kwani jamii husika inapata kujifunza na kuzinduka kifikra pale ambapo inakua imejisahau. Hivyo basi, kupitia mitazamo hii ya ajira za muda mfupi za Sensa, jamii hasa vijana, watakua wamejifunza na kupata mawazo tofauti tofauti ya uzalishaji mali na maendeleo ya kiuchumi.​
makala nzuri sana hii, kwa kutizama hiyo chati ni ukweli usiopingika yakuwa asilimia kubwa hawana ajira.
Serikali itumie takwimu hizi kupima kipato cha raia wake na itafute mbinu za kuwainua. 👍
 
Back
Top Bottom