Una tv ngapi? Simu janja ngapi? ... ni kuombea misaada tu hayo?hii ni Sensa ya kuombea misaada Tu,Sensa haijawahi kupanga maendeleo tanzania
Tozo na kodi zaidi ya mara moja, ni wizi hata kama ni %0.001
Kwanini watoze zaidi ya mara moja?
Kamshahara kenyewe kaduchu kameshakatwa PAYE, (Japo wanakata more than 10%, na wanasema ni single digit lakini wanakata zaidi)
Hii serikali, kinachozungumzwa hadharani na wanavyotenda ni tofauti kabisa. Na huo ndio ukweli. Hata kama watu watafukuzwa kazi au kulazimishwa kujiuzulu kwa kusema ukweli; bado ukweli utabaku kuwa ukweli daima!
Kodi za makazi, kodi za ardhi, tozo za miamala, tozo za kutoa na kuweka, VAT kwenye bidhaa, mikopo, royal tour, uwekezaji, lakini bado hakuna kinachofanyika!
Miradi ni ile ile kila kukicha! Tunaweka jiwe la msingi, tunafungua mradi x... Baadhi ya viongozi wamegeuza hii miradi kuwa vitega uchumi kwa maslahi yao binafsi!
Tutaendelea kuwa na uchumi tegemezi hadi lini?
Rasilimali za nchi ni nani wanazifaidi?
Fedha za royal tour, mikopo na uwekezaji zinafanya kazi gani?
Kodi na tozo zaidi ya mara moja kwa kipato hicho hicho, ni uonevu!
Inaumiza sana ni basi tu.Zingatia nyongeza iliyotolewa kwenye mishahara mei mosi kwa wote walioongezwa haitoshi kulipia tozo kwenye kuuchukua mshahara wote bank.
Wanasema huwa hatujashindwa kuzowea. Hivyo wanatuchukulia poa poa tu.Inaumiza sana ni basi tu.
Na tatizo la hizi tozo ni kwamba, hazina uwiano sawa kwa wenye vipato vikubwa na vidogo.
Mtu anatuma pesa kwa ndg, jamaa, rafiki anakatwa tozo, yule aliyetumiwa naye anakatwa tozo. Na wakati huohuo taasisi na makampuni nayo yameongeza makato! Na bado watawalipa serikali gawio lao
Hivi wanatuchukuliaje lakini? Mbona wao viongozi hawaoneshi kuunga mkono jitihada kwa kupunguza mishahara yao mikubwa na misafara?
Mtu anatoka jirani kabisa na ofisi lakini anatumia msafara wa magari mengi!