Separatus Fella awaasa Watumishi wa Umma kuhusu Ulevi na Rushwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Separatus Fella

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi wapya 80 ambao wameajiriwa hivi karibuni ikiwa ni Mpango unaoandaliwa na Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu katika kuwaandaa waajiriwa wapya kuendana na Misingi ya Maadili ya Utendaji kazi katika Utumishi wa Umma.

Akifungua Mafunzo hayo huku akimwakilisha Katibu Mkuu, Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Separatus Fella amewataka watumishi hao wapya kujiepusha na masuala ya kupokea rushwa na Tabia Za Kilevi ambazo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyika Jijini Dodoma huku mada mbalimbali ikiwemo elimu ya afya, elimu ya ustaafu,utoaji huduma na muundo wa Serikali na jinsi inavyofanya kazi kufikisha huduma kwa wananchi.




 
Hiv kilá watumishi wapya pamoja na walimu wanafanyiwa hivi au hizi ni Special kada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…