poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 453
- 175
Septemba 03, 2021, Bondia Hassan Mwakinyo anataraji kupambana na Bondia kutoka Namibia Julius Munyelele Indongo mwenye umri wa miaka 38 katika pambano la kugombea mkanda wa ABU (African Boxing Union) uzito wa Super Welter katika ukumbi wa Kilimanjaro Hall, Ubungo Plaza, Dar-Es-Salaam.
Rekodi ya Bondia Julius Indongo amepigana mapambano 26, ameshinda 23 na kupigwa 3 yote kwa KO na hana droo. Katika mapambano yake manne ya mwisho ameshinda moja kwa TKO na kupigwa matatu kwa KO.
Pambano lake la mwisho ni November 27, 2020 dhidi ya Daniyar Yeleussinov ambalo alipigwa kwa TKO.
Kumbukumbu zinaonesha mwaka 2015 Machi 20 alipigana na Bondia Ibrahim Class huko kwao Namibia katika ukumbi wa Ramatex Factory, Windhoek na akashinda kwa pointi kwa kupewa ushindi na majaji wote. Mcheza kwao hutunzwa. Nyumbani bondia anapoteza kwa KO sio Pointi.
Ni bondia anayetumia staili ya Southpow. Kwa uoni wangu ni Bondia mtelezo kama ganda la ndizi kwa Mwakinyo. Hamalizi Raundi Tano atakua ameshakalishwa chini. Tutafute mabondia wazuri zaidi wa kumchallenge bondia wetu.