Septemba 29, 2024: Siku ya Moyo Duniani, Wanaopoteza maisha kila mwaka kwa Magonjwa ya Moyo wafikia Milioni 18.6

Septemba 29, 2024: Siku ya Moyo Duniani, Wanaopoteza maisha kila mwaka kwa Magonjwa ya Moyo wafikia Milioni 18.6

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
1727588031749.png
Siku ya Moyo Duniani huadhimishwa Septemba 29 kila mwaka tangu ilipoanzishwa na Shirikisho la Moyo Duniani (WHF) kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 1999.
-
Siku hii hulenga kuongeza uelewa kwa Watu kushirikia katika kuzuia, kupima afya mara kwa mara na kubadili mtindo wa maisha. Kwa mujibu wa WHF, Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu yanayoongoza kwa kusababisha vifo takriban Milioni 18.6 kila mwaka.
-
Aidha, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge, Magonjwa ya Moyo ikiwemo Shinikizo la Damu, yanachangia 13% ya Vifo vinavyotokea nchini.

>>
1727588045322.png
ULAJI wa vyakula vyenye wanga hasa saa chache kabla ya mtu kwenda kulala, kunatajwa kuwa hatari kwa afya, hususan Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs), ukiwamo ugonjwa wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Peter Kisenge, ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani.

Pia soma: Magonjwa ya Moyo ndio Muuaji Mkuu kwasasa Duniani

Siku hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Septemba 29, lengo ni kuikumbusha jamii kupima afya angalau mara moja au mbili kwa kipindi kisichopungua miezi 12.

Akifafanua zaidi kuhusu siku hiyo, mbele ya waandishi wa habari, Dk. Kisenge ambaye pia ni bingwa wa magonjwa ya moyo, anasema idadi ya wanaougua maradhi hayo inakua, akisema kauli mbiu mwaka huu: Tumia moyo wako chukua hatua, ujilinde na magonjwa ya moyo na uwasaidie watu wengine.

“Duniani kote takribani watu milioni 17 hupoteza maisha kutokana na magonjwa ya moyo kila mwaka. Kwa nchi yetu tatizo hili limefikia asilimia 13, huchangia vifo vingi hasa vya ghafla. Kuna magonjwa ya mishipa ya damu, valvu na presha.

Vitu vinavyochangia sana magonjwa ya moyo ni pamoja na uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, unene uliokithiri, kutozingatia lishe, kula sukari nyingi na ulaji wa wanga hasa kula wakati umechelewa usiku sana, unachangia unene, hatimaye magonjwa ya NCDs

JKCI tunaadhimisha siku hii, kwa kufanya matembezi Septemba 28, mwaka huu, kwa kuwaambia wananchi kuwa unapofanya mazoezi unapotembea unaepusha magonjwa haya kwa zaidi ya asilimia 10,” amesema Dk. Kisenge.

Amesema pia maadhimisho hayo kwa siku ya pili, Septemba 29, mwaka huu JKCI itatoa huduma bure za vipimo na matibabu kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam, katika kambi itakayofanyika eneo la Kawe.

Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto JKCI, Dk. Sulende Kubhoja alisema upande wa watoto chini ya miaka 18 wengi huugua magonjwa hayo ikiwa ni tangu kuzaliwa kwao, tofauti na watu wazima ambao sababu ni mtindo wa maisha.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Dar Group-JKCI, Dk. Tulizo Sehemu, amesema viwango vya wagonjwa wanaotibiwa katika tawi hilo la taasisi hiyo kwa siku inafikia wagonjwa 500 hadi 600.



World Heart Day is a global reminder to take care of the heart. Cardiovascular disease is the world's number one killer. According to the World Heart Federation, conditions affecting the heart or blood vessels such as heart attacks, stroke and heart failure kill more than 20.5 million people every year. World Heart Day creates awareness about the importance of keeping a healthy heart via various global activities.
World Heart Day Date
World Heart Day is observed on September 29 every year to raise awareness about heart disease and preventive measures that can help prevent and manage cardiovascular diseases.

Theme of World Heart Day
From 2024 to 2026, the campaign will centre around the theme "Use Heart for Action," urging individuals to prioritize their heart health while encouraging them to demand that leaders take cardiovascular health seriously. This theme creates a global platform for meaningful initiatives, highlighting the importance of intentional and impactful efforts. It represents a transition from merely raising awareness to empowering people with clear objectives and a sense of purpose. The term "Action" reflects a dual approach that aims to influence policies and promote behavioural changes and physical activity, underscoring the necessity for sustained efforts and collaboration.

History of World Heart Day
World Heart Day was established by the World Heart Federation (WHF) in partnership with the World Health Organization (WHO) in 1999. The first official observance occurred on September 24, 2000, aiming to raise awareness about the rising impact of heart disease and stroke. Both conditions are largely preventable through healthy lifestyle choices, and the initiative was launched to promote global awareness and encourage preventive actions. Initially, the day was observed on the last Sunday of September, but in 2011, the WHF set the date as September 29 each year to standardize the event and increase its global visibility.

Significance Of World Heart Day
World Heart Day is crucial in reducing the global burden of heart disease by promoting preventive practices, regular health check-ups, and healthy lifestyle habits. Cardiovascular diseases are the leading cause of death worldwide, responsible for approximately 18.6 million deaths annually. Campaigns like World Heart Day are vital for educating the public on risk factors and how to manage them.


In many countries, the day is marked by various activities such as free heart screenings, walks, marathons, media outreach, and educational programs, all designed to raise awareness about heart health. Health professionals and organizations also use the occasion to advocate for policy changes that promote heart-healthy environments, such as smoke-free areas, healthier food options in schools, and improved access to healthcare.
 
DALILI ZA UGONJWA WA MOYO

i. Maumivu ya kifua hasa yanayotembea mpaka kwenye mabega, shingo au taya

ii. Moyo kwenda mbio (Moyo kudunda kwa nguvu isivyo kawaida )

iii. Uchovu uliopitiliza, mwili kuwa dhaifu na kuchoka haraka hata kwenye shughuri ndogo

iiii. Kukosa pumzi au kushindwa kupumua vizuri hasa unapolala chali

v. Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

vi. Tumbo kujaa, kichefuchefu na kutapika

vii. Kushindwa kulala vizuri hasa kushtuka usingizini kuhisi kama unakabwa na kukosa pumzi

Hizi ni baadhi ya dalili na mara nyingi mtu huanza kupata dalili wakati ameshaishi na ugonjwa kwa muda mrefu. Ni muhimu sana kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.

#worldheartday #sikuyamoyoduniani #Sik
FB_IMG_1727589292772.jpg
uyamoyoduniani2020
 
DALILI ZA UGONJWA WA MOYO

i. Maumivu ya kifua hasa yanayotembea mpaka kwenye mabega, shingo au taya

ii. Moyo kwenda mbio (Moyo kudunda kwa nguvu isivyo kawaida )

iii. Uchovu uliopitiliza, mwili kuwa dhaifu na kuchoka haraka hata kwenye shughuri ndogo

iiii. Kukosa pumzi au kushindwa kupumua vizuri hasa unapolala chali

v. Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

vi. Tumbo kujaa, kichefuchefu na kutapika

vii. Kushindwa kulala vizuri hasa kushtuka usingizini kuhisi kama unakabwa na kukosa pumzi

Hizi ni baadhi ya dalili na mara nyingi mtu huanza kupata dalili wakati ameshaishi na ugonjwa kwa muda mrefu. Ni muhimu sana kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.

#worldheartday #sikuyamoyoduniani #Sikuyamoyoduniani2020
Nyuzi madhubuti kama hizi zinakosa wachangiaji kabisa.
Labda wanadhani haziwahusu
 
Siku ya Moyo Duniani huadhimishwa Septemba 29 kila mwaka tangu ilipoanzishwa na Shirikisho la Moyo Duniani (WHF) kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 1999.
-
Siku hii hulenga kuongeza uelewa kwa Watu kushirikia katika kuzuia, kupima afya mara kwa mara na kubadili mtindo wa maisha. Kwa mujibu wa WHF, Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu yanayoongoza kwa kusababisha vifo takriban Milioni 18.6 kila mwaka.
-
Aidha, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge, Magonjwa ya Moyo ikiwemo Shinikizo la Damu, yanachangia 13% ya Vifo vinavyotokea nchini.
Katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani leo tarehe 29/9/2024, Madaktari bingwa wa moyo kutokaTaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), wafanya makubwa nchini Zambia.

Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Generali Matthew Edward Mkingule, ametuma salaam kutoka Zambia wakati akiwaaga madaktari hao bingwa, waliokaa nchini Zambia kwa wiki moja, sasa wanarejea nchini usiku huu. Balozi Mkingule, anaeleza zaidi.
View: https://youtu.be/Z3Wly_H4bhE?si=sORNK2XqGk9igyKO

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge amesema taasisi yake katika kuadhimisha siku ya moyo duniani, watatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani. Na kuanzia tarehe 2 -12 October, watapiga kambi Mjini Geita kwenye Wiki ya Madini.

P
 
Inashauriwa watu tujitahidi sana kufanya Kufanya mazoezi na kupunguza uzito usiofaa Yani Obesity hii inasaidia sana kujikinga na maradhi kama haya licha ya Kuwa pia wakati mwingine inaweza tokea mtu akazaliwa na changamoto kama hizo za moyo.
Japokuwa kwa taaluma yangu siyo mtu wa kada ya Afya lakini Ugonjwa huu nimepata kuushudia ni kwa namna Gani ni wa hatari baada ya Kupoteza ndgu yangu mwaka jana kijana mdgo aliyekua mwanataaluma mzuri kwenye hili taifa akiwakilisha Tanzania nnchi za Barafu kwani ilikua mapema sana kwa Umri na Afya njema alokua nayo hapo Awali.
Pia mwaka huu tumeona aliyekua muimbaji maarufu wa Zablon Singer Marco alifariki gafla kutokana na changamoto kama hii hapa hapo tunapaswa tujiulize je ni wangapi Wasokuwa maarufu wanakufa ghafla na changamoto kama hizi za maradhi ya moyo? Na pengine kuuza maswali mengi katika Jamii kama vile kifo kinaweza kimetokea pengine kwa kulogwa?
Sababu nijuavyo Mimi binadamu tunatembea na maradhi bila kujijua.
 
Back
Top Bottom