September AMATB - Niulize Chochote Kuhusu Tehama na Biashara

Mtangoo

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Posts
6,167
Reaction score
5,613
Nimeamua kila nipatapo wasaa kujaribu kusaidia kuelimisha na kushirikisha mawazo wadau mbalimbali juu ya Teknolojia na Biashara, hasa Teknolojia ya Habari na Mawasialiano. So haya na maswali ya Mwezi wa tisa kwenye Ask Me Anything Technology and Business (AMATB). Mambo ya kuzingatia katika mfululizo huu ni:
1. Maswali yasiyo na lengo la kujifunza sitayajibu. Sababu ni kuwa lengo ni kushirikishana ufahamu niliopata neema ya kuwa nao na si vinginevyo
2. Maswali yasiyohusiana na biashara na teknolojia sitayajibu. Hii ni kutunza focus kwenye mada husika
3. Maswali yenye mrengo wa kisiasa sitayajibu. Kwa sababu ni nje ya lengo
4. Maswali kuhusu maisha binafsi sitayajibu. Kwa sababu hii sio Biography. Unless yawe yanahusiana na mada na yatakuwa msaada kwa wasomaji, then nitaangalia namna bora ya kujibu
5. Sipo hapa 24/7 na wala sina msaidizi wa kusoma hapa. So ukiweka swali lako uwe na uvumilivu.

Best rule: Kama usingependa uulizwe swali hilo ni vyema usiulize...!

Karibu!
 
Mkuu ukiachana na mambo ya Subscription, Advertisment na Listing fee njia gani nyingine ziznaweza kutumika kupata revenue kwenye website au app??
Business Models zipo nyingi kutegemeana na aina ya solution unayoitoa. Kama solution inasaidia kutoa huduma za kiserikali unaweza kuangalia namna utafanya partnership na serikali ili iweze kugharamia kwa namna ambayo itafaidika na wewe utafaidika. Hii inaweza ku apply hasa kwa donors kwa maana ya wao kutoa msaada kwa serikali kupitia initiative uliyoianzisha. Kwa maana nyingine solution yako itakuwa ina operate katika kanuni za AZAKI (NGOs), ingawa yenyewe sio lazima iwe ni AZAKI

Pili unaweza kusukuma Product yako nyingine kwa mgongo wa Product maarufu ambayo hupati faida moja kwa moja. Kwa mfano, Google kuna huduma anatoa bure. Tuuite huduma A lakini katika kutumia ile huduma bure anajua kuwa kuna mahali utahitaji huduma B. Kwa hiyo huduma A inakuwa ni bure ila huduma B utalipia. Sasa ukiwa na huduma A ambayo inasababisha huduma B, C, na D kuuzika basi unaifanya A kuwa bure na B, C, na D zitarejesha gharama za uendeshaji na faida. Hii inahitaji uwe na mipango ya muda mrefu na uwekezaji wenye subira.

Mifano halisi ni Kama Android na vitu kama Ramani za Google, Firebase Cloud Messaging na Firebase Database. Na mifano ipo pia sehemu nyingine nyingi.

Hizi ni models mbili ambazo naweza kuongezea kwenye hizo ambazo umekwisha zisema. Kama nitakumbuka nyingine nitaongezea.
Natumai umepata kitu!
 
Appreciated Mkuu, ndo maa game kama fortnite huwa tunanunua v-bucks alafu tunazitumia ku fanya payment vya vitu kama nguo na kupata battle pass, ndo maa hawa jamaa wanapata ele japo game ni free
 
Yup! Ina maana hapo ana partnership na wauza vitu, anawaletea wateja then yeye anapata comission na game inakuwa "free"
 
Appreciated Mkuu, ndo maa game kama fortnite huwa tunanunua v-bucks alafu tunazitumia ku fanya payment vya vitu kama nguo na kupata battle pass, ndo maa hawa jamaa wanapata ele japo game ni free
Mkuu Fortnite unacheza kwenye platform gani?
 
Unadhani ni kwanini e-commerce bado haijafanikiwa sana kwa Tanzania, je sisi kama developers tuje na model/ mbinu gani kuwin zaidi upande wa e commerce?
 
Matatizo kwenye e-commerce ni mengi sana ila kwa uchache kuna observations kadhaa nimeziona:
1. Hakuna Mifumo thabiti na rahisi na nafuu ya malipo. Ili kuendesha eCommerce, unahitaji kuwa na mifumo thabiti ya malipo ambayo itakuwa reliable na bado iwe nafuu. Mwanzoni tulikuwa hatuna mifumo angalau ya kueleweka. Kwa sasa tuko angalau na mifumo ya malipo lakini tatizo ni charges. Kwa sababu ili uweze kuwa na eCommerce ambayo itavutia watu, lazima ishushe gharama ukilinganisha na namna iliyozoeleka. Kama nyanya nanunua kwa 1000 sokoni, tena nachagua mwenyewe, na gharama yote ni 1200, kwa nini nitumie eCommerce ambapo nanunua kwa 2000? Hapo convinience bado sio convincing factor

2. Addressing system yetu bado ni mbovu. eCommerce inavutia ikiwa na delivery. Kufanya delivery kwetu bado ni issue kwa sababu hatuna reliable addressing mpaka angalau kwa level ya mitaa. Kuna nchi zingine mitaa yote ina address, so kuniletea kitu nyumbani sio tatizo

3. Bado hakuna kampuni iliyoamua kufanya eCommerce seriously na kutafuta suluhu ya matatizo haya na mengine. Zilizopo sio eCommerce per se, bali ni kama listings, sehemu ya kufanyia udalali.

Haya kwa ufupi ndio naweza kuyasemea kwa sasa. Ila sio matatizo pekee. Yapo mengine mengi na ya msingi sana!
 
Je sisi kama developers tuje na model/ mbinu gani kuwin zaidi upande wa e commerce?
Cha kwanza ni kile huwa nawashauri developers siku zote, jifunze kuwa developer mzuri. Acha kelele nyingi na piga kazi sana. Pata uzoefu. Pili anza na kitu kidogo tu. Mfano kama una ndoto za kuwa Amazon ya Africa, anza na 1/1,000,000 ya Amazon ya sasa. Chagua kitu kidogo sana na uhakikishe unakifanya vizuri, kiTeknolojia, na kiBiashara.

Kikianza kukua hakikisha unaweka mifumo ya usimamizi ya kibiashara. Kama huna karama ya kusimamia tafuta mtu na wewe ubaki kama developer. Sio kila dev anaweza uongozi.

Mwisho hakikisha uko vizuri kwenye "Compliance". Najua kwetu kuna "Bureaucracy" lakini hakikisha umekaa vizuri kisheria na kiutaratibu. Yote haya yatachukua muda, so hakikisha una akiba ya kutosha ya uvumilivu!
 
Nashukuru sana mkuu kwa ufafanuzi mzuri, nimepata kitu hapa si haba
 
Ubarikiwe sana mkuu,
 
Mkuu mi naomba uni connect na developer yyte wa ios unae mfahamu kama hutojali
 
Mkuu nini mawazo yako kuhusu uwekezaji kwenye cryptocurrencies kwa sasa na baadaye

Je unaweza kuwashauri watu kuwekeza huko fedha zao
 
Back
Top Bottom