SoC02 Sera huru itakayotatua tatizo la ajira na kupandisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kupitia tozo nafuu

SoC02 Sera huru itakayotatua tatizo la ajira na kupandisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kupitia tozo nafuu

Stories of Change - 2022 Competition

Kelvin peter kisena

New Member
Joined
Jan 30, 2022
Posts
4
Reaction score
1
Tanzania ni nchi yenye wananchi walio na amani na subira sana mbele ya utawala lakini mioyoni na ndani ya fikra zao wameghubikwa na huzuni, mifadhaiko na hali duni ya maisha

Wananchi wengi wa kitanzania asilimia 72% wanatumia nguvu nyingi ili kuweza kuzungusha pesa na maisha yao ya kila siku

Tanzania ni moja ya nchi Afrika inayokua kwa kasi katika kusimamia basic education [elimu ya msingi] hii nikufatiwa na sera ya elimu ya elimu bure chekechea hadi kidato cha sita pamoja na ufadhilii unaotolewa elimu ya juu

Lakini sambamba na hayo tatizo la ajira pia nalo lipo mbele tena kwa kasi kubwa sana, wengi wa watanzania wanafikiri ni kwasababu ya wahitimu wengi vyuoni ambao wamejikita kinadharia tuu ila sio nadharia pamoja na vitendo kama ilivyo sera ya mtaala [competent based education] .ila chanzo cha haya yote ni sera za utawala ambazo sio rafiki katika nchi yetu kutatua matatizo ya ajira pamoja na kukuza nchi kapitia TOZO NAFUU [ affordable and conducive tax]

Kwamienendo ya kisera na falsafa ya dunia, falsafa inayotawala na inayoweza kuendana na maendeleo ya taifa letu kwa haraka sana ni falsafa ya capitalism [kibepari] na hii ni kwasababu zifuatazo

1. Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na kila primary products[zao la kwanza,naturaly] ya kila sekta mfano uoto wa asili ambao taifa linaweza kuuendeleza na kuwa chachu ya utalii.madini,mazao ya majini mfano samaki asilia,watu na utamaduni, mazingira mfano milima na kandokando ya bahari. Ukitofautisha na nchi nyingine ambazo hazina badala yake zinategemea katika artificial au Man made tools hivyo kila sekta hapa Tanzania ina mtaji wa awali kupitia hizo primary products ambazo zitawezesha wawekezaji ndani na nje ya nchi kutoa TOZO na wananchi kuwapunguzia TOZO,,,Kama ilivyokawaida mtoaji mkuu wa tozo katika taifa lolote mara nyingi ni haya makampuni binafsi na mashirika binafsi na sio makampuni au mashirika ya umma hivyo serikali naomba katika suala la uwekezaji ni vizuri zaidi wakapanua wigo wa hawa NGOs

2. Suala lingine ni nature ya utawala wa Tanzania,, viongozi karibu wote waliopo madarakani sio wazalendo
Mzalendo kwa mjibu wangu katika taifa hili ni mtanzania yeyote ambaye yupo tayari kuliona taifa pamoja na watu wake anawatoa au anawasaidia katika kutoa mchango wa namna gani tutaingia hatua nyingine ya uchumi ulioimarika zaidi tena kwa mwananchi mmoja mmoja ,, ukweli ni kwamba suala kubwa katika nchi hii ni uchumi na ndio chanzo cha mambo mengine mfano wa mambo hayo ni wizi,uwanzishwaji wa vyama vya siasa kwa kiholela [masilahi binafsi] pamoja na mambo machafu kama kukithiri kwa ushoga na ukahaba.. yote hii imesababishwa na urithi wa madaraka na urithi wa umasikini.

URITHI WA MADARAKA
Nini maana ya mtoto wa bilionea kumpa bilionea ya mtoto mwingine.. maana ake nikwamba baada ya mtu fulani kuwa na kiasi cha zaidi millioni 400 huyu hapaswi kabisa kuwa agent wa serikali badala yake awezekeze katika sekta binafsi ambazo atatoa faida tatu kuu katika jamii
  • Kwanza atatoa TOZO serikalin
  • Pili ataajiri watanzania
  • Tatu ataendesha familia yake
Na kubwa zaidi hyo nafasi alokuwa nayo serikalini angechukua mtoto wa maskini nayeye kujipatia mtaji wa kuelekea kuwa na NGOs ambayo ndio mtoa tozo mkuu wa serikali

Suala la viongozi kukaa madarakani na wafanyakazi serikalini kukaa kwa muda mrefu ni chanzo cha umaskini pia Kwan Mimi ningependekeza kwamba serikali liwe chimbo tu la mtaji wa maskini baada ya mda fulani miaka 10 na sio 40 awe amestaafu kazi za serikalini na kwenda kuwekeza hasa katika sekta binafsi na mashirika mengine binafsi ili tu awe mtoa tozo mkuu na Aachie fursa ya ajira kwa wengine kupitia vacancy na ajira atakazo toa kwa kufanya hivyo tutasonga mbele sana

Niaongea hivi nikufatiwa na uchunguzi niliofanya nikiwa mwaka wa kwanza tuu chuo kikuu mwaka jana,. ILIKUWA HIVI wanafunzi 100 niliowafanyia utafiti kwa swali la saba kwamba nini malengo yako baada tuu ya kupata ajira serikalini
Majibu yalikuwa hivi

Asilimia 70 watachukua mikopo ili waanze mambo mengine ya kimaendeleo huku wakiwa wanafanya kazi na kujenga nyumba pamoja na kuinua ndugu

Asilimia 10 watachukua Mkopo na kuacha kazi zao waanzishe sekta binafsi

Asilimia 5 walisema wasubiri mda ufike

Asilimia 15 walisema hawajui


Hivyo basi tukikomesha urithi wa madaraka tutaachia milango ya maskini wengi sana

Pia suala la urithi wa umaskini linaendana sambamba na urithi wa madaraka Kwan tayari kuna madaraja makuu mawili ndani ya taifa hili yashajigawa lile lenye diesel 3500 na lenye diesel bure na falsafa ya mtanzania wa asili kabisa anaamini kutoka daraja la 3500 per lita moja kwenda bure ni ngumu sana. Utafiti niliofanya pia mwanzoni mwa mwaka huu wanafunzi wengi wanatokea familia maskini wanafanya vizuri sana katika mitihani yao ya mwisho lakini mwishoni wanaishia ajila za tamisemi tu ambazo hazina interview na kwa hali ya kawaida hizo AJIRA hazina ujira mkubwa sana ukiachana na ajira za interview kama ENGEERING ambapo wengi watanzania wanaamini ajira za hivyo ni za wachache ambazo ni connection

Hivyo bas naomba kuwasilisha katika shindano la story of changes [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Upvote 0
Back
Top Bottom