Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha CHAUMA, Hashimu Rungwe amejikita katika ahadi ya kuhakikisha watanzania wanapata lishe bora kwanza, wali-kuku imekuwa ndio kibwagizo chake, na amekuwa akijitahidi kulitekeleza hilo kwa vitendo kwenye kampeni zake kwa kuleta kweli wali na kuku, na wananchi kuutafuna.
Hashimu Rungwe amekuwa akisisitiza kuwa mtu akila chakula kizuri na bora basi atafurahia maisha yake na pia ataweza kufanya jambo lingine lolote kubwa la kimaendeleo.
Kwa upande mwingine mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli naye ameibuka na sera mpya ya kuwaahidi watanzania kuwa ikiwa atachaguliwa tena kuwa rais wa Tanzania basi ndani ya kipindi cha miaka mitano ataifanya Tanzania kuwa kama Ulaya. Yeye akimaanisha kuwa kiwango cha kimaisha kwenye kipato cha mtanzania mmoja mmoja kitakuwa juu, miundo mbinu muhimu itaboreka na huduma za kijamii zitakuwa bora katika uwiano unalingana au kukaribiana sawa sawa na Ulaya.
Kwa kuwa hiki ni kipindi cha kampeni, na kila mgombea anaweza kusema chochote, ni vizuri pia tukajadili hapa JF kuona kama hizo ni ahadi zenye kuweza kutekelezeka ama la.