xack
New Member
- Aug 15, 2022
- 2
- 1
MBINU MPYA ZA KUBORESHA MAISHA YA WAFUNGWA
UTANGULIZI Napenda kumshukuru Mungu kwa ajili ya uhai alionipa na kunijalia mawazo mazuri ya kuandika ili jamii yangu iweze kuimarika, napenda kutumia nafasi hii kuandika kwa ajili ya rafiki zangu, ndugu zangu na jamaa yangu walio nyuma ya nondo za magereza katika sehemu mbalimbali nchini tanzania wakitumikia adhabu zao pengine walikusudia kufanya makosa ama wengine wamesingiziwa
Ninaona faraja na furaha kuwakumbuka katika andiko langu nikijua fika mimi pia naweza kuwa mfungwa mtarajiwa muda wowote.
TAASISI HURU YA WAFUNGWA AFRIKA
Tunajua fika wafungwa wa Afrika wanapitia Changamoto nyingi katika maeneo yao ya adhabu mataifa mengi yana sheria ya namna ya kushughulika na wafungwa pamoja na mahabusu.
Taasisi hii itakuwa ni taasisi huru yenye kutunga sheria ambazo kili mwanachama wa nchi huru za Afrika ataweza kuzifuata ilikujenga utu, haki na ubinadamu hatukuja hapa kubariki makosa waliofanya bali tuko hapa kuelekeza jinsi tunaweza kuwa na sehemu nzuri za magereza zilizo salama kwa ajili ya binadamu wanaojisahau. Afrika ni moja tupendane na kuelekezana katika kujenga kizazi kilicho bora
Sheria hizi zitamlazimu kila mwanachama aweze kutia sahihi ili kuweza kuzifuata kila mtu anaweza kuwa mfungwa muda wowote nina furaha na shauku kuwasilisha muswada huu katika baraza la Umoja wa Arika.
Wakati tunaendelea kufanya tafiti juu ya changamoto za wafungwa ni vibaya kusahau kundi la Askari magereza katika jamii ya wafungwa ni kama kujitoa muhanga na kuacha yote ili uweze kumlinda mfungwa asitoroke . Pia tunaangazia namna bora ya kuboresha maeneo yenu ya kazi yawe mazingira rafiki ili muweze kufany kazi kwa furaha na ufanisi.
CHAMA CHA WAFUNGWA NA MAHABUSU TANZANIA
Kuwepo kwa chama cha Taasisi huru kama hii Tanzania itasaidia kuwepo kwa haki za wafungwa na mahabusu.
Zifuatazo ni faida za kuwa na Chama hichi huru Tanzania
- Kufuatilia kesi ambazo zina ukakasi dhidi ya wafungwa
- Kuwepo kwa Elimu katika mazingira ya wafungwa kwani kifungo si mwisho wa maisha stadi za kazi
- Uendelezaji wa fani husika juu ya wafungwa
- Wafungwa wenye fani kupata kipato/ kulipwa ili waweze kuboresha Uchumi wa familia zao.
- Kuzingatia usalama wa Afya za wafungwa
- Adhabu zinatolewa ziangaliwe upya zinapelekea Ulemavu kwa baadhi ya wafungwa
- Malazi na chakula bora kitolewe bila kuzingatia ubaguzi
- Maabusu waachiwe kama hawana hatia
- Adhabu haiwezi kubadilisha tabia ya mtu pekee mbinu za ziada zinahitaji elimu ya Uraia
- Ushauri nasaha ni muhimu kutolewa kwa wafungwa na mahabusu ili kuboresha Afya ya akili.
- Utafiti wa ziada juu ya makosa wanayofanya wafungwa ufanywe katika jamii hii itasaidia kupunguza makosa na wafungwa magerezani kwa sababu kuna wengine wanasingiziwa kesi na hawapati haki yao
- Upendo kutoka kwa familia zao / kutembelewa ni muhimu kupiga simu ili kutengeneza mahusiano mazuri na familia zao.
- Wafungwa waweze kupata haki ya kupata taarifa na kutoa maoni yao
- Tunashauri Elimu itolewe bure kwa wafungwa kama sehemu ya kuwa na jamii bora baada ya kifungo kuisha, mfano kuna wafungwa wengine ambao walifanya makosa pindi walipokuwa wanasoma ,hivyo basi tunashauri kuwepo kwa utaratibu mzuri wa kuwapa nafasi ya kumalizia au kuendelea na masoma yao ili hali ni wafungwa.
- Kuwepo kwa siku ya wafungwa duniani / Afrika Tanzania. Wafungwa watakuwa wanakumbuka hali ngumu walizowahi kupitia kwenye maisha yao pamoja na familia zao, pia kukumbuka baadhi ya ndugu na marafiki waliokufa wakiwa gerezani, siku hii itakuwa maalumu kwa watu wote waliowahi kufungwa,lakini napendekeza iwe ni siku ya kuwekwa huru kwa baadhi ya wafungwa ambao wako ukingoni kumaliza adhabu zao.
- Wafungwa kupata haki ya kupiga kura kuchagua na kuchaguliwa kuwasilisha mawazo yao katika kujenga nchi yao.
JELA SOKO - Jela soko ni kusanyiko la pamoja la wafungwa ambalo litakuwa linauza bidhaa mbalimbali zitokanazo na nguvu kazi ya wafungwa pamoja na bidhaa za kibunifu za wafungwa ili kuondoa mtazamo hasi juu ya wafungwa kutokuchangamana na raia. Ni vyema kuwa na jela soko hii itarudisha imani kwa raia na kwa wafungwa. Tunajua fika ni ngumu wafungwa kuchanganika na raia kutokana nasababu mbalimbali ila tunataka kujenga jamii bora ya wafungwa huru. Uwepo wa soko jela itasaidia wafungwa kuuza na watu kununua baadhi ya bidhaa mbalimbali za wafungwa
- Faida ya jela soko itasaidia kuboresha mazingira mazuri ya wafungwa. Pia Askari magereza watafaidika na jela soko ikiwemo kuuza na kununua baadhi ya bidhaa.
- Hii ni njia nzuri ya kufaidika na wafungwa / mahabusu. Lakini pia nataka kubadilisha mtazamo hasi juu ya wafungwa.
ZIADA - Kuwepo kwa wanasheria huru watakaoweza kufuatilia makosa au kesi wanazotuhumiwa wafungwa.
- Kuwepo kwa kitengo au taasisi maalumu ya uchunguzi ambayo haitokuwa na mafungamaono na serikali kwa ajili ya uchunguzi wa adhabu zitolewazo kwa wafungwa kulingana na makosa yao.
- Nashauri wahamiaji walowezi au haramu wasiwe wafugwa katika taifa husika licha ya kukamatwa na makosa mbalimbali ikiwemo kuingia nchini kinyume na sheria.
- Uhamishaji wa wafungwa kutoka gereza moja kwenda jingine uzingatie ushirikishwaji jamaa ,rafiki au ndugu wa mfungwa ili kuwa na mahusiano endelevu.
- Mafanikio ya andiko hili yatasaidia kubadilisha jamiii ya wafugwa dhidi ya changamoto mbalimbali wanazozipitia sambamba na kuja na mbinu mpya za kuwa na jamii iliyo bora na yenye maadili mema.
Upvote
3