HOJA Sera Mpya ya 'Cashless' itafeli, sababu ni hizi

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mtu anauza bidhaa analipia kodi anataka kutuma hiyo pesa kwa ajili ya matumizi analipia tena kodi ananunua umeme ambao upo chini ya Serikali na huduma yao analipia kodi tena..
 
sio kwamba hawajui wanajua...issue ni kwamba wakitoa hizo tozo fuko la serikali litashuka watalambaje asali na wakati hawana mbadala mwingine wa kutunisha fuko...zingatia..na sio kwamba hakuna namna nyingine zakutunisha fuko, ila ndo ni miradi ya makumazani wa nchi hii.
 
SIMU ZOTE AMBAZO ZITAKUWA ZINAPOKEA MALIPO MADUKANI ZIWE REGISTERD!....KWA NANNA YA KIPEKEE NAMBA YA SIMU IWEPO KWENYE LESENI!.....(KU-DIVERT MALIPO KATIKA NAMBA NYINGINE ADHABU IWE KUFILISIWA)
Tusio na simu hatuta nunua kitu?
 
Utapaswa kuwa na card,hata kiswaswadu poa tu,
#Maisha ya ulaya ni kadi tu,zingine za gate pass,basi tunakuwa mfukoni na kadi mpaka 7.
Card ya nida wameshindwa kunipa hadi leo, hayo macard mengine labda tuwape miaka 20 kukamilisha
 
Inawezekana ikawa kweli kukurupuka ila sifikiri hivyo.

Tatizo la hao walioko kwenye madaraka wanajiona wao ndio final na wananchi ni watumwa wao hawawajali hata kuwaogopa kabisa.

Mfano fikiria, mbunge (spika wa sasa) anaishauri serikali kuongeza tozo kwy line ya simu ikiwa kama mbinu ya kuongeza mapato ya serikali πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kujua wao ndio wamiliki wa nchi na wananchi, angalia wanavyolipana mishahara na marupurupu kibao na bado kama haitoshi, hawakatwi kodi na nasikia hata kwy hizi transactions za simu wao hawana makato.
 
Kumbe Manzese kwa mfuga mbwa wanatumia dollar siku hizi?
 
Well said ,yaani nilipie kitu cha elfu 10 then nikatwe 1,500/= wakati mfukoni nina SHUKA LA MMASAI ,kwanini nisilipe tu cash? Waondoe tozo na tukatwe kidogo maana kwenye hiyo fedha tayari serikali ina kodi yake.
 
SIMU ZOTE AMBAZO ZITAKUWA ZINAPOKEA MALIPO MADUKANI ZIWE REGISTERD!....KWA NANNA YA KIPEKEE NAMBA YA SIMU IWEPO KWENYE LESENI!.....(KU-DIVERT MALIPO KATIKA NAMBA NYINGINE ADHABU IWE KUFILISIWA)
Una fikiria kimaskini, serikali yetu pekee ndio inawaza kudhibiti na ku control kila kitu... ni njia ya kufanya watu wako kua watumwa

Watu wakiwa na mifumo rafiki hauhitaji kua na fikra za kikoloni au kiutumwa namna hii
 
maendeleo huambatana na gharama, tusiogope mabadiliko πŸ’
Dunia ya sasa inaangazia kurahisisha, kuounguza gharama, kupunguzq mzigo na automatically the population hufata

Kwetu huku ni kutumikisha, kulazimisha wakati mazingira rafiki hayapo.
Kaa kwa dakika kumi uangalie matangazo ya nchi mbali mbali hata ya kitaasisi za serikali, ni lugha za kurahisisha huduma.

Tanzania yetu ni uthibiti, kupiga fine, kutishia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…