Chachasteven
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 1,941
- 2,044
Jana nimekuwa kwenye usaili (interview) na Kijana mmoja mwenye uzoefu mkubwa wa kazi na mwenye kujiamini akashindwa kupata kazi kwa sababu hajui kiingereza vizuri. Kazi ilikuwa inahitaji mtu mwenye ueledi wa lugha ya kiingereza na kiswahili.
Sasa najiuliza endapo Sera mpya ya elimu itatekelezwa na Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia toka shule za msingi hadi chuo kikuu, hawa wasomi wa Kitanzania wataishi dunia ipi?
Mtazamo wangu ni kwamba wasomi wa Kitanzania watakaotokana na sera mpya ya elimu watakuwa na chuki dhidi ya Watanzania wachache waliobahatika kupitia mfumo wa elimu ya English Medium (msingi hadi chuo) pia kuwa na chuki dhidi ya wageni watakaokuwa na uwezo wa kukimudu kiingereza na kiswahili kwa sababu hawatakuwa na uwezo wa kushindana na wasomi hawa wanaoweza kuzungumza lugha ya kigeni.
Pendekezo: Ili sera mpya ya elimu izae matunda ni lazima sera ya uwekezaji ibadilishwe na vilevile sera ya ajira itazamwe upya. Sera ya uwekezaji lazima iweke bayana kwamba lugha itakayotumika kwenye mikataba na mawasiliano ni KISWAHILI.
Hii itawafanya wageni ndio wajifunze lugha yetu ili waweze kuwasiliana nasi na SIYO Watanzania kujifunza kiingereza ili waweze kuwasiliana na wageni ndani ya Tanzania.
Japo lugha zote zinaweza kupewa kipau mbele. Sera ya Ajira ni lazima iweke bayana kwenye ajira zote nchini Wazawa wanatakiwa kuwa asilimia kadhaa kuanzia ngazi ya menejimenti hadi ngazi ya chini. Wasimamizi wa sera hizi tatu lazima watekeleze majukumu yao.
Kwa kifupi sera ya elimu ni lazima iendane na sera ya uwekezaji na sera ya ajira!