Sera mpya ya elimu na mafunzo, je tunajadili baada ya kusikia au kuisoma?!

Sera mpya ya elimu na mafunzo, je tunajadili baada ya kusikia au kuisoma?!

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Ni vyema tusijadili sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 kabla ya kuisoma na kuielewa. Mfano kwenye lugha ya kufundishia, sera imeshindwa kuchagua lugha ya Kiswahili pekee kuwa ya kufundishia and kujifundishia. Badala yake sera imeweka lugha zote mbili - Kiswahili na Kiingereza kuwa za kufundishia na kujifundishia katika ngazi zote za elimu na mafunzo (angalia attachment ukurasa kati ya 35 n 38)

Pia sera imeonesha umuhimu wa lugha zote mbili na kusema wazi ili kuingia kwenye anga za kimataifa English ni muhimu. Halafu eti Kiswahili na chenyewe kinaenea kwenye mabara.

Cha kushangaza ni kuwa sera imeshindwa kutoa uelekeo katika hili, nafikiri inaziachia taasisi husika za elimu kuamua kama ilivyo sasa kwa baadhi ya pre-primary and primary kutumia lugha ya Kiingereza kama medium of instruction!
 
Huu ni wendawazimu.

Serikali imeshindwa kubaini chanzo na sababu halisi za kushuka kwa elimu.

walianza kuchakachua matokeo kwa kuwaongezea marks kutoka hewani baadhi ya wanafunzi ili kuficha aibu ya serikali kama msemo wa raisi kikwete aliyezalisha aibu tani nyingi kulilko raisi mwingine yeyote aliyeahi kuwepo na naamini hatakuwepo mwingine wa hivi tanzania.

Kuongeza alama hakukutosha wakaongeza madaraja bila kuangalia athari zake kwa taifa.

Wakaanza kutangaza taarifa za uwongo kwamba elimu imepanda (kwa jina la kuficha aibu ya serikali), na matokeo yake sasa tunayaona.

Kana kwamba haitoshi sasa wanafuta mitihani kana kwamba kutahini wanafunzi kunapunguza quality ya elimu. Wanakimbilia kwenye lugha wakiamini kwamba ikifanywa kiswangilishi, kila mtu atafaulu, bila kujali anafaulu nini na kwa maslahi gani.

Swali kwa ccm. Hivi kwa akii zenu, mnadhani kwamba sasa hizi kuna biological evolution imetokea kubwa, katiak uraisi wa kikwte ambao watanzania wamekuwa mijuha kiasi haiwezi kusoma kama waliosoma hapo awali hadi ibadilishiwe lugha?

Ninamtwisha kikwete lawama zote kwa kuchagua watendaji wasio na uwezo wowote kwa maslahi yake bianfsi na familia yake. Taifa limeifka hapa lilipo kwa sababu yake 100%.

NINAOMBA RASI AJAYE, ASIWE AINA YA KIKWETE NA ASITOKE CCM ILI TUBORESHE ELIMU YA NCHI IWEZE KUSTAHIMILI USHINDANI WA KIMATAIFA KATIKA HII DUNIA YA UTANDAWAZI.

TUNAHITAJI RAISI MWENYE ELIMU SAHIHI, UWEZO WA KUONGOZA, NA NIA THABITI YA KULETA MAENDELEO YA TANZANIA KWA KTUMIA RASLIMALI ZETU NA SI UHUNI HUU.
NINADHANI RAISI MSOMI, ATAREVIEW HII SERA JINGA, KUTUMIA WATAALAMU KATIKA TAFITI NA KUZIFANYIA KAZI BILA HILA ILI ELIMU YETU IBOREKE.

HIZI SIASA ZA MAUAJI ZA KIKWETE, HAPANA.!.
 
Nakuunga mkono mkubwa!!.. Kwa kweli ukiangalia kwa jicho pana kwenye hii sera kuna nia ovu ndani yake.. Leo tunalalamika wageni wanachukua ajira zetu ndani ya nchi yetu kisa vijana wanaomaliza vyuo vikuu hawajui kujieleza kwa kiingereza.. Tunakipenda kiswahili chetu na tunakienzi lakini kwenye suala la elimu si la kubahatisha.. Kiingereza ni muhimu sana kuliko kiswahili kwenye dunia ya sasa..

Kila siku wanavutiwa wawekezaji, wawekezaji hawa wakija wanalalamika watanzania hatuajiriki kisa hatujui kiingereza,, halafu hawa MACCM ndo wanaamua kungoa kabisa hata hicho kidogo cha kuombea maji.. Tujifunze kwa wenzetu Afrika Kusini, pamoja na kuwa na lugha tisa rasmi lakini kiingereza ndicho chenye kupewa kipaumbele.. Mtoto atajifunza kizulu lakini kiingereza ndiyo msingi..

Kwa hili KIKWEKTE ndo kaamua kutuponda kichwa kutumaliza kabisa.. Mbona watoto wao hawawapeleki kwenye hizi shule, wanawapeleka nje ili wajue kiingereza.. Nasema no no no,, hii sera hapana inakuja kutuua kabisa...

KATAA CCM TANZANIA IPONE
 
Jiulize kwanin wachina wanatumia lugha yao tuu??? Kingereza ni kama somo!! English ni muhim globally na kiswahili ni muhim kitaifa... think twice broo!! We can't abandon our language at all. No any country in the world has ever done such madness!!
 
Ni vyema tusijadili sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 kabla ya kuisoma na kuielewa. Mfano kwenye lugha ya kufundishia, sera imeshindwa kuchagua lugha ya Kiswahili pekee kuwa ya kufundishia and kujifundishia. Badala yake sera imeweka lugha zote mbili - Kiswahili na Kiingereza kuwa za kufundishia na kujifundishia katika ngazi zote za elimu na mafunzo (angalia attachment ukurasa kati ya 35 n 38)

Pia sera imeonesha umuhimu wa lugha zote mbili na kusema wazi ili kuingia kwenye anga za kimataifa English ni muhimu. Halafu eti Kiswahili na chenyewe kinaenea kwenye mabara.

Cha kushangaza ni kuwa sera imeshindwa kutoa uelekeo katika hili, nafikiri inaziachia taasisi husika za elimu kuamua kama ilivyo sasa kwa baadhi ya pre-primary and primary kutumia lugha ya Kiingereza kama medium of instruction!

Mkuu hivi ushangai hata sera yenyewe imeandikwa kwa Kiingereza.
 
Back
Top Bottom