Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 ni nzuri kwenye makaratasi ila utekelezaji wake hauna maandalizi

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
107
Reaction score
97
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Utawala Bora (OR-TAMISEMI), imeanza utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 kwa Shule za Sekondari kuanzia Januari 2025.

Kwenye makaratasi, sera hii ni nzuri kwani imelenga kukuza vipaji na vipawa vya Wanafunzi, pamoja na kuongeza elimu ya amali kwa watoto wetu ili waweze kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii yetu.

Licha ya mazuri ya sera hii chini ya Wizara ya Elimu, nimegundua kuwa utekelezaji wake utakuwa mgumu sana kwa miaka ya mwanzoni kwa sababu zifuatazo:

Mosi, sera hii haikuwashirikisha wadau wakuu wa elimu ambao ni watekelezaji wakuu – Walimu na Wazazi.

(a) Wazazi:
Wengi hawajui kama kuna Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 ambayo imeanza kutekelezwa Januari hii (2025) kwenye shule zetu. Hawajui kuwa kuna mabadiliko makubwa yamefanyika, ikiwemo wanafunzi kuanza kuchagua masomo kuanzia kidato cha kwanza, tofauti na zamani ambapo masomo yalichaguliwa kidato cha tatu.

Hofu yangu ni kwamba watoto (wanafunzi) watachagua masomo bila wazazi kujua, maana hawana taarifa za yanayoendelea mashuleni. Kama mzazi ana mpango wa mwanae kusoma mchepuo wa sayansi, anaweza kushangazwa akifika kidato cha tatu kugundua mtoto alishachagua masomo ya biashara, ufundi, au sanaa tangu kidato cha kwanza. Hali hii inaweza kuleta sintofahamu kati ya wazazi, walimu na wanafunzi.

(b) Walimu:
Hawa ndio watekelezaji wakuu wa sera hii shuleni, lakini bahati mbaya hawajaandaliwa ipasavyo kwa utekelezaji wake. Licha ya kuwa wadau wengi walishirikishwa wakati wa kutunga sera hii, walimu – ambao ndio watekelezaji wakuu – wamepewa mafunzo juu juu tu.

Halmashauri nyingi ziliandaa mafunzo ya siku mbili kwa Walimu wanaofundisha Kidato cha Kwanza ili kuwapa A, B, C za kile wanachopaswa kutekeleza, cha kushangaza, mafunzo hayo yaliyotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yalikuwa ya rasha rasha tu, ambayo hayamfanyi Mwalimu kuwa mbobezi katika utekelezaji wa sera hii mpya.

Fikiria shule zimefunguliwa na wanafunzi wameshaanza kusoma, lakini walimu ndio wanapewa semina kuhusu utekelezaji wa sera hiyo, semina zenyewe zilikuwa za zimamoto, ilimradi tu ionekane wadau wamepewa mafunzo.

Mbaya zaidi, semina hizo zilitolewa kwa walimu wanaofundisha Kidato cha Kwanza tu. Walimu wengine hawakuhusishwa, hivyo hawana chochote wanachojua kuhusu sera hiyo na utekelezaji wake.

Pili, sera imetungwa na Wizara ya Elimu, lakini mtekelezaji mkuu ni OR-TAMISEMI. Hofu yangu ni usimamizi wa utekelezaji wake, kwani baadhi ya wasimamizi wa TAMISEMI wana mwelekeo wa kisiasa zaidi kuliko kitaalamu.

Tatu, kuna changamoto za rasilimali. Kwa mfano, imeanzishwa somo jipya la Business Studies, lakini asilimia kubwa ya shule za kata hazina Walimu wa masomo ya biashara. Je, hili walilifikiria kabla, au watatoa ajira kwa walimu mwaka huu?

Vitabu vya kujifunzia na kufundishia navyo, japo vinaletwa, bado havitoshi na vingine havipo kabisa. Walimu wanaambiwa waende ku-download vitabu hivyo mtandaoni.

Mfano, somo la Historia ya Tanzania na Maadili halina vitabu, na hakuna mwalimu aliyeandaliwa rasmi kufundisha somo hilo. Walimu wa Civics (ambalo limefutwa) ndio wameambiwa wafundishe. Hii inaonesha maandalizi hayakuwa mazuri.

Mwisho, napenda kuhitimisha kwa kusema kuwa sera hii ilijikita zaidi kushirikisha wadau katika kutoa maoni lakini ikasahau wadau wakuu wa kutekeleza sera mashuleni.

Kwa uelewa wangu, najua kuwa mwalimu ili awe mahiri na mbobezi anapaswa kuandaliwa vizuri katika somo husika. Sasa swali langu ni, walimu wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili wameandaliwa lini na wapi? Au tumechukulia tu kuwa watakuwa competent hata kama hawajawahi kusoma somo hilo?
 
Mkuu kwa mtizamo wako upo sahihi ila mimi maoni yangu ni kwamba mabadiliko ya mtaala ilikuwa ni lazima kwa mfumo wetu kwa maana hakuna ukuaji bila mabadiliko.

Lakini swala la mzazi asijue swala la mabadiliko mpaka leo. Hii huyo mzazi hajui maana ya elimu maana elimu ni kujinyima, kujitoa na kushindana. Sasa kama mzazi hajui sikupingi maana ili elimu iwe na thamani ni lazima kuwe na wazazi goigoi na wazembe.. Kwa hiyo wakati ni sasa... Asiyejua maana haambiwi maana..
 
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Utawala Bora (OR-TAMISEMI), imeanza utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 kwa Shule za Sekondari kuanzia Januari 2025.

Kwenye makaratasi, sera hii ni nzuri kwani imelenga kukuza vipaji na vipawa vya Wanafunzi, pamoja na kuongeza elimu ya amali kwa watoto wetu ili waweze kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii yetu.

Licha ya mazuri ya sera hii chini ya Wizara ya Elimu, nimegundua kuwa utekelezaji wake utakuwa mgumu sana kwa miaka ya mwanzoni kwa sababu zifuatazo:

Mosi, sera hii haikuwashirikisha wadau wakuu wa elimu ambao ni watekelezaji wakuu – Walimu na Wazazi.

(a) Wazazi:
Wengi hawajui kama kuna Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 ambayo imeanza kutekelezwa Januari hii (2025) kwenye shule zetu. Hawajui kuwa kuna mabadiliko makubwa yamefanyika, ikiwemo wanafunzi kuanza kuchagua masomo kuanzia kidato cha kwanza, tofauti na zamani ambapo masomo yalichaguliwa kidato cha tatu.

Hofu yangu ni kwamba watoto (wanafunzi) watachagua masomo bila wazazi kujua, maana hawana taarifa za yanayoendelea mashuleni. Kama mzazi ana mpango wa mwanae kusoma mchepuo wa sayansi, anaweza kushangazwa akifika kidato cha tatu kugundua mtoto alishachagua masomo ya biashara, ufundi, au sanaa tangu kidato cha kwanza. Hali hii inaweza kuleta sintofahamu kati ya wazazi, walimu na wanafunzi.

(b) Walimu:
Hawa ndio watekelezaji wakuu wa sera hii shuleni, lakini bahati mbaya hawajaandaliwa ipasavyo kwa utekelezaji wake. Licha ya kuwa wadau wengi walishirikishwa wakati wa kutunga sera hii, walimu – ambao ndio watekelezaji wakuu – wamepewa mafunzo juu juu tu.

Halmashauri nyingi ziliandaa mafunzo ya siku mbili kwa Walimu wanaofundisha Kidato cha Kwanza ili kuwapa A, B, C za kile wanachopaswa kutekeleza, cha kushangaza, mafunzo hayo yaliyotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yalikuwa ya rasha rasha tu, ambayo hayamfanyi Mwalimu kuwa mbobezi katika utekelezaji wa sera hii mpya.

Fikiria shule zimefunguliwa na wanafunzi wameshaanza kusoma, lakini walimu ndio wanapewa semina kuhusu utekelezaji wa sera hiyo, semina zenyewe zilikuwa za zimamoto, ilimradi tu ionekane wadau wamepewa mafunzo.

Mbaya zaidi, semina hizo zilitolewa kwa walimu wanaofundisha Kidato cha Kwanza tu. Walimu wengine hawakuhusishwa, hivyo hawana chochote wanachojua kuhusu sera hiyo na utekelezaji wake.

Pili, sera imetungwa na Wizara ya Elimu, lakini mtekelezaji mkuu ni OR-TAMISEMI. Hofu yangu ni usimamizi wa utekelezaji wake, kwani baadhi ya wasimamizi wa TAMISEMI wana mwelekeo wa kisiasa zaidi kuliko kitaalamu.

Tatu, kuna changamoto za rasilimali. Kwa mfano, imeanzishwa somo jipya la Business Studies, lakini asilimia kubwa ya shule za kata hazina Walimu wa masomo ya biashara. Je, hili walilifikiria kabla, au watatoa ajira kwa walimu mwaka huu?

Vitabu vya kujifunzia na kufundishia navyo, japo vinaletwa, bado havitoshi na vingine havipo kabisa. Walimu wanaambiwa waende ku-download vitabu hivyo mtandaoni.

Mfano, somo la Historia ya Tanzania na Maadili halina vitabu, na hakuna mwalimu aliyeandaliwa rasmi kufundisha somo hilo. Walimu wa Civics (ambalo limefutwa) ndio wameambiwa wafundishe. Hii inaonesha maandalizi hayakuwa mazuri.

Mwisho, napenda kuhitimisha kwa kusema kuwa sera hii ilijikita zaidi kushirikisha wadau katika kutoa maoni lakini ikasahau wadau wakuu wa kutekeleza sera mashuleni.

Kwa uelewa wangu, najua kuwa mwalimu ili awe mahiri na mbobezi anapaswa kuandaliwa vizuri katika somo husika. Sasa swali langu ni, walimu wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili wameandaliwa lini na wapi? Au tumechukulia tu kuwa watakuwa competent hata kama hawajawahi kusoma somo hilo?
Upo deep, nimependa uchambuzi wako
 
Back
Top Bottom