Sera ya Elimu ya JK 2014 ingesaidia kuimarisha ajira za uhakika, kwanini wapinzani waliibeza na Uongozi huu ikaitupilia mbali kabisa?

Sera ya Elimu ya JK 2014 ingesaidia kuimarisha ajira za uhakika, kwanini wapinzani waliibeza na Uongozi huu ikaitupilia mbali kabisa?

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Kifupi kabisa ni sera iliyolenga kila Mtanzania anapomaliza elimu awe na ujuzi mahususi utakaosaidia kujiajiri na kujenga Taifa.

  1. Sera hiyo ilikusudia kila mwanafunzi amalize kidato cha nne na kisha ajiunge ama na chuo cha ufundi au ustadi kitakachokuwepo kila Kata ili apate mafunzo ya kumsaidia kuchapa kazi.

  2. Kwa sasa bado Tanzania watu wanaojiajiri stadi na ujuzi wameupata kupitia kurithi stadi hizo kwa wazazi wao au kwa watu wenye ujuzi huo waliopo mtaani tu na elimu rasmi imeshindwa kabisa kuzalisha wataalam rasmi. Siruhusiwi kuandikiwa takwimu lakini takribani asilimia 95 ya mafundi stadi wanaojenga Taifa hili hawajasoma elimu rasmi ya stadi husika na hili ni pengo kubwa. Sio seremala, uashi, uchomeleaji, cherehani na hata udarizi na ufinyanzi.

  3. Sera ilipunguza umri wa madarasa ya kusoma kutoka 7 hadi sita kwa elimu ya msingi. Iliruhusu kurusha wanafunzi wenye uwezo mkubwa madarasa. Hivyo ingesaidia watu kuweza kujiajiri wakiwa katika umri mzuri kufanya kazi kuliko kuwa chuoni au darasani anasoma.

  4. Kama wigo wa elimu ya sekondari ungegusa wanafunzi wengi na hivyo vyuo kila kata ajira nyingi zingezalishwa kukidhi mabadiliko hayo ya mitaala. Walimu wengi wangeajiriwa kukidhi mahitaji yatokanayo na idadi ya wanafunzi ambao wangejiunga sekondari. Miradi ya kuongeza madarasa sekondari na ujenzi wa vyuo ingezaa ajira katika sekta ya ujenzi.

  5. Mradi ungejaza mapesa mtaani kwani ulikuwa umeshaandika write-up na wahisani walijitolea kujenga madarasa, kusomesha walimu kama wale waliofukuzwa UDOM na uchapishaji wa vitabu.
Hata kama ulikuwa na mapungufu lakini kwanini wapinzani waliibeza kila kitu chake?

Je, kwanini CCM ambao waliipisha sera hii kwa mbwembwe, kelele, vifijo na nderemo wameshindwa kabisa kuiimplement na kuwaacha watu na elimu ya makarasi tu kwa asilimia kubwa na wachache tu wanaopenya tundu la sindano ndio wanaofikia ujuzi wa kuweza kujiajiri au kuajiriwa.

Tunategemea elimu imsaidie kila mtu kupata ujuzi wa kufanya kazi na stadi kulingana na uwezo wake wa akili na sio kuwaandaa watu wenye akili za juu tu.
 
Haya sielewi ni kwa nini mambo muhimu kama hili kwa vyama vyetu sio kipaumbele badala yake wanakazania vitu vinavyoonekana na sio misingi ya kufanya vitu vionekane.
 
Back
Top Bottom