Cha Msingi ni kujadili dhana ya federalism, ni aina gani ya ufiderali kwa muundo upi hilo ndio suala ambalo nimesema hapa ni la kikatiba.
Kwamba bila sera ya majimbo CHADEMA haitaweza kuongoza dola, hilo si kweli. Kumbuka kubadili mfumo wa utawala ni suala moja tu katika sera na za CHADEMA na hata katika ilani yake.
Kwa hiyo, hata bila ya mfumo wa majimbo CHADEMA itatekeleza ajenda zake za kisiasa ambazo zinakusudiwa katika kuleta mabadiliko katika taifa letu mathalani rejea
http://www.chadema.net/maoni/ilani.php
Ila tunasisitiza kwamba mabadiliko ya kimfumo na kitaasisi kupitia katiba mpya, yatawezesha mabadiliko kufanyika kwa haraka na urahisi zaidi.
Kupitia misingi hii muhimu ambayo nakumbuka niliwahi kuichambua kidogo miaka kadhaa nyuma kupitia makala yangu haya:
http://www.chadema.net/makala/mnyika/mnyika_18.html
Kilichowasilishwa Mwanza ni rasimu sifuri ya mawazo ya Timu maalum iliyofanya uchambuzi. Chama kama taasisi kinaendelea kuchukua maoni ya watu mbalimbali. Kwa hiyo endelea kutoa maoni yako tu. Siku chama kitakapofanya uzinduzi wa sera hii inayofanyiwa marejeo, mara baada ya kupitishwa na vikao vya kikatiba. Unaweza kutupima vizuri zaidi.
JJ