Sera ya Muingereza juu ya Zanzibar

Sera ya Muingereza juu ya Zanzibar

doriani

Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
42
Reaction score
38
Sera hiyo ililenga kuvipatia Uhuru wa bandia na kuvitenga moja kwa moja na mwambao wa Kenya (Mombasa) na kuiviunganisha na Tanganyika. Lengo la Sera hii ya Uingereza ni kupunguza nguvu ya Waislamu wa Zanzibar na wa mwambao wa Kenya kwa kuweka kizuwizi baina yao na kuondoa fungamano la kimaumbile, vilevile kupunguza nguvu ya Kenya kwa kuipunguzia idadi ya Waislamu. Waingereza walitaka mustakbal wa Zanzibar usiwe mikononi mwa Waislamu moja kwa moja, jambo ambalo Uingereza ililiona linaweza kuwa tatizo katika maslahi yake siku za mbele. Na mwisho kwa kuwa asili ya maeneo yote ya mwambao wa Afrika Mashariki yalikuwa ni maeneo ya Waislamu na kutokana na asili ya dini yao yamekuwa chachu kubwa ya Ustaarabu, maendeleo na mapambano dhidi Ukoloni.

Uingereza ilibidi iyatazame kwa jicho la udhibiti na la umakini ili maeneo haya yasije ya kaathiri maslahi yao katika Bara. Suala hili la kudhibiti mwambao hususan visiwa vya Zanzibar ( Unguja na Pemba) ni suala ambalo Madola yote makubwa yalikuwa na mtazamo sawa. Kama kiongozi wa Ujerumani Bismark alivyowahi
kusema katika Bunge lao Ruchstag katika mwaka 1889.
"Mwambao una umuhimu mkubwa kwetu, jitihada yetu katika Bara haitokua na faida yoyote kama hatukudhibiti eneo la Mwambao".
Marekani kupitia kwa Waziri wake wa mambo ya Nje Dean Rusk nae alisema: "Zanzibar japo kwamba ni kisiwa kidogo ni muhimu kwetu kisiasa kwa sababu ya ukaribu wake na Tanganyika na Kenya".
Sera ya kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika ilikuwa ni miongoni mwa ajenda ya Uingereza.

Amma Msukumo wa baadae wa Marekani kutaka kufanikisha ajenda hii kwa haraka kutokana na khofu yake katika kipindi cha vita baridi kwamba chama cha kikoministi cha Zanzibar (Umma Party) kingeweza kuja kuigeuza Zanzibar kuwa Cuba ya Afrika Mashariki, ilikuwa chachu nyongeza, kwani asili eneo hili palikuwa ngome ya Uingereza ikiwa ni dola yenye kushikilia mfumo na ambayo bila ya shaka ilikua na malengo katika eneo hili kwa hivyo, mawasiliano baina ya Frank Calucci aliekua Balozi mdogo wa Marekani katika Zanzibar kuitaka Uingereza kuharakisha Muungano sio kitu pekee kilichosukuma Uingereza kuja na ajenda hio, bali jambo hili lilikua ni Sera ya Uingereza ya asili na malengo yake ni kuwa mustakbal wa visiwa hivi vya Zanzibar. Kama alivyowahi kubainisha hayo mapema afisa wa Uingereza ambae baadae alikuja kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. James Callaghan kumueleza aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zanzibar baada ya Uhuru wa bendera Bw. Ali Muhsin Baruani kwa kumwambia :-
"Zanzibar msitarajie hata mara moja kuwa Dola huru, mustakbal wake upo katika kuanganishwa na Tanganyika".

Kufikia lengo hili Uingereza ilibidi kuja na mikakati miwili mikubwa. Kwanza iunde chama kitakachoweza siku za mbele kuifanikisha agenda hii, kwa hivyo awali aliilenga jumuiya ya African Association na kuitumia kama jukwaa la kuchochea hisia za kibaguzi baina ya wafuasi wake ambao wengi wao walikuwa ni wenye asili ya Bara dhidi ya watu wa Zanzibar wenye asili za kiarabu.

Hata hivyo Waingereza walitanabahi kwamba kwa kupitia Jumuiya ya African Association peke yake haitaweza kufanikisha lengo lake hili bila ya kuwashirikisha na wazawa wenye asili ya Ushirazi walioko Zanzibar. Waingereza wakamtumia Julius Kambarage Nyerere kuifanya kazi hiyo.

Tarehe 1February 1957 siku ya Ijumaa Nyerere aliwasili Zanzibar akiwa na Bw. Zuberi Mtemvu pamoja na bibi Maida Springer ambae ni Mmarekani, walikuwa wageni wa African Association. Usiku wa saa 3 mtaa wa Kisima majongoo watu wengi walifika hapo, na hapo ndipo Nyerere aliposimama na kuwashukuru watu pamoja na kuwaaga. Mwalimu alitowa hatuba ifwatayo na kusema:

"Sisi ni watu wawili tunataka kufyeka pori na pori hilo sharti tuwe na panga na bei ya panga ni shilingi 3/- na sisi ni watu wawili kila mmoja ana shilingi 1/- Je ile shilingi ya 3 tutaipata wapi?. Kama sisi tunataka kufyeka mwitu huo tuwe sote mkono mmoja, tuungane, tuchange tununuwe panga, ndipo tutapoweza kuweka safi huu mwitu, huu ni wakati wakuwa pamoja. "

" Waafrika wasijiweke nyuma tena, kuna mambo mengi yanayoturejesha, hata majumba tukaayo sisi yanaonesha hali mbaya. Hao wenzetu, wa Amerika ni matajiri wa kweli, wazee wangu na ndugu zangu nawaambia tufanikiwe, mkifanikiwa nyinyi na sisi tutafanikiwa, tena hata sisi tukifuzu na nyinyi mtafuzu bila ya shaka. Tuondowe hiki kizingiti cha upotovu tuwe sote sauti moja".
Kwa hivyo ikaamuliwa kuunganisha chama cha Shirazi Association na African Association na kuundwa chama cha Afro Shirazi Party (A. S. P.).

Kama aliyoweka wazi afisa wa Kiingereza Mr. Peny aliposema: "Ofisi yangu na idara ya Utawala zisaidia kuundwa Afro Shirazi Party".

Mkakati wa Pili wa Muingereza ni namna ya kukitawalisha Chama Chake Cha A. S. P. bila ya kuonekana moja kwa moja kuna mkono wake ili kiweze kuja kutekeleza ajenda yake na kulinda maslahi yake kwa ujumla. Ilibidi chama hiki kiingie kwenye chaguzi mara kadha, huku Uingereza ikiwa na tamaa ya fisi ya ushindi, lakini kilishindwa kupata viti vya kutosha kuunda serikali.

Hapana shaka yoyote kwamba jambo hili lilidhofisha dhamira ya Muingereza na kuifanya kuwa na chaguo gumu kisiasa katika Zanzibar, japo kwamba vyama vingine ni vyama vya kisecula kama ilivyo A. S. P. lakini vilikuwa na hisia kali za kitaifa na KAMWE havitakua tayari kubeba ajenda yake ya Muungano.

Mchafuko, vurugu na mauaji ya watu wasio na hatia katika mavamizi ya tarehe 12 January, 1964 ilikuwa so zaidi ila ni Mbinu chafu za Muingereza kukifikisha madarakani kimabavu Chama Cha A. S. P.
Baada ya kuona hakuna namna nyengine zaidi ya hivyo ili kuweza kutekeleza ajenda yake ya Muungano na kulinda maslahi yake kwa ujumla.
Ikumbukwe kwamba serikali iliopinduliwa na A. S. P. hata kwa mujibu wa Uingereza yenyewe ilikuwa serikali halali kufwatia Uhuru wa bendera wa Zanzibar uliotolewa na Uingereza mwaka 1963.

Na kutokana na ukweli huo na ikitiliwa maanani kwamba Uingereza ndio iliyokuwa ikishikilia hatamu za Ulinzi na Usalama Zanzibar, Serikali hiyo ya Zanzibar iliomba msaada rasmi kwa Muingereza ili isaidiwe
Kudhibitiwa kwa vurugu lile lakini dola ya Uingereza ilikataa katakata. ( yale maneno ya upuuzi yaliokua yakisemwa na ASP kwamba Waingereza wakikipendelea chama cha Waarabu yaliishia hapo).

Hivyo ndivyo ilivyojiri na kupelekea A. S. P. kuingia madarakani na kuunda serikali na baada ya siku mia moja tu baada ya Mapinduzi katika hali ya kustaajabisha na mshangao, Zanzibar iliunganishwa na Tanganyika.

Maana hapa kuna suala la kujiuliza vipi Umoja wa Mataifa umeridhia Muungano huu wa Nchi mbili ambazo kila mmoja wao alipitia njia tofauti ya kujikombowa. Kwa kweli Tanganyika walipata Uhuru wao kwa njia ya kura. ambayo ni njia sahihi inayokubalika ndani ya UN. Zanzibar iliopinduliwa serikali halali iliochaguliwa na wananchi wake kwa njia halali na wananchi wake kwa njia ya kura na kisha kupinduliwa na kutokea umwagaji wa damu mkubwa wa wananchi wake.

Vipi Umoja wa Mataifa uliridhia Muungano wa aina hii hata bila ya kutaka kura ya maoni ya wananchi wa Zanzibar?. Haya yote yanatuthibitishia kwamba zilitumika njia chafu na kwa mashirikiano ya nchi, za Magharibi kwa kuunga mkono Mapinduzi hayo toke lini Mapinduzi yakaungwa mkono na nchi za Mashariki na nchi za, Magharibi nazo vilivile ziunge mkono?.

Muungano wa Zanzibar na Tanganyika uliasisiwa na Uingereza kwa mikono ya watawala wa wakati ule kwa lengo lenye maslahi mapana ya nchi za Magharibi tena juu ya msingi wa kibepari.

KAMWE haukuabzishwa Muungano huu kwa lengo la kuwaunganisha watu kwa dhati wala kuwatumikia kiuadilifu, kwa sababu mfumo wa kibepari unazingatia juu ya kipimo kimoja tu "Maslahi" katika hali yoyote ile, hata kama maslahi hayo yatapatikana kwa kuwagombanisha au kwa kuwadhulumu wengine, kwa hivyo hata leo ikiwa Muingereza na Marekani itahisi Muungano umekuwa tishio kwa maslahi yao basi utaweza kuuvunja mara moja.
 
Mhuuuu hii halwa ,kumbe walituandalia mauti tangu zama zile,
kweli Mkoloni si mtu
leo umasikini umetulemea na hali mbaya za maisha kwa kukosa Uwezo wa kuendesha nchi yetu.
hali inatisha sana.
 
Makande sina la kukwambia maana ndio Makande ndugu yangu. Basi ungalitowa mawazo angalau kidogo tukafaida.
 
Back
Top Bottom