Je, tunafeli wapi mpaka tunashindwa kuwa na viwanda vidogo vidogo vingi na vya kati maeneo mbalimbali ya nchi ikiwa tuna malighafi mbali mfano Chuma ili kuepuka kuagiza bidhaa za kawaida kutoka China mfano bidhaa za majumbani, spea za pikipiki, baiskeli nk. Inawezekana vipo huko mkoa uliopo, tuhabarishane.
Kwa mfano, huwa natazama mtandaoni video fupi fupi kuhusu viwanda vidogo vidogo katika nchi za Asia mfano Bangladesh, India na nchi nyingine zinazoendelea.
Viwanda hivyo vidogo vidogo kwa asilimia kubwa mikono ya binadamu inatumika kuiongoza mitambo na wala si maroboti lakini wanazalisha bidhaa ambazo wangeagiza nje ya nchi.
Pia, wakati mwingine viwanda hivyo vipo uchochoroni tu kwa zana duni lakini bidhaa zinazalishwa.
Huku kwetu TZ, tatizo ni nini? Hatuamini katika viwanda hata vidogo vidogo?
Je, sheria za kuanzisha viwanda ni ngumu sana?
Je, mashine na mitambo ya viwanda ni gharama hata za bidhaa ndogo ndogo? Au tatizo ni nini?
Utasikia tu mtu anasemwa mtaani, yule jamaa ana pesa ndefu. Watu kama hawa tuwashauri wawekeze katika viwanda vidogo vidogo ili kuzalisha ajira kwa Watanzania wenzao na siyo kujenga majumba tu na frame za kupangisha kwa kutegemea kuchuuza bidhaa za China.
Kwa kweli huko Asia wanapambana na kuamini katika viwanda. Inawezekana sisi Watanzania hatuamini katika viwanda mana tunashindwa kabisa.
Watunga sera walitizame suala la viwanda kwa jicho la tatu kwakweli. Ikiwezekana, serikali hata imuondolee kodi zote kwa miaka kadhaa mtu anayetaka kuanzisha kiwanda ili tuachane na uchumi wa fremu za kupangisha pamoja na uchuuzi wa bidhaa za China ambazo tunaweza kuzalisha humu humu.
Naambatanisha video baadhi (zipo nyingi) fupi fupi za viwanda vidogo vidogo kutoka huko Asia ambapo sisi huku TZ tunaagiza China mfano spea za pikipiki nk. Naomba usionee huruma bando lako, bali zitazame hizo video halafu tujilinganishe na sisi. Waonesheni matajiri wakanunue mitambo na watunga sera warahisishe mazingira.