Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Utaratibu huu ambao ndio kama sera ya vyuo vikuu vingi nchini kiliwemo Chuo Kikuu cha Dar -es-Salaam, sio tu umepitwa na wakati, bali pia haufai kwani unachangia vyuo kuwa na walimu ambao hawaja-practice katika field wanazofundisha na hivyo kuzalisha wasomi wenye kukosa maarifa na uzoefu kutoka kwa watu waliofanya kazi kwenye field husika.
Utaratibu huu ulifaa miaka ya nyuma ambapo wasomi walikuwa ni wachache lakini sio leo hii ambapo wasomi ni wengi wakiwemo waliofanya kazi katika field husika.
Mtu ambae amemaliza chuo na kupata first class kisha akaunganisha masters na baadae PhD ila hajafanya kazi katika field husika, sidhani kama anaweza kuwa mwalimu mzuri zaidi ya kubobea kwenye theory tu.
Pamoja na uwepo wa mafunzo kwa vitendo baada ya theory za darasani wakati wa likizo, bado kuna umuhimu mkubwa wa taaluma katika vyuo vyetu kutolewa na watu wenye sifa na moja ya sifa ya ziada ila muhimu ni walimu wawe walau wamefanya kazi katika field wanayofundisha.
Najua kwa baadhi ya field inaweza kuwa ni changamoto kupata na kuajiri wataalamu /wasomi wa kufundishia walioko katika field, ila vyuo bado vinaweza kutenga muda wa wataalamu hawa kuja kutoa mihadhara kwa utaratibu wa part- time vyuoni.
Tukikubali kutazama upya utaratibu huu na kuufanyia marekebisho kadri inavyowezekana, bila shaka tutakuwa na nafasi ya kuzalisha wasomi wazuri wanaoweza kushindana na wasomi kutoka katika mataifa mengine katika soko la ajira na hata katika kujiajiri.
Elimu yetu sehemu kubwa ni theory, na walimu wetu ambao nao ni zao la theory wanafundisha bila hata ku-practice field husika, halafu eti tunatarajia tuweze kuwa na wahitumu wenye viwango! Itawezekana kweli?
Tujitafakari.