Sera za kibiashara za DStv na media zingine zinakera

Sera za kibiashara za DStv na media zingine zinakera

CHEF

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2013
Posts
222
Reaction score
122
Kwa ukweli kuna sera zingine za kibiashara zinakera sana, mfano DStv unakuta wanataka malipo ya kifurushi cha mwezi wakati unakuta kwa mwezi mtu anapata muda wa kuangalia TV mara mbili au tatu.

Sasa kwanini kusiwe na kifurushi cha siku, wiki na mwezi kulingana na mtumiaji atahitaji kifurushi gani, ili iwe kama LUKU (lipia umeme kadri unavyotumia) au mitandao ya simu, na wenyewe wafanye hivyo basi.

Tulipie kadri tunavyotumia siyo nataka kuangalia kipindi fulani tu, unanilazimisha kulipa kifurushi cha mwezi mzima ndiyo niangalie hicho kipindi, inakuwa haileti mantiki kabisa.

Na wenye kusikia msikie ili wakikwama apatikane mshindani anaweza kufanya hivi tukimbilie huko, Azam wana hii sera lakini waipanue zaidi.
 
Nimewahi kujiuliza na kuwauliza. Sikupata jibu la kueleweka.
 
Nimewahi kujiuliza na kuwauliza. Sikupata jibu la kueleweka.
Tunatakiwa kupata ya majibu kueleweka hapa, kama watakuwa kimya itakuwa ndio mwanzo wa kuanzisha sera hii mpya ya kibiashara, tutaomba muongozo kutoka kwa wakubwa
 
Huu sio Uzi wa kisiasa peleka kule

State agent
Mkuu siasa maana yake ni sera, sasa kuna sera za kiuchumi,sera za kijamii na n.k , sasa wewe unajua siasa ni kuzungumzia vyama , watu na wanasiasa si ndio, kama unafikiria hivyo basi haupo sahihi
 
Hata Mimi nilishawahi kutamani hvyo iwe kama vocha unalipia kwa cku ingependeza sana. Mawazo mazur mkuu.
 
Kuna mwenzio ameyashtaki makampuni ya simu. Unaweza fata nyayo zake
 
Kuna mwenzio ameyashtaki makampuni ya simu. Unaweza fata nyayo zake
hapa hakuna kesi mkuu, hapa ni kuomba kubadilisha sera za malipo ya kifurushi
 
Hata Mimi nilishawahi kutamani hvyo iwe kama vocha unalipia kwa cku ingependeza sana. Mawazo mazur mkuu.
Tunaomba waje watutolee ufafanuzi juu ya hili suala
 
Huyu anaongelea Pay As You Go, yaani unalipia kile unachotaka kuangalia kwa muda huo, badala ya kulazimishwa kununua kifurshi chote cha mwezi husika. Nadhani Azam na Startimea wa vifurushi vya siku na wiki
Kuna mwenzio ameyashtaki makampuni ya simu. Unaweza fata nyayo zake
 
Back
Top Bottom