SoC02 Sera za kodi ,ushuru bandarini zinavyozorotesha maendeleo ya nchi

SoC02 Sera za kodi ,ushuru bandarini zinavyozorotesha maendeleo ya nchi

Stories of Change - 2022 Competition

iliasakhamis

Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
9
Reaction score
7
Habari wana JF

Napenda kuwashirikisha wanajamii wenzangu juu ya uchumi wa nchi ya Tanzania kudhoofika na kuendelea kukua kwa kiwango kidogo sana kwa kila mwaka ni kutokana na kuwa na sera za kikodi na ushuru ambazo zinawavunja moyo wawekezaji na wafanyabiashashara wengi kupelekea kudorora ukuaji wa kiuchumi.

Leo tuangazie eneo la Bandarini ambalo ni eneo muhimu sana kwenye ukuaji wa kiuchumi wa Taifa letu ila sera za kikodi na ushuru zimekuwa mwiba wa ukuaji uchumi wetu, kutokana na kuwa na urasimu ambao unapelekea udororaji wa kiuchumi.

Sera za kikodi ambazo sio himilivu kwa wafanyabiashara wengi ambazo zinamlenga moja kwa moja mfanyabiashara zinapelekea kuwepo na uwanja mpana wa mazungumzo ambayo yanapelekea kuwa na urasimu na viashiria vya rushwa vinavyopelekea kushusha mapato ya kodi na ushuru ambayo mfanyabiashara angepaswa kuzilipa ila kutokana na sera za kikodi na ushuru kuwa kubwa na kumpelekea mfanyabiashara kutafuta unafuu wa kodi kwa meza ya mazungumzo.

Nini kifanyike?
1) Serikali na sekta zinazosimamia kodi zikae pamoja kujadiliana na wafanyabiashara ili kuondoa urasimu katika sekta hiyo ili kuweza kuingizana kutoa mizigo mengi na kutoka kwa wakati ili kuwawezesha wafanyabiashara wengi zaidi kuweza kuagiza mizigo mengi zaidi na kukuza uchumi kwa kupittia kwa walipa kodi wengi zaidi

2) Serikali kuingia kwenye mpango wa ushindani wa kibiashara wa kikanda wa nchi zinazotumia bandari ili kuongeza wigo wa kuingiza na kutoa mizigo mengi na kwa wakati ili kupunguza urasimu unaweza kupelekea ucheleweshaji wa mizigo katika bandari na bandari kavu kwani soko la ushindani litawawezesha kushindana kibiashara

3) Kuwajibishwa kwa viongozi wanaopelekea udhoofishaji wa maendeleo ya bandari na kiuchumi wanaendeleza urasimu na kula rushwa katika sekta ya bandari

4) Kupunguza kodi na ushuru ili kuwawezesha wafanyabiasha wengi zaidi kuweza kuingiza na kutoa mizigo kupitia bandari zetu ili kuwavutia wafanyabiashara wa nje ya nchi kwa nchi ambazo hazina ukanda wa bandari ili kuongeza mapato kwa nchi yetu

5) Uboreshaji wa miundombinu ya upakiaji na utoaji mizigo bandarini kutaondoa ucheleweshaji wa mizigo ambao unapelekea urasimu na viashiria vya rushwa

Naomba kura yako kama umependa andiko langu
0656040880
 
Upvote 4
Nimekupigia kura mkuu, karibu pia katika chapisho langu "Vita ya vijana dhidi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia"
 
Katika nchi za kiafrica kodi ni moja ya tools ya kuwafanya wananchi wawe masikini Ili waweze kuwatawala
 
Kwani bandarini wamejiweka au wamewekwa na mamlaka ...kama mamlaka ya juu ndiyo wamewateua na kuwajiri huna haja ya kuhoji utendaji wao..wenye mamlaka ndiyo watapima utendaji wao..
 
Back
Top Bottom