Sera za Uwekezaji, je ni rafiki kuvutia uwekezaji toka nje?

Sera za Uwekezaji, je ni rafiki kuvutia uwekezaji toka nje?

Full 8

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
313
Reaction score
271
Serikali imekuwa ikifanya jitihada nyingi za makusudi ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuwekeza katika viwanda. Tumeshuhudia mikutano na warsha nyingi zikijadili namna ya kuwekeza na fursa zilizopo nchini.
Lengo la kuanzisha uzi huu ni kutaka kutoa nafasi kwenu kujadili suala zima la uwekezaji hasa kunusisha sera zetu na uwekezaji wenyewe.

Mfano rejea.
Nilipata wasaa wa kubadilishana mawazo na mwekezaji mmoja kutoka Ujerumani, anadai mazingira na sera zetu sio rafiki kabisa kuvutia uwekezaji kutoka nje hasa uwekezaji mkubwa. Anasema alikuja na mtaji mkubwa tu na kuwekeza katika sekta ya madini lakini Kodi, rushwa na janja janja ya waswahili vilimfanya akapoteza fedha zake nyingi. Pia, anaelezea udhaifu uliopo katika sera za uhamiaji (kibali cha makazi na kufanya kazi nchini), sera hazimpi unafuu kwa mwekezaji kuishi nchini kwani anakumbwa na tozo kubwa pale anapotaka kuongeza muda wa kukaa mara kibali cha awali kinapoisha muda wake achilia mbali kutopewa uraia kwa mgeni aliyewekeza nchini na kubahatika kuoa/kuzaa na mzawa.

Natumai michango/Hoja zenu mbalimbali zitachingia katika kuboresha sera au kuibua mjadala utakaoanzisha maboresho ya sera zetu ili kufikia malengo ya uchumi wa kati 2025.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom