Sera zisizotabilika kwenye kilimo zitaua kilimo

Sera zisizotabilika kwenye kilimo zitaua kilimo

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Kilimo kitaendelezwa na upatikanaji wa soko la uhakika.

Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania tulikuwa tumeanza kukamata masoko ya chakula katika nchi jirani kama Kenya na Kongo.

Tunasikia jinsi ambavyo kenya inahangaika na uhaba wa chakula, badala ya watanzania kuplani hawa ndugu zetu kuchukua masoko yao yote ya chakula ni ajabu eti tunabadairika na kuzuia kuuza chakula nje.

Haya mambo ya kununua chakula wenyewe na kutunza hayana tija. Serikali iache wakulima wetu wahudumie masoko ya jirani na yenyewe inunue ziada na kuhifadhi.

Cha msingi ni wizara ya kilimo kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishaji, wahamasishe matumizi ya mbolea, utaalamu n.k
 
Ni upuuzi sana ,Hawa viongozi wa ccm hawajielewi na hawaelewi wanataka nini..

Just imagine Bashe amesisitiza sana sera ya Kilimo Biashara na kwamba hakutakuwa tena na mazuri ila anakuja mtu anakutupuka from no where eti hakuna kuuza chakula Nje ya Nchi,huyo huyo wiko Moja kabla alisema mahindi na mchele yamekuwa rasmi mazao ya biashara ambayo yataingiza pesa za kigeni Kwa haraka..

Kila mtu anatoa tamko lake,na uhakika ukimuuliza Rais ajenga 10/30 anazijua sidhani maana asingetoa tamko la kienyeji kama Hilo.

Ukienda kwenye takwimu za Mabenki sekta ya Kilimo ilianza kuwa inaongoza Kwa mikopo Kwa kuwa watu walihakikoshiwa kwamba hakutakuwa na uingizaji wa kipuuzi wa Serikali..

Huu upuuzi ukomeshwe na Kwa staili hii Kijana gani ambae ataingia kwenye Kilimo? Kilimo ni vulnerable bila kuwa na sera zinazotabilika hakuna mtu ataingiza pesa yake..

Na Kilimo kitafanikiwa tuu kama Kuna uhakika wa soko na si vinginevyo
 
Nenda kajisajiri kama mkulima wa kibiashara upewe kibali cha kuuza mazao nje, mambo ya kufanya ulanguzi kutoka kwa wakulima wadogo kupeleka nje mnasababisha uhaba mkubwa wa chakula nchini.
 
Nenda kajisajiri kama mkulima wa kibiashara upewe kibali cha kuuza mazao nje, mambo ya kufanya ulanguzi kutoka kwa wakulima wadogo kupeleka nje mnasababisha uhaba mkubwa wa chakula nchini.
hizo ni fikra za watu wasiojitambua

katika jamii yetu, uholela ndiyo mipango katika kila kitu. kama tunataka kuondoa uholela tuanze kutunga kanuni taratibu na kuweka taratibu bila kuvuruga shughuli za kiuchumi.

kwa wananchi kuuza mazao nje hata bila utaratibu ni faida kwa wakulima wenyewe na taifa ila tukiwa na utaratibu tungepata faida zaidi.

siyo makosa ya wakulima au mtanzania yoyote kwamba hatuna utaratibu,

upungufu wa chakula hautokani na kutokuwa na utaratibu bali unapopanua masoko, demand inaongezeka na autoatically utapata shida kwenye upungufu na bei lakini haya hayadhibitiwi kwa kuzuia masoko bali hayo ni chachu kwa wakulima kuongeza uzalishaji.

serikali iweke utaratibu kwa kuanza kusajili vibali na pengine ndani ya miaka miwili watkuwepo wafanya biashara wenye vibali na wasiokuwa na vibali na hapo ndipo unazuia wasio na vibali.

tena unawaambia kabisa kuanzia mwaka 2026, mazao ya chakula yatauzwa na wenye vibali tu.


siyo huu upuuzi wa mtu ameshapakia mzigo yuko mpakani unamzuia kupita eti hana kibali bila taarifa yoyote.
 
Formalization ndio mpango mzima, Mhe Bashe yuko kwenye right track. Watanzania tubadilikeni.
 
Nyakati kama hizi (mwezi Mei hadi Julai) miaka minne mitano iliyopita, bei ya kilo moja.ya mahindi hapa kwetu ilikuwa sh.200/=.
Hivi sasa bei ya kilo moja ni sh.800/= hadi 1,110/=.
Hii ni faida kubwa ya moja kwa.moja kwa wakulima.

Siku hizi mbili, tatu bei imeporomoka tena.
Kazi ya mkulima haina bima.
 
Lakini sinimesikia Bashe ana sema kuwa hawajazuia kuuza nje bali yasafirishwe kwa kufuata sheria ina maana kuanzia tarehe 1/7 mipaka inafunguliwa tena kwa wafanya biashara walio kamilisha kujisajili?
 
Back
Top Bottom