Ndugu zangu wanajukwaa, kwanza nawapa pole sana kwa majukumu mengi na magumu ya kulijenga Taifa Letu, ambalo mpaka leo linaitwa Taifa changa.
Pamoja na hayo yote, tumezidi kushuhudia jinsi nchi yetu inavyokosa kuhudumia raia wake ipasavyo kwa kisingizio cha kukosa fedha. Huduma za muhimu kama maji, barabara, afya na nyinginezo hazipatikani na kama kuna juhudi basi tunaambiwa serekali imekopa kwa wahisani au tumepewa misaada na wafadhili, Rais wetu amekuwa msafiri mashuhuri akizunguka kuomba hiyo mikopo na ufadhili wa miradi ambayo, ambayo hata baada ya kuipata kuisimamia ili iwanufaishi wananchi inakuwa shida kubwa. Tumekuwa tukishhudia mkaguzi wa mahesabu ya serekali akitoa taarifa ya wizi wa mabilioni kila mwaka na hakuna hatua za kuridhisha zunazochukuliwa, wanasiasa wetu waliopo serekalini wamekuwa wakitueleza jinsi wanavyojitahidi kupunguza tatizo hilo lakini mafanikio yake kama yapo basi ni kidogo mno.
Pamoja na hayo yote, serekali yetu haikusanyi kodi kwa umakini hata kidogo, nimeshuhudia kwa macho yangu wafanya biashara wengi wakikwepa kodi kwa kisingizio cha mashine ya tra imeharibika na mara nyingine hali hiyo inakuwa hata wiki mbili, mfano nzuri ni vituo vya mafuta (petrol stations ) nyingi hazitumii mashine hizi kwa maelezo kuwa zimeharibika, pia maduka ya spare za pikipiki, na magari pale kariakoo ama hupati kabisa hizo risiti za tra na au ukipewa basi gharama ya risiti hiyo hailingani na kiasi cha pesa ulicholipa. Sehemu nyingine ni mpaka uombe risiti ndipo unaambiwa kama unahitaji ni lazima uongeze pesa. Je serekali yenye kujali raia wake haijui haya yote? Au ndyo vile mwalimu Nyerere alivyosema kuwa serekali corrupt haikusanyi kodi!!! Badala yake inawaandama wamachinga tu?
Nawasilisha.