Serekali mnalijua hili?kiliniki kwa mjamzito ni hela arusha,

Serekali mnalijua hili?kiliniki kwa mjamzito ni hela arusha,

mnyinda

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Posts
277
Reaction score
64
Tunaiomba serikali iweke wazi kwamba kumudumia mama mjamzito anapokwenda kiliniki kuwa nihela
imekuwa kawaida sasa kwa hosptali zetu kuwatoza fhedha wamama wajawazito wanapokwenda kilini,kati ya hospitali ambazo zimeweka wazi kuwa ni hela ni kaloleni levolosi ambapo kama hautakuwa na hela itakubidi kurudi
serekali imekuwa ikitangaza kuwa huduma ya mama na mtoto ni bure jambo ambalo sikweli.
 
Ni kweli hata hapa Morogoro bado tunatozwa hela kwenye hizi hospitali za serikali
 
Muda mwingine huwa naona ni bora kwenda hospitali ya binafsi ambapo nitapata huduma nzuri zaidi ya huko serikalini
 
Sasa wakikutoza si unagoma unawaletea vile vipeperushi vinavoonyesha kila kitu
 
Sasa hii inatisha kama serikali inasema ni bure alafu wao wanawatoza fedha wamama wajawazito serikali sasa inafanya nini?

BlackBerry 8900 using JamiiForums
 
serekali imekuwa ikitangaza kuwa huduma ya mama na mtoto ni bure jambo ambalo sikweli.

Huo ulikuwa usanii wa kisiasa unaofanywa na serikali ya ccm ila nadhani umejifunza.
Sasa 2015 usirudie makosa chagua CHADEMA si hilo la klinik tu hata watoto wako watasoma bure.
 
mkuu ,kama wamama wana uwezo wa kununua vitenge iweje washindwe kujigharamia huduma ya uzazi?
 
mkuu ,kama wamama wana uwezo wa kununua vitenge iweje washindwe kujigharamia huduma ya uzazi?

kamanda elewa kwamba unapo tangaza nibure unawaaribu wamama kisaikolojia nibora watangaze nihela tujue,
 
sasa wakikutoza si unagoma unawaletea vile vipeperushi vinavoonyesha kila kitu

halafu ukishagoma anayekufa ni nani kati yako wewe na huyo dactar? Au anayeumwa kati yenu ni nani? Wewe goma kutoa utakiona cha moto, mimi huwa natoa pale m/nyamala hosp na napata matibabu fasta na mazuriiiiiiiiiii! Tena ukitaka kufaidi toa buku tano, utaona utakavyohudumiwa unapata mpk dawa ambazo ukienda dirishani unaambiwa hamna ukanunue. Chezea pesa wewe!!
 
mkuu ,kama wamama wana uwezo wa kununua vitenge iweje washindwe kujigharamia huduma ya uzazi?
Labda vijijini hiyo ni kweli kabisa inakuwa ngumu sana mtu kupata pesa ya kununua kitenge, lakini hapa mjini kila siku wanacheza rusha roho, wanaenda hadi kukopa FINCA kwa ajili ya Rusha roho na kutunzana, lakini akifika pale m/nyamala Hosp hataki kutoa pesa ili ahudumiwe vizuri ndipo hapo nami nashangaa sana, wanathamini rusha roho kuliko afya zao.
 
Back
Top Bottom