Serena acquires Mövenpick Hotel in Dar es Salaam


kwa nini watz waendelee kulalamikia iko kitu cha kukwepa kodi kama mlishaifuta watangazieni kuwa ataubadilishe jengo kama sio jina kodi ipo pale pale na kwa maandishi ya kushuhudia yaani reference..
 
Reactions: EMT
Hayo ni majina ya hotel management. Jina la kampuni ni Tanruss Investment tokea zamani. Hao Sheraton, Royal Palm, n.k. ni hotel management. Kubadilisha majina ya hotel management hakuna significant tax implications.
Ni kama Airtel, kampuni ilikuwa inaitwa Celtel Tanzania Ltd tangu zain. Kwa sasa imebadilishwa jina inaitwa Airtel kwa kuwa mmiliki amebadilika.
Kuhusu kulalamika kwa watu, nadhani inatokana na kutojua ukweli. Information za kampuni zote Tanzania zinapatikana BLERA na ni public information upon request.
 
Reactions: EMT

Remember that currently the issue of building, owning, ie majority share is no longer a deal, people are currently talking on management and controlling. hakuna wizi hapo ni tubadilike tu kwenda na wakati
 

Very true ila ishu ya wafanyakazi ndo inakuwaga na mawenge sana pamoja na tax holidays wanazopewa wawekezaji wapya.
 
Wajinga ndio waliwao!
Tanzanians are loosing millions of taxes through this process. All of us know, but.......
What else can you say? Sahmba la bibi, a country where, everyone can do and play whatever he/she likes!
Mungu ibariki Tanzania.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]
Kampuni ya Serena yanunua Mövenpick
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 24 November 2011 20:19 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Na Mwandishi Wetu
Kampuni inayojishughulisha na Huduma za Hoteli na Utalii Afrika Mashariki (Tourism Promotion Services (TPS) ambayo pia inamiliki hoteli za Serena imenunua hoteli ya Mövenpick Royal Palm ya jijni Dar es Salaam.

Kutokana na kununuliwa hoteli hiyo na TPS sasa itabadilishwa jina na kuwa Dar es salaam Serena Hotel kuanzia mwanzoni mwa mwezi ujao. Mövenpick Royal Palm Hotel ni hoteli yenye vyumba 230 na hadhi ya nyota tano.

TPS (D) Limited ndiyo kampuni ya ununuzi inayomilikiwa na Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED), TPS Eastern Africa Limited (TPSEAL), PDM (Holdings) Limited, PROPARCO and NORFUND .

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSEAL, Mahmud Jan Mohamed katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema kufunguliwa kwa hoteli za Serena jijini Dar es Salaa ni utekelezaji wa mpango wa muda mrefu wa kufungua hoteli katika miji mikuu Afrika Mashariki, yaani "City Hotel Circuit"

Alisema kutokana na kuwapo kwa hoteli tanzu za Serena, hoteli hii itafaidika na mtandao ulioenea Tanzania, Zanzibar, Kenya, Msumbiji, Rwanda na Uganda.

" Lengo letu ni kupanua wigo wetu nchini na maeneo mengine. Hotel za Serena zinalenga kufikisha huduma bora kwa wateja wake, kutoa fursa za kazi za kuvutia kwa wafanyakazi wake," alisema

Kwa sasa hoteli za Serena zina waajiriwa 3,400 kwa Afrika Mashariki.Jan Mohamed alisema Serena Hotels imepanuka kutoka vituo vinne mwanzoni mwa miaka ya 1970 hadi kufikia hoteli za kifahari za aina tofauti 25 zinazotoa huduma za kitalii katika nchi sita za Afrika.

Alisema mbali na uwekezaji katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, pia TPS ina vitega uchumi vitega uchumi 10 katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Tajikistan.

Serena Hotels zilianzishwa Tanzania mnamo mwaka 1996 zikianza na vituo 5 na kupanuka hadi
10 uwekezaji ukiwa Arusha, Ukanda wa Kaskazini wa Utalii, Ukanda wa Kusini wa Utalii na sasa Dar es salaam.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

jamani naangalia hii trend ya hoteli hii kubadilishwa "wamiliki" wa hoteli hii, leo kwenye mwananchi nasikia imekwenda sasa hivi kwa serena hotels!!!! soma mwenyewe...... source gazeti la mwanachi
 
Mkuu mambo ya corporate tax hayo na sheria zetu 'malaya' za uchumi!
 
Thu Nov 24, 2011 6:53am GMT

* Dar es Salaam Serena has 230 rooms
* Value of transaction not disclosed

NAIROBI Nov 24 (Reuters) - Kenya's TPS Eastern Africa , operator of the Serena Hotels chain, has bought a five-star hotel in the Tanzanian capital Dar es Salaam, giving the chain a presence in one of the region's fastest-growing economies.
TPS said it had acquired the 230-room, five-star Royal Palm Hotel from Movenpick Hotels and Resorts, without disclosing the value of the transaction.

The hotel will be renamed the Dar es Salaam Serena Hotel from next month, TPS said in a statement late on Wednesday.
"The hotel will be positioned as the premier up-market five-star hotel for the discerning corporate and leisure clientele," the company said.

TPS operates in Kenya, Zanzibar, Mozambique, Rwanda and Uganda. It also has a small presence in northern Tanzania.
Serena Hotels has expanded from four units in the early 1970s to a collection of 25 luxury hotels, resorts, camps and safari lodges catering to the leisure and business markets.

Its main shareholder is the Aga Khan Fund for Economic Development, an international development agency. (Reporting by Duncan Miriri; Editing by Barry Malone and Will Waterman)



 
Kempinsi - waarabu wa Mafuta wametukimbia - Agha Kan - Serena anatuchukulia hio hoteli yetu

Kumbuka Kempinsi wana Hotel CHAD na ni kwanini wameondoka TZ; from Zanzibar, Arusha na Dar?

Ningewapendelea Kempinsi zaidi sababu nikitimbelea Arabuni na Far East Mahoteli yao ni Mazuri na huduma Safi

Hii ni kwasababu tuliwasema na Suit walizompa Rais wetu Mpendwa?
 
Mkuu hapa inaongelewa Movenpick sio Kempenski.
 
Mkuu, si fice years exemption. Ilikuwa ni five year tax holiday. Ni vitu viwili tofauti. Hiyo sheria ya five years tax holiday ilishareebishwa na hicho kipengele kilishaondolewa wakati masuala ya tax exemption yana taratibu zake


Wakuu mnaweza kutufafanulia zaidi? Ninachoelewa ni kwamba Tax holidays iliyoondolewa kwa wawekezaji kwenye sekta ya mabenki mwaka 2000. Kabla ya hapo serikali ilikuwa tayari imeshapunguza muda wa tax holidays kwa mabenki kutoka miaka mitano hadi miwili baada ya kulazimishwa na IMF and wafadhili kufanya hivyo. Huko kwingine, ni sheria ipi iliyoondoa ay kufanya mabadiliko?

Inawezekana tax holidays zimeondoshwa lakini tax incentives ndio bado zipo. Kama sivyo, ni kwa nini tunapoteza mapato mengi hivyo kama zimeondolewa? kwa mfano mwaka wa fedha 2009/10, tax exemptions zilikuwa jumla ya Tsh 695 billion ($464 million). Hii ni zaidi ya nusu ya Tsh 1.3 trillion ($867 billion) serikali ilipanga kukopa kwenye commercial banks kwa ajili ya kugharamia infrastructure kwa mwaka wa fedha 2010/11.

Nashindwa kuelewa kama mambo yalishakuwa sorted tokea 2000, inakuwaje tax exemptions zinaongezeka kwa speed kila mwaka tena kupita nchi nyingine za Afrika Mashariki? Kwa mfano, tax exemptions ziliongezeka mara mbili ndani ya mwaka mmoja kuanzia Tsh 459 billion ($306 million) mwaka 2004/05 hadi kufikia Tsh772 billion ($515 million) mwaka 2005/06. Mwaka 2008/9, tax exemptions zilikuwa 2.8% ya GDP na mwaka 2009/10, 2.3% ya GDP. Mwaka 2008/09 and 2009/10, serikali ilishindwa kufikia target ya iliyojiwekea ya ukusanyaji mapato kwa Tsh453 billion ($302 million) kwa wastani. Kipindi hichi hicho, tax exemptions zilikuwa Tsh 724 billion ($483 million) kwa mwaka.

Kwa vile mnasema masuala ya tax exemptions yana taratibu zake, mnaweza kutufafanulia hizo taratibu? Kwa sababu pamoja na mabadiliko hayo yote mliyoyataja, haiwezekani, tax exemption ziendelee kuwa kubwa hivyo.
 
Yale yale ya samaki wa Fukushima, watanzania tuamke rasilimali za nchi yetu zinachakachuliwa hivi hivi mchana kweupeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!
Cheki huu mchakachuo utatamani kuwa rebel:

Mheshimiwa Spika,

Kwenye sekta ya Viwanda, Kampuni ya Bia Tanzania ambayo inamilikiwa na SABMILLER nayo pia imeripotiwa kutumia njia ya kimkakati kukwepa kodi ikiwemo kusajili hatimiliki na hivyo kupata mrahaba ambao hautozwi kodi , mfano ni kwenye pombe aina ya CHIBUKU ambapo jina hilo limesajiliwa huko Netherlands na kampuni tanzu ya TBL.

MHE.KABWE ZUBERI ZITTO (MB) August 2011

Mpaka hatimiliki za pombe za mataputapu zinasajiliwa Netherlands kukwepa kodi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…