Serengeti Boys kuna Mzanzibar hata mmoja?

talentbrain

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Posts
1,187
Reaction score
760
Habari wadau wa soka hasa mnaoumizwa na matokeo ya kikosi chetu cha serengeti boys katika kashindano yanayoendelea sasa.
nitangaze interest yangu kwanza. Mimi ni mtu wa Bara kwa kuzaliwa na kukulia ila kwa sasa nipo zanzibar kiutafutaji tu. Sasa tuko kibanda umiza hapa tunaangalia match inayoendelea ambapo mjadala umezuka kuwa kikosi ni kibovu kwakuwa hakuna mzanzibar hata mmoja aliye kwenye kikosi hiki na kwamba sio timu ya taifa hii bali ya Tanganyika.

Naomba kujuzwa maana limeongelewa hili tangu match ya kwanza tuliyofungwa 5:4. Wazanzibar wamechachamaa hapa natetea ila wameng'ang'ana. kuna ukweli katika hili?? kwamba kwenye youth system ya mpira wa zanzibar hakupatikana hata kijana mmoja mwenyekiwango cha kujumuishwa??

nawasilisha....
 
Tatizo wanacheza sana show game,..wenzao wakipata mpira wanawaza kushambulia,..lakini hawa watoto wanacheza upuuzi tu
 
Jecha alipaswa kuwa mlezi wa hii timu!
 
Tanzania bado ina nafasi ya kusonga mbele
1. Tanzania akimfunga angola , na Nigeria akimfunga Uganda basi Tanzania itasonga kwa idadi kubwa ya magoli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…