Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Upo msemo unasema "a viper strikes while you feel safe and secure" yaani nyoka huyo mwenye sumu kali anakugonga ukiwa unajihisi uko salama,timu ya Vipers itaikaribisha timu ya Simba nchini Uganda,uimara wa timu ya Vipers unafananishwa na kizazi cha akina Majid Musisi,Kamaza Batambuze, George Semogerere,Kamaza ni baba wa Shafiq Batambuze lakini Majid Musisi ndiye aliyekuwa na upinzani mkali na Jamhuri Kiwelu,ni bahati mbaya hatuna uwekezaji wa kudumu ndiyo maana simba ya mwaka juzi haiwezi kurudi tena lakini leo nitakukumbusha kidogo Simba ile iliyofikaga fainali na Stella Artouis ya Ivory Coast.
Niwakumbushe mchezaji mmoja wa kimataifa wa Simba aliitwa William Fanibula uchezaji wa William Fanibula ulinifanya nikubali, class is permanent but form is temporary,timu zetu ni average hua tunapata hype ya muda sasa hua tunajisahau na kujiona tupo class moja na kina ahly, Zamalek, Mamelodi, WAC,T.P Mazembe,Vita nk wachezaji wetu ni average grade C ndio maana wakienda nje wakikutana na grade A na B hua wanafeli vibaya
Mwaka 1997 katika mchezo wa kufuzu Afcon , Tanzania vs Liberia, wakati Taifa Stars ikiweka kambi jeshi la wokovu,George Weah akija na Private Jet toka Ac Milan,alikuwa ndio nyota zaidi anakuja akiwa ameshatwaa Balon D'or hiyo wanayotwaa Ronaldo na Messi ambayo kwa Afrika ni yeye tu kaishika,Kocha Charles Boniface Mkwasa Master,anaamua kuita viungo watupu na washambualiaji na makipa,
Kocha wa Liberia anasema wanakuja tisa tu mchezaji wa kumi anakuja na ndege binafsi toka Italy na mchezaji wa kumi na moja watamkuta Tanzania yupo klabu ya Simba anaitwa William Fanibula, Siku ya mchezo mkwasa anapanga washanbuliaji na viungo tupu kasoro beki mmoja katili alikuwa anacheza Prison anaitwa Gerald Hillu na anapewa shavu la kulia ambapo kushoto aliupiga Alfonce Modest center beki anacheza Hussein Masha na George Magere Masatu katikati anawapanga Sekilojo Chambua na Steven Mussa namba tisa anampanga Said Mwamba Kizota wakati golini Tanzania one yupo Mohamed Mwameja.
Nikukumbushe tu ndugu msomaji George Masatu aliapa kumdhibiti vilivyo mchezaji hatari kabisa Afrika na duniani ndugu George Opong Weah,wakati huo George Wear alikua akichezea klabu bingwa ya Italy na Klbu bingwa ya Ulaya na klabu bingwa ya dunia kwa mwaka 1997, AC Milan.
George Weah alipomuona George Masatu akadharau akaamua kucheza namba tano dakika ya 18 William Fanibula akatufunga goli maridadi sana mtangazaji alikuwa ndugu Ahmed Jongo akasema ni yule yule anaekula chakula chetu anatumia viwanja vyetu tunamlea sisi wenyewe na mke tumempa anatuweka kambani 😀mpira raha sana lakini kipindi cha pili "Master" Kocha Charles Boniface Mkwasa anaongea na wachezaji wake wanarudi uwanjani na dakika ya 77 Said Mwamba Kizota akawainua Watanzania akasawazisha bao ambalo linamfanya George weah aende kucheza nafasi yake ya asili namba tisa baada ya kuona hali tete lakini Sekilojo Chambua na George Masatu walijitoa kumkabili anamkaba kihuni kisela kimjini mpaka mwisho matokeo yanakuwa Moja Moja,hapo katika list namba kumi alicheza Yusuph Macho Musso,mwisho wa mechi George Wear aliitoa dola mia tano akampa George Masatu kwa kuweza kumtuliza dakika 90.
-Simba ya Mwaka 2007
Nikusimulie Simba ya mwaka 2007 ya akina Haruna Moshi Boban,mchezo kati ya Simba na Ashanti katika dimba la Jamhuri, Mkoani Morogoro ulimalizika kwa kosa la askari ambae alifyatua bomu la machozi alipotishwa na mashabiki wa Simba hiyo ilikuwa ligi ndogo ya TFF, mashabiki walikuwa wakimlaumu mwamuzi Gilbert Mande kutoka Pwani wakimshumtumu anawabeba watoto wa Jiji timu ya Ashanti United, wakati huo kocha wa Simba Nelsen Elias aliyekuwa na cv kubwa zaidi ya Robertson mwenye hadhi ya Ferguson na Arsene Wenger alikuwa anafundisha timu kwa simu akiwa jijini Dar es Salaam wakati timu inacheza mjini Morogoro wakati huo uwanja wa uhuru umefungwa Kwa matengenezo,dakika ya ya 28 Gaudensi Mwaikimba anamchungulia kaseja anawaandikia bao Ashanti watoto wa jiji lakini dakika mbili baadae Haruna Moshi Boban anasawazisha, sasa wakati mpira unaanzishwa mashabiki wa Simba wakawa wanamtisha askari mmoja alikuwa amesimama katika uzio wa jukwaa akafyatua bomu la machozi ikawa tafarani katika dimba la Jamhuri mpira ukaishia hapo na TFF wakapanga marejeano Simba akashinda,huyo askari aliyefyatua bomu aliacha kazi mwenyewe na sasa hivi ni mwalimu yupo halamshauri ya mji Geita,
Nimalizie na salute kwa watangazaji wa zamani Ezekiel Malongo, Charles Hillary, Ahmed Jongo, Dominic Chilambo, Abithai Steven na Halima Mchuka ambae mbadala wake mpaka Leo haujapatikana, George Weah kwa sasa ni Rais wa nchi ya Liberia, naamini atakuwa kampa shavu William Fanibula, nimalizie kwa kuirudia mechi ya Simba na Raja Casablanca nimegundua raja wana experience halafu wanajua,walicheza kwao bila mashabiki na bado wakampiga Vipers 5.
Hapa taifa hii atmosphere ya leo ya mashabiki wa Simba haiwatoi mchezoni, ukiwatizama wakiwa na mpira hawana papara na hata attempts zao ni za hatari, hawapotezi mipira,wana accuracy kubwa, Simba imepata somo sasa tunasubiri ushindi kwa kumpiga yule nyoka vipers ya nchini Uganda.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management
Recent Publications;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.