Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
"Serengeti shall never die" Huo ni usemi wa enzi na enzi ukitumiwa hasa na watafiti wa hifadhi za mazingira na wanyama waliotumia muda mwingikufanya tafiti mbali mbali za wanyama na mazingira yao.
Leo wakati namaliza ziara au ukipenda utalii niliotumia siku kadhaa naweka kambi kwa muda Seronera natafakari niliyojionea Serengeti najikuta naukumbuka ule usemi maarufu "SERENGETI SHALL NEVER DIE".
Natama waliotujia na usemi huo wafufuke wajionee wenye Serengeti inayofanyiwa vitimbi vyote vya kuuwawa tena maksudi kabisa.
Barabara ni mbaya kupitiliza hali ya usafi katika sehemu za kujisiri ni mbaya hata toilet paper hakuna na usafi ni duni nikajaribu kuuliza kulikoni naambiwa hakuna fedha !!!!!!!.Yaani Hifadhi inayoingiza mabilion ya USD hawana fedha ????????.
Nauliza fedha zote zimeenda wapi naambiwa siku hizi fedha zooooote zina kwenda hazina kwa yule Bingwa wa Uchumi na Mipango Dr mkubwa kuliko madaktari wote wa uchumi ambao Tanganyika iliwahi kuwashuhudia.Zikishachukuliwa wanagaiwa fedha kiduchu ambazo hazikidhi gharama za uendeshji wa HIFADHI zooooote.
Kifupi HIFADHI zote zipo hoi hakuna fedha ingawa zinaingiza fedha !.
High season ndio inaanza halafu HIFADHI hazina fedha ingawa zinatarajiwa kuingiza fedha.Barabara mbovu,madaraja mabovu,huduma mbovu,watumishi hawalipwi, hakuna miradi ya ujirani mwema halafu tunahimizwa kuipigia kura SERENGETI eti kivutio bora duniani !.
Mambo madogo madogo tunashindwa kuyafanya lipi tunaweza,hakika aliyetuliga waafrika sijui tumpatie nini aturejeshee akili na maarifa.
Tumezifanya hifadhi zetu sawa na halmashauri,hakika ni suala la muda tu hizi hifadhi zetu tutazizika wenyewe kwa kukosa maarifa kidogo ya kuziendesha zinavyotakiwa.
Ngongo kwasasa Seronera.