SERGIO CARLES BUSQUETS BURGOS

SERGIO CARLES BUSQUETS BURGOS

Messi Lionel

Senior Member
Joined
Jan 11, 2018
Posts
170
Reaction score
159
Wakati tunakua mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 tuliaminishwa na kaka zetu na baba zetu wa kisoka zaidi kwamba enzi za mfumo unaomtumia namba 6 kama mkabaji basi lazima namba 6 awe mtu mgumu(solid),mapafu ya mbwa na mwenye nguvu nyingi.

Ikafika wakati katika timu za watoto kipindi nacheza soka la ushindani kama umiseta,makombe ya mbuzi,Ndondo hata Copa cocacola kila mmoja alikuwa haipendi namba 6 kutokana na imani ya majukumu yake..
Niliona wachezaji kadhaa duniani waliocheza namba 6 ya kizamani kwa ufanisi mkubwa kama Roy Keane,Claude Makelele,Taribo West,Suleiman Matola,Ali Mayay na wengine wengi lakini kwa kipindi cha miaka ya karibuni bado niliendelea kuona mafundi walioweza kuitendea haki nafasi ya kiungo mkabaji(defensive midfielder) kama Yaya Toure,Gilberto Silva,Marcos Senna,Gennaro Gattuso,Thiago Motta,Michael Carrick,Michael Essien,Javier Mascherano hata Mara nyingi nilimuona mtu mgumu Javier Zanetti na Internazionale yake..

Baaada ya Msomali wa Uholanzi Frank Rijkaard kuipa mafanikio Barcelona ile ya utatu wa kawaida wa Ronaldinho Gaucho,Anderson De Souza(Deco) na Samuel Eto'o Fils aliondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Kocha aliyekuwa na kikosi cha Vijana(Barca B) Josep Pep Guardiola ambapo wote tunafahamu mapinduzi aliyoyafanya.

Wengi tuliokuwa mashabiki wa moja kwa moja Wa Gaucho tulimlaumu sana Pep lakini wale mashabiki wa viungo wakabaji walimshangaa sana Pep kwa Kwanza-kumchezesha Toure Yaya kama beki wa kati na baadaye kumuuza kabisa..

kafara zote hizo alizokuwa akifanyiwa tembo huyu wa cote d'voir ilikuwa ni kumpa nafasi kinda kutoka clinic ya soka ya Barceolona maarufu kama La Masia Sergio Busquets Burgos wengine kiutani walimwita biskuti hahahaa..

Japo alipandishwa kikosi kikubwa pamoja na wenzake kama Pedro Rodriguez,Bojan Krkic,Gerrard Piqué akitokea Manchester United lakini Sergio alibadilisha mtazamo wa watu wengi sana waliokuwa wanaitafsiri nafasi ya kiungo Mkabaji.

Siku ya kwanza namuona 2009 nilimuona kijana amevaa namba 16 mgongoni mwembamba,kapewa eneo la kiungo mkabaji katika fainal dhidi ya Manchester United na Man Utd walikufa 2-0 maholi ya Eto'o na Messi.
Kuanzia hapo nilianza kujiambia na kuwaambia wenzangu kuwa kwa mara ya kwanza naona toleo jipya la kiungo mkabaji(new version of defensive midfielder) ambapo jamaa hakuonesha sana matumizi ya nguvu sana lakini akionesha matumizi ya akili nyingi sana..

Akiwa amezaliwa July 16 1988 katika eneo moja linaloitwa Sabadell Huko Barcelona na akiwa pia ni mtoto wa gwiji na golikipa wa zamani wa Barcelona miaka ya 1990 Carles Bisquets alianza Kucheza soka lake katika timu za nyumbani(local clubs) kama CD Badia,Barbera Andalucia kabla ya kupelekwa timu B ya Barcelona mwaka 2007 na 2008 ndipo alipoitwa rasmi na Pep katika kikosi cha wakubwa..

Akiwa timu B alifanikiwa kumwezesha Guardiola Kuifikisha Barcelona B katika ligi daraja la 3 la hispania(La Tercera Divisíon)
Akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 2 jamaa ni mnyumbulifu(flexible) sana na ana uwezo mkubwa sana wa kuumiliki mpira na kuufanyia ujuzi anaotaka na katika mahojiano na vyombo vya Habari Gwiji la Ajax na Barcelona Marehemu Johan Cruyff aliwahi kukaririwa akisema," Jamaa anaonekana kama Veteran akiwa hana mpira na kwakuwa anagusa pasi moja na mbili tu(one-two passes) lakini kwa ujumla anavifanya vitu vigumu kuwa rahisi.

Amewahi kulalamikiwa na mashabiki wengi wa soka kwa kudanganya sana hasa kwa zile faulu ndogondogo na ye kuifanya kuonekana kubwa(diving),lakini ilikuwa ni mbinu ya kuisogeza timu yake mbele..
Tangu jamaa amejiunga na timu ya wakubwa mafenikiwa kushinda vikombe vya ndani(La Liga,Copa del Rey na Spanish Super cup) zaidi ya 8,mataji ya klabu Bingwa ulaya mara 3(2009,2011&2015) na katika hatua zote akiwa mtu muhimu katika kikosi.

Tangu alipoanza kuitwa katika timu ya vijana ya Taifa ya Hispania u-21 na baadaye mwaka mmoja mbele aliitwa kikosi cha wakubwa kwenda kuchukua nafasi ya mbrazil Marcos Senna aliyeluwa Villareal basi Sergio B16 amefanikiwa kupata Medali ya dhahabu ya Kombe la dunia pale kwa mzee Mandela,Euro 2012 Poland na Ukraine na akiwa sehemu muhimu ya Timu..

Akiwa na urefu ule amekuwa mzuri sana katika mapambano ya mipira ya Juu(Aerial duels),mzuri katika kucheza sehemu sahihi uwanjani anakaba sana,anaichezesha timu vema na mara nyingi sana amekuwa akifunga mabao muhimu kwa Barcelona..
Staili yake kuwa ni soka la pasi nyingi na ufundi mkubwa wa kuuchezea mpira..

Alikuwa katika vikosi vyote vya Barca vilivyoshinda mara mbili Vikomba vitatu kwa msimu mmoja(TREBLE) mwaka 2009 na 2015 akiungana na Dani Alves,Andreas Iniesta,Xavi Hernandez Creus,Lionel Messi,Gerrard Pique,Pedro Rodriguez..

Na Kocha wake Vicente Del Bosque kocha aliyewapa mafaniko sana Timu ya Taifa ya Hispania akiwa na Kombe la Dunia na La Ulaya aliwahi kusema "KAMA ANGEKUWA MCHEZAJI ANGEPENDA KUCHEZA KAMA BUSQUETS NA KAMA UNAIANGALIA MECHI NZIMA HUWEZI KUMUONA BUSQUETS LAKINI KAMA UNAMUANGALIA BUSQUETS UTAIONA MECHI NZIMA-if you see the whole game you can't find Sergio but if you find Sergio you can see the whole game..
Kwa kushinda Klabu Bingwa ulaya yeye na baba yake Carles Busquets jamaa anaungana na familia ya Maldini ambapo Baba Cesare Maldini na mwanae Paolo Maldini wamewahi kushinda ubingwa wa ulaya kwa nyakati tofauti wakiwa na timu moja..

Akiwa chini ya vivuli vya vya kina Messi,Xavi,Iniesta,Villa lakini niliwahi kutamani sana siku moja nikuandikie makala ya kutambua mchango wako katika burudani ya soka Sergio Busquets ..
Safi sana Sergio kwa Mapinduzi ya Namba 6 ya kizamani..
Tutakumbuka uwezo wako na kusifia kadiri inavyobidi..

[HASHTAG]#footballaddicted[/HASHTAG]
 
Safi sana, umechambua vyema kabisa bwana MESSI Mungu akubariki.

Binafsi sijaona namba 6 bora duniani kama Sergio Bosquets jamaa ni fundi.

  1. Sergio Bosquets
  2. Mascherano
  3. Zanetti
  4. Gattuso
  5. Gabriel Heinze huyu jamaa ailikuwa balaa.
    There are four types of defenders: centre-back, sweeper, full-back, and wing-back. The centre-back and full-back positions are essential in most modern formations. The sweeper and wing-back roles are more specialised for certain formations. though kizazi hiki most of them hawamjui vizuri
  6. Yaya toure hii nayo ni mashine
  7. Marcos senna...
 
Kuna siku nliwah kukutana na mnaz mmoja wa chelsea baada ya draw ya Uefa akimlinganisha busquet na Ngolo kante. Sababu alizokua anazitoa ni kwamba ngolo ana nguv nyingi na anakaba sana. Nlimwambia tu km umefikia kuwa na hyo laana ya kumlinganisha Ngolo na Busquet ni heri nikuache tu.
 
Wakati tunakua mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 tuliaminishwa na kaka zetu na baba zetu wa kisoka zaidi kwamba enzi za mfumo unaomtumia namba 6 kama mkabaji basi lazima namba 6 awe mtu mgumu(solid),mapafu ya mbwa na mwenye nguvu nyingi.

Ikafika wakati katika timu za watoto kipindi nacheza soka la ushindani kama umiseta,makombe ya mbuzi,Ndondo hata Copa cocacola kila mmoja alikuwa haipendi namba 6 kutokana na imani ya majukumu yake..
Niliona wachezaji kadhaa duniani waliocheza namba 6 ya kizamani kwa ufanisi mkubwa kama Roy Keane,Claude Makelele,Taribo West,Suleiman Matola,Ali Mayay na wengine wengi lakini kwa kipindi cha miaka ya karibuni bado niliendelea kuona mafundi walioweza kuitendea haki nafasi ya kiungo mkabaji(defensive midfielder) kama Yaya Toure,Gilberto Silva,Marcos Senna,Gennaro Gattuso,Thiago Motta,Michael Carrick,Michael Essien,Javier Mascherano hata Mara nyingi nilimuona mtu mgumu Javier Zanetti na Internazionale yake..

Baaada ya Msomali wa Uholanzi Frank Rijkaard kuipa mafanikio Barcelona ile ya utatu wa kawaida wa Ronaldinho Gaucho,Anderson De Souza(Deco) na Samuel Eto'o Fils aliondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Kocha aliyekuwa na kikosi cha Vijana(Barca B) Josep Pep Guardiola ambapo wote tunafahamu mapinduzi aliyoyafanya.

Wengi tuliokuwa mashabiki wa moja kwa moja Wa Gaucho tulimlaumu sana Pep lakini wale mashabiki wa viungo wakabaji walimshangaa sana Pep kwa Kwanza-kumchezesha Toure Yaya kama beki wa kati na baadaye kumuuza kabisa..

kafara zote hizo alizokuwa akifanyiwa tembo huyu wa cote d'voir ilikuwa ni kumpa nafasi kinda kutoka clinic ya soka ya Barceolona maarufu kama La Masia Sergio Busquets Burgos wengine kiutani walimwita biskuti hahahaa..

Japo alipandishwa kikosi kikubwa pamoja na wenzake kama Pedro Rodriguez,Bojan Krkic,Gerrard Piqué akitokea Manchester United lakini Sergio alibadilisha mtazamo wa watu wengi sana waliokuwa wanaitafsiri nafasi ya kiungo Mkabaji.

Siku ya kwanza namuona 2009 nilimuona kijana amevaa namba 16 mgongoni mwembamba,kapewa eneo la kiungo mkabaji katika fainal dhidi ya Manchester United na Man Utd walikufa 2-0 maholi ya Eto'o na Messi.
Kuanzia hapo nilianza kujiambia na kuwaambia wenzangu kuwa kwa mara ya kwanza naona toleo jipya la kiungo mkabaji(new version of defensive midfielder) ambapo jamaa hakuonesha sana matumizi ya nguvu sana lakini akionesha matumizi ya akili nyingi sana..

Akiwa amezaliwa July 16 1988 katika eneo moja linaloitwa Sabadell Huko Barcelona na akiwa pia ni mtoto wa gwiji na golikipa wa zamani wa Barcelona miaka ya 1990 Carles Bisquets alianza Kucheza soka lake katika timu za nyumbani(local clubs) kama CD Badia,Barbera Andalucia kabla ya kupelekwa timu B ya Barcelona mwaka 2007 na 2008 ndipo alipoitwa rasmi na Pep katika kikosi cha wakubwa..

Akiwa timu B alifanikiwa kumwezesha Guardiola Kuifikisha Barcelona B katika ligi daraja la 3 la hispania(La Tercera Divisíon)
Akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 2 jamaa ni mnyumbulifu(flexible) sana na ana uwezo mkubwa sana wa kuumiliki mpira na kuufanyia ujuzi anaotaka na katika mahojiano na vyombo vya Habari Gwiji la Ajax na Barcelona Marehemu Johan Cruyff aliwahi kukaririwa akisema," Jamaa anaonekana kama Veteran akiwa hana mpira na kwakuwa anagusa pasi moja na mbili tu(one-two passes) lakini kwa ujumla anavifanya vitu vigumu kuwa rahisi.

Amewahi kulalamikiwa na mashabiki wengi wa soka kwa kudanganya sana hasa kwa zile faulu ndogondogo na ye kuifanya kuonekana kubwa(diving),lakini ilikuwa ni mbinu ya kuisogeza timu yake mbele..
Tangu jamaa amejiunga na timu ya wakubwa mafenikiwa kushinda vikombe vya ndani(La Liga,Copa del Rey na Spanish Super cup) zaidi ya 8,mataji ya klabu Bingwa ulaya mara 3(2009,2011&2015) na katika hatua zote akiwa mtu muhimu katika kikosi.

Tangu alipoanza kuitwa katika timu ya vijana ya Taifa ya Hispania u-21 na baadaye mwaka mmoja mbele aliitwa kikosi cha wakubwa kwenda kuchukua nafasi ya mbrazil Marcos Senna aliyeluwa Villareal basi Sergio B16 amefanikiwa kupata Medali ya dhahabu ya Kombe la dunia pale kwa mzee Mandela,Euro 2012 Poland na Ukraine na akiwa sehemu muhimu ya Timu..

Akiwa na urefu ule amekuwa mzuri sana katika mapambano ya mipira ya Juu(Aerial duels),mzuri katika kucheza sehemu sahihi uwanjani anakaba sana,anaichezesha timu vema na mara nyingi sana amekuwa akifunga mabao muhimu kwa Barcelona..
Staili yake kuwa ni soka la pasi nyingi na ufundi mkubwa wa kuuchezea mpira..

Alikuwa katika vikosi vyote vya Barca vilivyoshinda mara mbili Vikomba vitatu kwa msimu mmoja(TREBLE) mwaka 2009 na 2015 akiungana na Dani Alves,Andreas Iniesta,Xavi Hernandez Creus,Lionel Messi,Gerrard Pique,Pedro Rodriguez..

Na Kocha wake Vicente Del Bosque kocha aliyewapa mafaniko sana Timu ya Taifa ya Hispania akiwa na Kombe la Dunia na La Ulaya aliwahi kusema "KAMA ANGEKUWA MCHEZAJI ANGEPENDA KUCHEZA KAMA BUSQUETS NA KAMA UNAIANGALIA MECHI NZIMA HUWEZI KUMUONA BUSQUETS LAKINI KAMA UNAMUANGALIA BUSQUETS UTAIONA MECHI NZIMA-if you see the whole game you can't find Sergio but if you find Sergio you can see the whole game..
Kwa kushinda Klabu Bingwa ulaya yeye na baba yake Carles Busquets jamaa anaungana na familia ya Maldini ambapo Baba Cesare Maldini na mwanae Paolo Maldini wamewahi kushinda ubingwa wa ulaya kwa nyakati tofauti wakiwa na timu moja..

Akiwa chini ya vivuli vya vya kina Messi,Xavi,Iniesta,Villa lakini niliwahi kutamani sana siku moja nikuandikie makala ya kutambua mchango wako katika burudani ya soka Sergio Busquets ..
Safi sana Sergio kwa Mapinduzi ya Namba 6 ya kizamani..
Tutakumbuka uwezo wako na kusifia kadiri inavyobidi..

[HASHTAG]#footballaddicted[/HASHTAG]

Ila hii yote ni jeuri ya Guardiola kuwa na mtazamo wa kipekee kabsa na uthubutu wa aina yake. Angekua kocha mwingne angekomaa na Toure pale Barca mpka kieleweke ila aliona kwamba kwa mfumo wake hafai. Ndio maana kuna wakat naanza kuona Fernandinho hana maisha maref pale city. Kuna mtu ataletwa kila mmoja wetu atashangaa na atatuziba midomo.
 
Safi sana. Ningeomba ututajie sifa za namba sita sahihi na majukumu yake. asante mkuu!!
 
Mkuu sifa zoote hizi kumbe unasifia BISKUTI??!!🙂
 
Back
Top Bottom