Series bora ulizowahi kuangalia

1. IRIS
2. City Hunter
3. Kitu Warriors Turkish Drama (Savasci),yenye subtitles za kiingeleza mbona balaa wazeee!!!!
 
1. Tehran
2. Fauda
3. Hit and Run
4. Dark Desire 1 & 2

Ova
 
Kama kwenye list yako hakuna BREAKING BAD na GOT nakushauri nenda kaangalie tena series. Bado hujaziona series kali aseeh
 
Season ya pili ya breaking bad waliibatiza 'better call saul'...nitaitafuta hiyo better call Saul maana inasifiwa sana
 
Ila Blacklist pamoja na The flashback kiboko ya pseudo science kudadek
Mkuu una uhakika the blacklist ni moto? Namalizia ku re-watch breaking bad nitaanza na hiyo aise.
 
Hobbit,lord of the rings ligend of the seeker, nikiwa teen nilizipenda ,nikiwa young adult nilipenda viking na GOT,walking in dead but now in early middle age tv ishakuwa pambo Tu. lakin bado naikumbuka seeker
Sasa hamia kwenye Playstation 5.
 
Sijabisha mkuu,nilikua sijui better call Saul ni series nyingine tofauti na breaking bad, nimesema season 2 breaking bad waliita better call Saul,ambaye ni lawyer

Yani Breaking Bad na Better Call Saul ni series mbili tofauti,Breaking bad inaonyesha zaidi maisha ya Walter White na Jesse Pinkman kwenye uhalifu wao hadi wanakuja kumchukua Saul kama lawyer wao kuwatetea.

Ukirudi kwenye Better Call Saul hii inaonyesha maisha ya Saul Goodman kabla ya kukutana na Walter White na Baada ya pale,inshort hii series inaonyesha hustle za Saul hadi anakuwa wakili na vikwazo alivyopitia toka kwa kaka yake ambaye alikuwa lawyer tayari.Lakini pia utaona jamaa anavyo hustle kufungua ofisi yake ya uwakili na kutafuta wateja,ila mwishoni mwa Series itaonyesha event zilizotokea baada ya Breaking Bad kuisha.
 
FROM hii ni horror ila ndio iko season 2 season 3 nasikia inatoka nov inavutia kiasi chake
 
Binafsi serie bora niliyopata kutazama mpaka sasa nitasema The Blacklist kwa sababu hizi:
Kwanza ni uhusika wa Bwana Mkubwa Raymond Reddington humu ndani huyu jamaa ameonesha ukweli wa namna magenge ya uhalifu yanavyofanya kazi kwa kushirikiana na vitengo vya kiusalama, ukitazama kuanzia season ya kwanza mpaka season ya sita utajikuta umeanza kuelewa mfanano na muunganiko wa magenge mbalimbali.
Pia suala la Raymond kutaka kufanya kazi na Binti Elizabeth Keen huku mumewe Lizzy akiwa ni miongoni mwa wahalifu wakubwa tu, Raymond anakwenda kumfichua Tom Keen na kuharibu uhusiano wake na Elizabeth.
Halafu kuna muziki wa kutosha kutoka kwa Mzee Baba Dembe. Aisee yaani season 10 za The Blacklist kwangu ndo bora zaidi.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…