Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
Tukiendelea kufuata ushauri wa wataalamu kipindi hichi kigumu dunia inachopitia, ukiachana na vitu vyote ushauri muhimu wanaotoa wataalamu ni kukaa nyumbani na kutulia ili kujilinda wewe pamoja na familia yako na ukitoka nje usiache kuvaa barakoa (mask) kwa usafi na kufuata taratibu za kiusalama unapovaa na kuvua na kuepuka mikusanyiko mikubwa ya watu.
Sasa basi tukiendelea kutimiza hili kubwa la kukaa ndani kila mtu anafanya lake kusogeza siku mbele hadi hali itakapokuwa shwari. Muziki na filamu ndio burudani ya wengi kipindi hiki. Mimi filamu ndio burudani yangu, kipindi hiki nimepata kufuatilia series nyingi sana tofauti na hali ilipokuwa kawaida sasa hivi mambo machache muda mwingi. 😅 hizi ndio series ninazofuatilia hadi sasa;
Itaewon Class (JTBC)
Hii ni Korean drama; ina episodes 16, nipo ya 14. Ninachoipenda ni jinsi watu wanavyoshindana kibiashara bila kutishiana uhai, story kali sana ipo kitofauti sana.
Home Before Dark (Apple TV)
Hii inamuhusu mtoto wa kike anayependa kazi ya uandishi wa habari anaejaribu ku-solve kesi ya utekaji mtoto iliyotokea miaka kibao iliyopita kwenye mji aliokulia baba yake na wanaoishi. Ina episodes 10 nipo ya 7.
Unsolved: The Murders of Tupac & The Notorious B.I.G (USA Originals)
Hii kila episode ninayoangalia sichoki, kuyaona mambo yaliyotokea miaka ya 90 na wahusika kufanana na Tupac na Biggie Smalls na jinsi walivyovaa uhusika inazidi kunogesha hili picha. Napenda pia jinsi wanavyoweka na clip halisi za matukio yaliyotokea kipindi cha mauaji ya hawa ma-legend.
Marianne (Netflix)
Aisee hii ndio naianza kabisa, nipo episode 1. Humu ndani ni kisanga kwa wale wapenda horror tunakaa humu.
Narcos (Netflix)
Plata O Plomo (Silver or Lead) pamoja na hii kitu kutoka kitambo sana, niliwahi kuicheki online kama dakika 7 hivi nikaacha, ila sasa hivi naiwekea kambi. Pablo na madawa yake, madawa na Pablo wake. Humu ni cocaine tu. Ndio naanza S01E01.